Tundu Lissu, vita na Wasafi hutoiweza, utagalagazwa wewe na chama chako

Lissu hajaongelea masuala ya uchama hapo ila alichokiongea yeye ni kwamba huyo Diamond kuwa upande wa watesi na uovu bila kulaani. Kutokana na ufuasi wake na heshima yake hapa nchini Diamond alipaswa kuwa mstari wa mbele kulaani vitendo viovu vya watawala au basi ingekuea bora kutokuonesha upande wowote kama labda aliogopa kufilisiwa.
 
Wanachohubiri demokrasia ni tofauti na matendo yao. Kuchagua chama ni haki ya mtu, anataka watu wote wawe chadema? Huyu jamaa ashakuwa compromised na hawezi tokea akawa raisi wa tz.
Lisu ametoa maoni yake ni haki yake..na wala hajasema anataka kila mtu awe chadema..heshimuni hilo.
 
Kamjibu huko TWITTER,pili natumai hujamuelewa kabisa LISSU alichomaanisha.
 
Ukisikiliza za kanisan itakua bora....hayo maisha mema wengne hatuyatak..nchi lazima iwe na ladha buana..sasa tuanze kuhubiriana kanisan..nako mtaan iwe hvyo hvyo...ni sawa yule mbunge aliemsemea mwenzie..yaan wanataka wanawake sjui wavaeje...nchi ikiwa na visheria ving inakua haina ladha
 
Wasafi ni jeshi kubwa ! unataka kumtisha nani ? Jeshi kubwa limeshindwa kummaliza Harmonize !

Ni hivi , Kila mtu ashinde mechi zake , Utaratibu ni ule ule Kale ulikopeleka Mboga .
 
Naseeb alijiaribia kwa nani? Kwa Lissu? Si mlifanyaga kampeni Zuchu asichukue Afrimma mbona aliipata au hamjipimagi ushawishi wenu mnaropoka tu!
Wewe bila shaka ni mtu duni sana kichwani , hivi nani kakwambia kuna mtu anahangaika na mtu kama Zuchu ?
 
Kutetea haki hakuna chama we mama
 
Wasafi ni jeshi kubwa ! unataka kumtisha nani ? Jeshi kubwa limeshindwa kummaliza Harmonize !

Ni hivi , Kila mtu ashinde mechi zake , Utaratibu ni ule ule Kale ulikopeleka Mboga .
Nawashangaa wanaCCM eti wanataka wote tumuunge mkono mwanaCCM wao domo kaya. Kwani alipokuwa akinengua jukwaani na JIWE hakujua kuwa wasanii wanapaswa kutokuwa na upande wa kisiasa ili waungwe mkono na wote? Upande waliouchagua waende huko wataungwa mkono huko.
 
Ukiona haueleweki kwa namna nyepesi basi rudi nyuma ujitafakaari.
Utaelewekaje kwa namna nyepesi kwa vichwa panzi kama vya wanaCCM? Huwezi toa hoja ikaeleweka kwa watu kama ninyi. Mlihudhuria tu shule lakini hakuna kilichoingia kichwani.
 
Kwa kweli jamaa amebaki kuwa wa hovyohovyo tu. Kiongozi wa chama cha siasa unalazimisha kila mwana muziki awe chama chako. Demokrasia ipi wanayotutangazia sasa. Kwa kweli wamebaki wanadandia mada za hovyo hovyo tu. Mond akikosa tuzo yeye inamsaidia nn?
 
