Tundu Lissu, vita na Wasafi hutoiweza, utagalagazwa wewe na chama chako

Wachukueni ccm sie hatuwataki ,mbona unalazimisha Mambo ,aendelee nao na wamfuate huko ccm Kama 2020 walivyo mfuata uliona wapi chadema ikimpigia MAGOTI,
 
Ushindi wapi bana hamjawahi kujitambua njaa tupu, kifupi hawana issue wawape tu mpaka watakapo jotambua siku moja.
Sasa usiwe unatoka ubelgiji mbio mbio na kuzunguka nchi nzima kuomba kura kwa wasiojitambua na wenye njaa.
 
Yaani TZ bhana mtu akiwa chama fulani basi anataka kila mtu awe mfuasi wa hicho chama, sasa ni nini maana ya Demokrasia.

NB; Tusipende kuchanganya siasa na vitu vingine kama mpira na music, binafsi naona mh. amefeli sana.
 
Kwa hiyo Lisu nae akitaka kuja kuomba kura hahitaji kura za wana ccm, act, cuf ila ni za chadema tu?

Akili mgando hizi
 
Alichosema Lissu ndio kweli.

Diamond ndio walewale walioishi ktk unafiki na uzandiki mtupu, kamwe mie siwezi kumuunga mkono mnafiki.
ni kweli kaka unalolisema - wewe ni kama mimi - wanafiki nafiki na mimi ni mbali mbali kabisa.
 
Mkuu hivi unafahamu maana ya Demokrasia kweli, sasa wote tukiwa chama kimoja (upinzani) kuna haja gani ya kuwa na mfumo wa vyama vingi.??
 
Watu wa siasa mnakuwaga vipofu sn[emoji16]..sasa wewe unamkosoa mleta mada wakati nawe umerudia hichohicho..

Km ni demokrasia sasa ni Kwa nn na nyie wanachadema mnawalazimisha watu Kwa kuwaambia wasimpigie Kura diamond?hapo Uhuru wa kuchangia upo wapi,si ni udikteta huohuo mlioupingaga enzi hizo

Mkuu,km hujui kinachoendelea Ila umekomenti Tu baada ya kuona huu Uzi ni kwamba diamond yeye amekuwa nominated na BET,Ila huko Twitter wafuasi wa chadema ndy wanaotumia nguvu kubwa kushawishi watanzania wasimpigie Kura diamond..sasa niambie huo Uhuru unaouongelea hapa ni upi?
 
Wachukueni ccm sie hatuwataki ,mbona unalazimisha Mambo ,aendelee nao na wamfuate huko ccm Kama 2020 walivyo mfuata uliona wapi chadema ikimpigia MAGOTI,
Hata wakati anapiga kampeni tulitoa ushauri hakusikia ila watu kama nyie ndio akawasikiliza matokea yake akambulia 18%
 
Mungu hapendi uongo na dhuluma,that,s mmeyaona mliyoyaona bado mpaka kila mshiriki wa dhuluma atubu,
Ukweli wa mungu na mungu anajua,ccm 2020 hamkushinda, Sasa kanusha mbele ya mungu wako unaemuabudu ,
 
Hivi Samia akienda sehemu akatoa maoni ya jambo flani hayawi maoni ya tz?

Lisu angekuwa na akili hiyo ligi angeachia watu wajinga kama hao kina JACOB wa ubungo ila kwa kuwa nae ndio wale wale ndio hivyo tena.
 
Kwa hiyo Lisu nae akitaka kuja kuomba kura hahitaji kura za wana ccm, act, cuf ila ni za chadema tu?

Akili mgando hizi
Kama akigombea tena inabidi aulizwe hili.

Imefika hatua watu wajielewe sasa, siasa zimewashinda wanataka waiaribu na tasnia ya music, ambayo watu wachache wameipambania sana hadi hapa ilipo..
 
Kila binadamu na malengo yake, si lazima kila msanii apiganie haki kiuanaharakati. Huyu kijana inawezekana malengo yake ni kupata mafanikio kifedha na si kuwa mwanasiasa au mwanaharakati ila wanasiasa wanatumia mafanikio yake aliyoyapigania kwa jasho kufikia alipofika. AIBU.

Wakati unafikiri kuhakikisha kuwa hafanikiwi Jambo ambalo hulifikiri ni kuwa huyu kijana anaongelewa kwa sababu amechaguliwa kugombea hizo tuzo. Kwa umri wake ameshafanikiwa kimziki, hata asipoipata wengine wataendeleza alipoishia.
 
Naelewa vizuri huko twitter bwana Reel Haule analazimisha watu wote wampigie kura Diamond kigezo eti ni mtanzania mwenzetu, Lissu na vijana wa chadema wanasema hawampi wala kumuunga mkono kwa vigezo siyo mpigania haki za watanzania na kushiriki kupigia kampeni watesi wao, ni sahihi kwani lazima wampigie demokrasia ni kuchagua mtu mwenye vigezo unavyotaka siyo kushinikizwa na mtu kwa sababu eti uzalendo
 
Hata mimi ni raia wa kawaida tu, lakini sijawahi kumuunga mkono Diamond Platinum...

Na unajua nini eti..?

Yeye na Mwendazake mungu wao ni mmoja, walikuwa wanalelewa na madhabahu moja...

Asipobadilika na kuachana na ibada za mashetani na kumwabudu Mungu wa kweli, Yehova atamfuata Kanumba na Magufuli walipo
 
kama huna akili huwezi kuelewa lakini kama una akili utaelewa.
π™·πš’πšŸπš’ πšπ™Ύπ™Όπ™° 𝚊𝚞 π™½π™΄πšˆ πš πšŠπš•πš’πš πšŠπš‘ πš”πšžπš πšŠ πš—πš˜πš–πš’πš—πšŽπšπšŽπš πš‘πšžπš”πš˜ π™±π™΄πšƒ?
 
Mkuu haya yanayoendelea ki ukweli yana sikitisha sana.....lakini mtu unaogopa kuchangia maoni yako ambayo unajua yatakwenda kinyume na utashi wao kwa kuwa utaambulia matusi ya nguoni......

UKWELI NI KWAMBA CHAMA CHA SIASA KINAPOACHANA NA AJENDA ZA KIMSINGI ZA KITAIFA KINAELEKEA KUBAYA.......
 
Wanachohubiri demokrasia ni tofauti na matendo yao. Kuchagua chama ni haki ya mtu, anataka watu wote wawe chadema? Huyu jamaa ashakuwa compromised na hawezi tokea akawa raisi wa tz.
 
Uvumilivu wa kisiasa ndo tatizo, ila msanii anaweza kuchukua mlengo wowote wa kisiasa au kukosoa bila bughudha kwa sababu ni haki yake. Sasa wasanii wenye mlengo mwingine wanapokosoa na kuanza kushushiwa rungu zito hapo ndo kunakuwa na walakini.
 

Ungeanzia definition (tafsiri) ya nini maana ya kushambulia ili kujiridhisha kuwa huo ndiyo ulio msingi wa hoja yako.

Haiyumkiniki unabwaja bwabwaja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…