Tundu Lissu: Vyombo vya Usalama haviwezi kujichunguza, Tume ya Kijaji inaripoti kwa Rais, njia halali ni kuleta Wachunguzi wa Kimataifa

Hiyo gari ya Lissu mbona kama ina matobo ya risasi?

Halafu wakati anahojiwa, hao jamaa waliosimama pembeni yake ndo walinzi wake au?

Labda kama walikuwepo zaidi ya hao.

Lakini kama ni hao wawili tu, basi walisimama kizembe sana.

Hamuwezi wote mkawa mnaangalia mbele tu halafu nyuma hamuangalii.
 
Vijana hawa wata tawaliwa na madikteta kama wanasubiri mjomba Mbowe, Lissu au Heche wabadilishe nchi
 
Ni hivyo tu si vinginevyo. Well said Lissu!

Opposition tumieni hii oppportunity vile balozi zimezungumza mna green light mwanzo mwisho. Fungueni kesi haraka.

Mbowe anasema eti iundwe tume na .., how n why?
 
Hiyo gari ya Lissu mbona kama ina matobo ya risasi?

Halafu wakati anahojiwa, hao jamaa waliosimama pembeni yake ndo walinzi wake au...
Yes, hiyo gari ina matobo ya risasi....

Ni ile aliyopigwa nayo risasi ktk makazi ya viongozi Area D - Dodoma mwaka September 7, 2017...

Bado hajaibadilosha. Anatembea nayo hivyo hivyo...
 
Muda si mrefu nilikuwa naangalia TBC1 nilikuwa naangalia kipindi kilichohusisha watu kadhaa akiwemo Stevene Wasira na Hamad Rashid.

Kitu pekee kilichonisukuma niandike kabla maumivu kupoa ni maneno yao ambayo mengi yalionesha ukihoji kitu inaonekana unavuruga amani.

Naomba Wasira arejee MATUKIO kadhaa. Akina soka imesemekana walikamatwa na watu wanaosemekana ni polisi na bado kina Soka hawajulikani wako wapi!

Mzee Kibao inasemekana waliomshusha kwenye gari ni polisi.

Pia tukio la Chadema kukamatwa wote waliokuwa wanakwenda kwenye kongamano la vijana kwenye siku ya vijana duniani linatufundisha kitu.

Aliyesema vijana wa Tanzania waangalie vijana wa Kenya alikuwa mtu mmoja lakini Chadema yote ilihusishwa. Kwanini hawakumkamata aliyesema wakawakamata viongozi wote?

Kwa nn walifanya hivyo? Vivyo hivyo kama wameonekana polisi wakitenda kosa halafu hawajafafanua kati yao nani katenda unataka walaumiwe akina nani? Na kama wao ndo wa kulaumiwa wachunguzwe na nani? Angekuwa miongoni mwao wapo waliotajwa au kukamatwa, jeshi lisingetuhumiwa.

Wasira nakuomba Mzee wetu usiingize siasa kwenye maisha ya watu. Watanzania wote tunapenda amani ndiyo maana tunapenda uwazi. MATUKIO haya yametokea mara nyingi.

Kuna watu mpaka leo hatujui wako wapi na watarudi lini, polisi wako kimya. Na hasa asipopotea mtu mwenye jina hawasemi kama muda huu. Kuna kipindi ilisemekana kutekwa watu ni DRAMA.

Hivi kweli muda si mrefu uambiwe drama (maigizo) na muda si mrefu watu wanatekwa tena, mara muda si mrefu mtu anatekwa anakutwa amekufa.

Watu unataka wawaze nn, wawe na majibu gani! Serikali Wala polisi haiwezi kulaumiwa kukiwa na uwazi.

Mzee Wasira nakuomba uziache siasa za miaka ile. Sasa hivi ni vigumu kuwaficha mambo kama kipindi chenu ambacho hata taarifa za ajali zilikuwa zinaka baada pengine ya siku 2 au 3. Watu wa leo siyo wa mwaka 47.
 
Uwoga ni kanuni ya kwanza Kwa jeshi au askari. Askari lazima uwe muoga kwasababu askari usipokuwa na kanuni ya uoga upo uwezekano wa kuangamia...
Unashindwaje kuelewa kwamba mission zote za vyombo vyetu walizofanya miaka ya karibuni zimefeli na kuwaacha uchi? Mission zote ziko crystal clear kwamba vyombo hivyo vimehusika kwa 99%

1. Shambulio la Lissu.

2. Kutekwa kwa Sativa.

3. Kuuawa kwa huyu mzee.

Matukio yote haya yana viashiria vikubwa kwamba vyombo vimehusika.

Wakati mossad kidon shinbet nk vya israel vikifanya mission bila kuacha alama wala maswali sisi hawa wakwetu wanafanya mission hovyohovyo kiasi cha kuifedhehesha serikali na amiri jeshi. (magu na sasha) sasa katika mazingira haya utaviaminije vyombo vyetu vijichunguze vyenyewe?
Lissu yuko sahihi.
Bravo Tundu Lissu
 
TUNDU LISU NA MBOWE HAWAELEWANI WALA HAWAENDANI.
nashauri Lisu aanzishe chama chake chenye misimamo mikali. MBOWE amepowa sana.
 
Lisu yuko sahihi Kwa maoni yake lakini sisi sote tujiulize kwamba Rais na jeshi lake watakubali kushindwa?
Swali: nchi ina watu karibu milioni 64 harafu anayejua mambo na mwenye uthubutu ni lisu peke yake je, itawezekana vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…