Tundu Lissu, vita na Wasafi hutoiweza, utagalagazwa wewe na chama chako

Alichosema Lissu ndio kweli.
Diamond ndio walewale walioishi ktk unafiki na uzandiki mtupu, kamwe mie siwezi kumuunga mkono mnafiki.
Lazima mkubali uhuru na haki ya kila mtu kuchagua anachopenda na kuamini anachoamini.

Lissu aliamini tukipigania madini yetu tutapelekwa mahakamani za kimataifa JPM aliamini tunaweza kupambana na wazungu na tukagawqna kinachopatikana. Kila mtu aachwe aamini anachoona sawa.

Mnachofanya Chadema ni kama waliompiga risasi Lissu kwa sababu ya kutofautiana mitazamo.
 
Chama hakina ajenda zaidi ya kudandia trending issues hata zisizo na mashiko. Chadema hawapendi kukosolewa JPM nafuu! Hivi makamu mwenyekiti anaingia kwenye malumbano ya akina Diamond kweli?

Hawa kwao kikwazo si alikuwa mwendazake? Sasa watakuwa exposed jinsi wasivyo na ajenda.
Yani Lisu anataka kutwambia kwamba kwa vile kina Roma wapo chadema basi wana ccm wasiwaunge mkono kwenye mziki wanaoufanya.
 
View attachment 1806668
Lissu nakushauri kabisa achana na habari za Diamond maana vita yake hauiwezi. Diamond anafanya sanaa na anawapa watu burudani.

Team Wasafi ni jeshi kubwa na likishambulia linashambulia kama waveitnamu.

Yeye kuchagua chama cha CCM chama cha watoto wa mjini, kosa lake mpaka wewe na wafuasi wako wa Chadema kumshambulia mitandaoni ni lipi?
Mnahubiri haki ila haki ya wenzenu kuchagua wanachopenda hamuitaki...Huu mbona ni udikteta sasa, siku mkipewa nchi watu wasiounga mkono chama chenu hakuna rangi wataacha ona hapa hamna polisi hamna jela ila mnataka kila mtu aamini mnachoamini kwa mabavu akiwa tofauti ni adui.

Beyonce alimpigia Hillary Clinton kampeni za kufa mtu ila Trump akachukua nchi , Trump akumgeuza Beyonce adui wala Republican hawakuanzisha vita na Beyonce kwanza full unyamwezi yani Beyonce support bila kujali vyama.

Lissu na viongozi wa huko dizaini yako mnafanya vijana wa kisasa wasivutiwe na Chadema. Yani kwa kifupi mnatuonyesha nyie sio watu poa, kwenu huko ni vurugu, visasi, ukamanda, usela nnya ndio umejaa mpo so harsh 😖😖 mnayafanya maisha kama kitu kigumu sana.

Huyo Ney wenu mnaemsifia mkumbuke jina halisi ni Elibariki wa kule kule sasa kwa nini asiwe Chadema.
Ili ni onyo Lissu fanya siasa zako na kina Polepole achana na Wasafi kama unahitaji kuungwa mkono na watoto wa mjini.
Lissu vs chadema haiwezi humiza kichwa na media ikiwemo Wasafi ,bland ya CHADEMA inajitosheleza ,media uchaguzi 2020 zilikua mfukoni mwa mwendazake ila bado ccm chin ya mwendazake ukweli wa mziki wanaujua,na mungu anajua

Sasa Wasafi KWA Chadema kitu gani , au kipi chadema itegemee toka kwenu, walitimuliwa TBC kwenye MKUTANO wa kampeni na bado Mambo yakaenda sembuse Wasafi, Chadema ikiamua inaweza anzisha izo Wasafi hata mia hacheni jitutumua wakati hamna effect yoyote kwa lissu na Chadema
 
Chama hakina ajenda zaidi ya kudandia trending issues hata zisizo na mashiko. Chadema hawapendi kukosolewa JPM nafuu! Hivi makamu mwenyekiti anaingia kwenye malumbano ya akina Diamond kweli?

