Tundu Lissu: Vyombo vya Usalama haviwezi kujichunguza, Tume ya Kijaji inaripoti kwa Rais, njia halali ni kuleta Wachunguzi wa Kimataifa

Tundu Lissu: Vyombo vya Usalama haviwezi kujichunguza, Tume ya Kijaji inaripoti kwa Rais, njia halali ni kuleta Wachunguzi wa Kimataifa

View attachment 3093238
Video hii ni kwa hisani ya On-line JAMBOTV;

Kwa ufupi:

TUNDU LISSU: Yanayoendelea Sasa hivi wanaokumbuka ni kama yaliyofanyika mwaka 2019 na 2920, utekaji, utesaji na mauji. Ni maandalizi ya ushindi wa wizi wa chaguzi zilizo mbele yetu kwa kutisha watu....

TUNDU LISSU: Huyu mama ni kama Magufuli anaongoza watu walewale, wauaji walewale, watesaji walewale. Hii ndiyo tabia na mtindo wa watawala madikteta wote duniani ya kuua na kuteka na kutesa Ili kulinda nafasi zao za utawala. Hakuna sababu nyingine yoyote ya mauaji haya, bali yote haya yanadanyika ili kina Samia na wenzake wabaki kilaini madarakani....

Haka kama mama nako ni kadikteta tu, hakana tofauti na madikteta wengine wote duniani...

TUNDU LISSU: Tutakomesha mauaji haya kwa wananchi kuweka pressure ndani ya nchi na pressure toka jumuiya ya kimataifa. Wakipigwa pressure watakoma na watafanya yawapasayo kufanya.....

TUNDU LISSU: 4Rs za huyu mama ni uongo zilipoanzishwa, ni uongo sasa na leo, na ni uongo na ulaghai mtupu mpaka kesho....

##Kwa ufasaha na mapana tazama na sikiliza video hii ya takribani dakika 11 hivi

Karibu tena Tanganyika Mh. Tundu Lissu
Hiyo gari ya Lissu mbona kama ina matobo ya risasi?

Halafu wakati anahojiwa, hao jamaa waliosimama pembeni yake ndo walinzi wake au?

Labda kama walikuwepo zaidi ya hao.

Lakini kama ni hao wawili tu, basi walisimama kizembe sana.

Hamuwezi wote mkawa mnaangalia mbele tu halafu nyuma hamuangalii.
 
Vijana hawa wata tawaliwa na madikteta kama wanasubiri mjomba Mbowe, Lissu au Heche wabadilishe nchi
 
Ni hivyo tu si vinginevyo. Well said Lissu!

Opposition tumieni hii oppportunity vile balozi zimezungumza mna green light mwanzo mwisho. Fungueni kesi haraka.

Mbowe anasema eti iundwe tume na .., how n why?
 
Hiyo gari ya Lissu mbona kama ina matobo ya risasi?

Halafu wakati anahojiwa, hao jamaa waliosimama pembeni yake ndo walinzi wake au...
Yes, hiyo gari ina matobo ya risasi....

Ni ile aliyopigwa nayo risasi ktk makazi ya viongozi Area D - Dodoma mwaka September 7, 2017...

Bado hajaibadilosha. Anatembea nayo hivyo hivyo...
 
Muda si mrefu nilikuwa naangalia TBC1 nilikuwa naangalia kipindi kilichohusisha watu kadhaa akiwemo Stevene Wasira na Hamad Rashid.

Kitu pekee kilichonisukuma niandike kabla maumivu kupoa ni maneno yao ambayo mengi yalionesha ukihoji kitu inaonekana unavuruga amani.

Naomba Wasira arejee MATUKIO kadhaa. Akina soka imesemekana walikamatwa na watu wanaosemekana ni polisi na bado kina Soka hawajulikani wako wapi!

Mzee Kibao inasemekana waliomshusha kwenye gari ni polisi.

Pia tukio la Chadema kukamatwa wote waliokuwa wanakwenda kwenye kongamano la vijana kwenye siku ya vijana duniani linatufundisha kitu.

