Tundu Lissu, vita na Wasafi hutoiweza, utagalagazwa wewe na chama chako

Yani wangepewa nguvu ya dola kila mtu angekuwa Chadema kwa lazima na wimbo wao wanasema ni upande wa haki usipowaelewa basi wewe unapinga haki ushighulikiwe
 
Tangu lini umekua mshauri wa mh Tundu lissu na Chadema ,? Wanachama wa chadema wakigawanyika kisa sijui nani uliemtaja,si ndo vizuri ccm inazidi kuimarika Sasa shida yako ipo wapi tena mkuu
 
Me nadhani sasa ni wakati chadema iachane na siasa za ki che Guevara na ianze kufanya siasa za kimfumo.. siasa za kiarakati zimepitwa na wakati,hata mbowe nilimsikia anasema hivyo.Hizi siasa za Kiki na kusafiri na upepo zinaidumaza chadema,maana hili la diamond ashinde,asishinde ila nalo litapita na chadema itabaki pale
 
Nakuhurumia kwa sababu haulijui jeshi halisi la Wasafi ni kina nani. Labda kama Lissu Hana mpango wa kugombea tena urais. Kama ungelijua jeshi nalolizungumzia ungeskitikia chama chenu.
Siku zote unapokuwa adui wa haki tambua kuwa kila binadamu anapenda haki na anathamini uhuru wake na ule wa wengine, hivyo hats uwe na jeshi, jeshi hilo ndilo lotakalo kuangamiza.
 
Naunga mkono hoja.
P
 
Utakuta hata Lisu nae ana mawazo mfu kama haya akilini mwake!

Wasafi siyo ile tv na redio tu!

Wasafi ni kundi la mashabiki ambao wameea nchi nzima, hao wana impact maana ni wapiga kura na wengine wako huko chadema.

Sasa kwa akili kama hizi ccm inashindwaje kuwagonga kwenye box la kura?
 
Hao ndio huwa wanaipa ccm ushindi ila kwa akili zako na kina Lisu unaona hawana impact
Ushindi wapi bana hamjawahi kujitambua njaa tupu, kifupi hawana issue wawape tu mpaka watakapo jotambua siku moja.
 
Tangu lini umekua mshauri wa mh Tundu lissu na Chadema ,? Wanachama wa chadema wakigawanyika kisa sijui nani uliemtaja,si ndo vizuri ccm inazidi kuimarika Sasa shida yako ipo wapi tena mkuu
Lisu tulimuonya toka anatoka ubelgiji na mimi binafsi nilisema hatapata zaidi ya 20% ya kura zote.

Huwezi ukabeba mtu toka ubelgiji eti awe ndio anakupigania uwe rais kisha watz wakuelewe!

Sasa hapa amejiingiza kwenye ligi za akina diamond bila kujua diamond ana mashabiki wake wapo huko chadema pia.

Umbumbumbu wa siasa huu
 
Siku zote unapokuwa adui wa haki tambua kuwa kila binadamu anapenda haki na anathamini uhuru wake na ule wa wengine, hivyo hats uwe na jeshi, jeshi hilo ndilo lotakalo kuangamiza.
Kwako wewe haki ni kitu gani? Haki ni kuwa shabiki wa chadema basi?
 
Hillary clinton alipigiwa kampeni na black community ya Marekani hadi na watu kama Michelle Obama maana Trump alionekana kama mtu mbaguzi wa rangi. Hivyo kuona black celebrity akiungana na Blacks wenzie kama alivyoungana nao katika kampeni ya Black Lives Matter

sio kitu cha ajabu kama Burna boy, wizkid, Tiwa Savage, Yemi alaide, Simi na Davido etc walivyofanya kipindi wanapinga uonevu wa polisi nchini Nigeria. They were with their people kama Miriam makeba au Yvonne chakachaka alivyosimama na watu Weusi wenzie kipindi cha Apartheid pasipo kujalisha maslahi yao binafsi ya kisanaa au kibiashara

"HIKI KITU DIAMOND HANA, DIAMOND ANAJALI BIASHARA ZAKE NA HAWEZI KUFANYA CHOCHOTE KITAKACHOHARIBU BIASHARA YAKE YAANI ATAISEMA SERIKALI PALE ITAPOGUSA MASLAHI YAKE BINAFSI, HATA HILI LA BASATA LA JUZI LILIKUWA LINAMHUSU ILA AKAACHA WASANII WENZIE WAMPIGANIE, INSHORT HUO UZALENDO DIAMOND HANAAAA"

Binafsi sipigi kura na hata ningepiga ningempigia Diamond cause sina baya nae na ninaelewa anapigania biashara zake ila wanaompinga pia wana point yao ya msingi the same way black communities zilimjia juu Kanye west alipojifungamanisha na Trump. Heshimuni mawazo yao
 
Nakuhurumia kwa sababu haulijui jeshi halisi la Wasafi ni kina nani. Labda kama Lissu Hana mpango wa kugombea tena urais. Kama ungelijua jeshi nalolizungumzia ungeskitikia chama chenu.
Nguvu na umoja wa umma ndo kila kitu Sasa chama Kama Chadema kipo katika imani za watu au umma,unaanzia wapi itishia na Wasafi mkuu, Lissu ata akipitishwa na chama gombea bland yake vs ya chama inatosha hapaitajiki Wasafi kupata ushindi bali Tume huru basi,
 
Washauri wa Diamond hawakutimiza wajibu wao, huyu bwa mdogo anajiharibia sana kujikomba komba kwa CCM, mwanamziki bora ni yule anayesiamamia HAKI na si kujikomba komba kwa watawala !! hapo si kuwagawa tu watanzania na mashabiki wake ila bali anakosa credits !!

Lissu upo sahihi.
 
Tundu Lissu na Chadema walishashindwa mengi.Baada ya uchaguzi mwaka 2015 walihamasishana kutosikiliza nyimbo wasanii wa bongo,wakafeli na matokeo yake Diamond akazidi kupasua anga.

Walishawahi kuhamasishana kugomea laini za voda matokeo yake wao ndio wamezidi kuzinunua.

Sasa hivi wanatangaza kutoshiriki uchaguzi wowote lakini watashiriki chini ya hii hii NEC.

Tundu Lissu na chama chake sio relevant tena,webaki kupiga ramli.

Tundu Lissu yupo chini sana ukimlinganisha na Diamond.
 
Beyonce alimfanyia kampeni Hillary.

Lil Wayne alimfanyia kampeni Trump.

P Didy alimfanyia kampeni Obama.

Tokeni huko gizani nyie Chadema msikifanye chama cha walugaluga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…