Hawa kwao kikwazo si alikuwa mwendazake? Sasa watakuwa exposed jinsi wasivyo na ajenda.
Sidhani kama umewahi kuzitafuta agenda za Chadema ukazikosa, google utazipata.

Kwahiyo Lissu asitoe maoni yake kwasababu Diamond kahusika! wacha ushamba.
 
Alichosema Lissu ndio kweli.
Diamond ndio walewale walioishi ktk unafiki na uzandiki mtupu, kamwe mie siwezi kumuunga mkono mnafiki.
Kwahiyo songi za akina Roma ziskilizwe na chadema ila wana ccm na ADc sio? Munaingiza ushamba kwenye mambo ya siasa halafu ssiem inawaitia mnasema wameiba, cdm hamjitambui

Baada ya sukuma gang
Mko na Diamond award
Who is next?
Ni Madikteta

Lema Godbless my rolemode washauri hawa jamaa zako hata kisirisiri.

Wanaweza tumia neno hayo ni maoni ya watu binafsi sio chama. Au twiter Republic tu.
 
View attachment 1806668
Lissu nakushauri kabisa achana na habari za Diamond maana vita yake hauiwezi. Diamond anafanya sanaa na anawapa watu burudani.

Team Wasafi ni jeshi kubwa na likishambulia linashambulia kama waveitnamu.

Yeye kuchagua chama cha CCM chama cha watoto wa mjini, kosa lake mpaka wewe na wafuasi wako wa Chadema kumshambulia mitandaoni ni lipi?
Mnahubiri haki ila haki ya wenzenu kuchagua wanachopenda hamuitaki...Huu mbona ni udikteta sasa, siku mkipewa nchi watu wasiounga mkono chama chenu hakuna rangi wataacha ona hapa hamna polisi hamna jela ila mnataka kila mtu aamini mnachoamini kwa mabavu akiwa tofauti ni adui.

Beyonce alimpigia Hillary Clinton kampeni za kufa mtu ila Trump akachukua nchi , Trump akumgeuza Beyonce adui wala Republican hawakuanzisha vita na Beyonce kwanza full unyamwezi yani Beyonce support bila kujali vyama.

Lissu na viongozi wa huko dizaini yako mnafanya vijana wa kisasa wasivutiwe na Chadema. Yani kwa kifupi mnatuonyesha nyie sio watu poa, kwenu huko ni vurugu, visasi, ukamanda, usela nnya ndio umejaa mpo so harsh 😖😖 mnayafanya maisha kama kitu kigumu sana.

Huyo Ney wenu mnaemsifia mkumbuke jina halisi ni Elibariki wa kule kule sasa kwa nini asiwe Chadema.
Ili ni onyo Lissu fanya siasa zako na kina Polepole achana na Wasafi kama unahitaji kuungwa mkono na watoto wa mjini.
Mungu mwenyewe mwanzilishi wa mfumo wa demokrasia ametupa uhuru wa kumfata au lah,kwanini mnalazimisha kila mtu amchague Diamond, huo ndiyo udikteta uchwara, amesema mapenzi hayalazimishwi hivyo ni haki yake na demokrasia kumpigia ampendaye siyo lazima diamond na ameweka vigezo vyake anampa mtu mpenda kupigania haki, msilazimishe watu ninyi lumumba
 
Kwahiyo Lissu asitoe maoni yake kwasababu Diamond kahusika! wacha ushamba.
Mkuu maoni ya Lisu ndio maoni ya chadema.

Unapotaka kuleta u diamond kwenye chama huo ni ushamba pia.
 