Aliyesema vijana wa Tanzania waangalie vijana wa Kenya alikuwa mtu mmoja lakini Chadema yote ilihusishwa. Kwanini hawakumkamata aliyesema wakawakamata viongozi wote?

Kwa nn walifanya hivyo? Vivyo hivyo kama wameonekana polisi wakitenda kosa halafu hawajafafanua kati yao nani katenda unataka walaumiwe akina nani? Na kama wao ndo wa kulaumiwa wachunguzwe na nani? Angekuwa miongoni mwao wapo waliotajwa au kukamatwa, jeshi lisingetuhumiwa.

Wasira nakuomba Mzee wetu usiingize siasa kwenye maisha ya watu. Watanzania wote tunapenda amani ndiyo maana tunapenda uwazi. MATUKIO haya yametokea mara nyingi.

Kuna watu mpaka leo hatujui wako wapi na watarudi lini, polisi wako kimya. Na hasa asipopotea mtu mwenye jina hawasemi kama muda huu. Kuna kipindi ilisemekana kutekwa watu ni DRAMA.

Hivi kweli muda si mrefu uambiwe drama (maigizo) na muda si mrefu watu wanatekwa tena, mara muda si mrefu mtu anatekwa anakutwa amekufa.

Watu unataka wawaze nn, wawe na majibu gani! Serikali Wala polisi haiwezi kulaumiwa kukiwa na uwazi.

Mzee Wasira nakuomba uziache siasa za miaka ile. Sasa hivi ni vigumu kuwaficha mambo kama kipindi chenu ambacho hata taarifa za ajali zilikuwa zinaka baada pengine ya siku 2 au 3. Watu wa leo siyo wa mwaka 47.
 
Uwoga ni kanuni ya kwanza Kwa jeshi au askari. Askari lazima uwe muoga kwasababu askari usipokuwa na kanuni ya uoga upo uwezekano wa kuangamia...
Unashindwaje kuelewa kwamba mission zote za vyombo vyetu walizofanya miaka ya karibuni zimefeli na kuwaacha uchi? Mission zote ziko crystal clear kwamba vyombo hivyo vimehusika kwa 99%

1. Shambulio la Lissu.

2. Kutekwa kwa Sativa.

3. Kuuawa kwa huyu mzee.

Matukio yote haya yana viashiria vikubwa kwamba vyombo vimehusika.

Wakati mossad kidon shinbet nk vya israel vikifanya mission bila kuacha alama wala maswali sisi hawa wakwetu wanafanya mission hovyohovyo kiasi cha kuifedhehesha serikali na amiri jeshi. (magu na sasha) sasa katika mazingira haya utaviaminije vyombo vyetu vijichunguze vyenyewe?
Lissu yuko sahihi.
Bravo Tundu Lissu
 
TUNDU LISU NA MBOWE HAWAELEWANI WALA HAWAENDANI.
nashauri Lisu aanzishe chama chake chenye misimamo mikali. MBOWE amepowa sana.
 
Unashindwaje kuelewa kwamba mission zote za vyombo vyetu walizofanya miaka ya karibuni zimefeli na kuwaacha uchi? Mission zote ziko crystal clear kwamba vyombo hivyo vimehusika kwa 99%

1. Shambulio la Lissu.

2. Kutekwa kwa Sativa.

3. Kuuawa kwa huyu mzee.

Matukio yote haya yana viashiria vikubwa kwamba vyombo vimehusika.

Wakati mossad kidon shinbet nk vya israel vikifanya mission bila kuacha alama wala maswali sisi hawa wakwetu wanafanya mission hovyohovyo kiasi cha kuifedhehesha serikali na amiri jeshi. (magu na sasha) sasa katika mazingira haya utaviaminije vyombo vyetu vijichunguze vyenyewe?
Lissu yuko sahihi.
Bravo Tundu Lissu
Lisu yuko sahihi Kwa maoni yake lakini sisi sote tujiulize kwamba Rais na jeshi lake watakubali kushindwa?
Swali: nchi ina watu karibu milioni 64 harafu anayejua mambo na mwenye uthubutu ni lisu peke yake je, itawezekana vipi?
 
Back
Top Bottom