Lissu kasema yeye binafsi hatampigia kura Diamond. Wewe umeigeuza vita. Beyonce unayemsema hajawahi kusita kutetea haki za jamii yake Marekani. Album yake ya Lemonade na kwenye Super Bowl 50 aliwaenzi Black Panther. Yuko active kwenye mapambano kuliko hata mume wake. Alimpigia kampeni Hillary kwa sababu ya imani yake kuwa Hillary angewatendea haki watu weusi. Ingawa Trump alishinda uchaguzi lakini Hillary alimshinda kwa kura zaidi ya milioni tatu.
Watu wengi wanampinga Diamond kwa sababu ya ukimya wake katika masuala ya haki za raia wenzake. Kuwakumbatia bila kificho watu kama Makonda ambao wengine walimuona kama anahusika katika dhulma dhidi yao. Hii kumtetea kuwa yeye ni entertainer tu ndio mnamuharibia kabisa maana mnasema yeye ni mamluki asiyekuwa na imani kabisa. Mtu mwenye msimamo alipaswa kutetea mapenzi yake kwa chama alichochagua na sio kujifanya kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya pesa.
Mpigieni kura na mfanyieni campaign mtu wenu lakini msilazimishe wengine wampigie kura. Wasiomtaka nao wana haki ya kufanya campaign dhidi yake. Mwisho wa siku wapiga kura ( ambamo watanzania ni wachache sana) ndio watakao amua.

Amandla...
 
Mtafanya nini nyinyi Chadema sana sana mnazidi kupoteza watu wenye akili maana wanaona kama genge la machokoraa tu halina ustaarabu fujo mizuka chuki ndio mtaji wenu sio ushawishi.
sawa mwana lumumba, utajonea.
 
Nimesikitika sana na baadhi ya coment kwenye huu uzi.
.
Coment nyingi zina reflect mitazamo ya watu wanavyoona vichwani mwao na kwa coment hizi, Tanzania bado sana
.
Kwa ufupi tu tanzania haikustaili kuwa nchi huru ilibidi iwe inawatwalia tu mpaka sasa pengine akili zetu zingkuwa mbali sana tofauti na sasa..
 
maisha ya wanadamu wengi waliofanikiwa walijipendekeza huo ndio ukweli
chunguza utaona
kama unabisha angalia mkeo anaogopa simu ya nani kati ya yakwako na boss wake? au wewe simu ya boss wako na baba yako
 
Wewe inaonekana huelewi hata hicho unachokipinga. Unachokipinga ndiyo unachounga mkono.

Lisu amesema hamuungi mkono Diamond kwa sababu alizozitaja. Kwani hana huo uhuru wa kufanya hivyo? Unazungumzia uhuru wa kila mtu kuamua anachokitaka alimradi havunji sheria, halafu unataka kila mtu amuunge mkono Diamond.

Demokrasia ni kumuacha kila mtu aunge mkono au asiunge mkono. Huku ndiyo kuheshimu maamuzi na matakwa ya mtu yasiyo kinyume na sheria. Tundu Lisu amefanya maamuzi yake. Kwani amekulazimisha wewe nawe ufanye au uamini kama anavyoamini yeye?

Humu JF tupo tunaounga mkono maamuzi mengi ya Rais Samia, na wapo wanaopinga. Kama Rais anapingwa, Diamond ni nani hata asipingwe na yeyote?

Hata kama ikatokea wengi wakawa wanuunga mkono Diamond, na wachache wakawa wanampinga,bkwani hiyo inaondoa haki ya hao wachache wanaompinga kuamini wanachokiamini?

Usipende udikteta wa kumlazimisha kila mtu afikiri na kutenda kama utakavyo wewe. Anayepinga au anayemuunga mkono ana haki ya yeye kuamua anachotaka kutokana na anavyoamini, na ana haki ya kuwashawishi wengine pia ili wakubaliane na fikra zake, siyo kosa.
 
Kama kuna link yeyote ya kumchagua diamond tumeni hapa tumchague , huyu ni MTZ mwenzetu bhana bila kujali itikadi zake.
Kosa linalofamywa na chadema ni kurely only na vijana na watu wa kaskazini tu na kusahau kuwa kuna vijana pia watanzania nje ya kanda hiyo ambao ni wengi zaidi, sidhani upinzani wa aina hii utaweza kutwaa madaraka nchini, tutaishia kuimia kila mwaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…