Lissu vs chadema haiwezi humiza kichwa na media ikiwemo Wasafi ,bland ya CHADEMA inajitosheleza ,media uchaguzi 2020 zilikua mfukoni mwa mwendazake ila bado ccm chin ya mwendazake ukweli wa mziki wanaujua,na mungu anajua
Sasa Wasafi KWA Chadema kitu gani , au kipi chadema itegemee toka kwenu, walitimuliwa TBC kwenye MKUTANO wa kampeni na bado Mambo yakaenda sembuse Wasafi, Chadema ikiamua inaweza anzisha izo Wasafi hata mia hacheni jitutumua wakati hamna effect yoyote kwa lissu na Chadema
Nakuhurumia kwa sababu haulijui jeshi halisi la Wasafi ni kina nani. Labda kama Lissu Hana mpango wa kugombea tena urais. Kama ungelijua jeshi nalolizungumzia ungeskitikia chama chenu.
 
Mkuu maoni ya Lisu ndio maoni ya chadema.

Unapotaka kuleta u diamond kwenye chama huo ni ushamba pia.
Sioni tatizo kwenye hiyo comment ya Lissu, tena katumia lugha nzuri sana, na kusema maoni ya Lissu ndio maoni ya Chadema sijui walikaa kikao wapi wakaamua hivyo, wacha ushamba.

Above all, Lissu ana haki yake kikatiba kutoa maoni yake kwenye jambo lolote, msitupigie makelele hapa.
 
Mungu mwenyewe mwanzilishi wa mfumo wa demokrasia ametupa uhuru wa kumfata au lah,kwanini mnalazimisha kila mtu amchague Diamond, huo ndiyo udikteta uchwara, amesema mapenzi hayalazimishwi hivyo ni haki yake na demokrasia kumpigia ampendaye siyo lazima diamond na ameweka vigezo vyake anampa mtu mpenda kupigania haki, msilazimishe watu ninyi lumumba
Udikteta ni kusema mchagueni yule maana huyu hayuko kwenye chama chetu.

Huo ni upumbavu kwa sababu diamond ana mashabiki wake ambao ni wanachadema pia!

Ndio maana ccm huwa inawagonga kila uchaguzi sababu ya mambo ya hovyo kma haya.
 
Lissu vs chadema haiwezi humiza kichwa na media ikiwemo Wasafi ,bland ya CHADEMA inajitosheleza ,media uchaguzi 2020 zilikua mfukoni mwa mwendazake ila bado ccm chin ya mwendazake ukweli wa mziki wanaujua,na mungu anajua
Sasa Wasafi KWA Chadema kitu gani , au kipi chadema itegemee toka kwenu, walitimuliwa TBC kwenye MKUTANO wa kampeni na bado Mambo yakaenda sembuse Wasafi, Chadema ikiamua inaweza anzisha izo Wasafi hata mia hacheni jitutumua wakati hamna effect yoyote kwa lissu na Chadema
Sisi washabiki wa Ney ambao tuko sisiem tunaomba.
MUONGOZO tafadhali
 
Mim napenda sana songs za Diamond za kipindi hicho

Very touching songs...Ila hizi za siku hizi za paka mate iteleze, Mara nasafisha mtaro, mara alichokupa mama kwa kweli nikiwa home nawaonea aibu WATOTO na wadogo zangu.

Aondoe lugha za kuchochea ngono /sex abakie kwenye kuchochea mapenzi/love Kama mwanzoni

Kwangaruu wimbo mzuri Sana ukiondoa vineno ngonoka alivyochomeka diamond
Kwani anayo elimu ya kutofautisha mapenzi na ngono? Huyo mtu elimu aliyonayo ni ya mitaani. Alijifunzia Tandale kwenye ngono, unategemea nini? Angalia kundi lote hilo la wasanii ni watu wa aina gani ndo utajua umuhimu wa elimu badala ya kipaji.

Hapo sasa, hata wanasiasa tunahitaji wenye elimu na kipaji. Siyo mtu kukosa aibu anahangaisha nchi nzima eti ni mwanasiasa, bila hata elimu.
 
Back
Top Bottom