Pre GE2025 Tundu Lissu: Walimu wasifanye kazi ya kusimamia Uchaguzi

Pre GE2025 Tundu Lissu: Walimu wasifanye kazi ya kusimamia Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kamanda, kama upo karibu na Mwenyekiti wako wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu, mwambie aje na mikakati ya kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa huru, wa haki na pia usio na wizi wa kura!

Kutoa matamko tu, tena yasiyo nguvu ya kisheria! haisaidii chochote! Hao walimu na watendaji wa Vijini/Kata, Bosi wao ni DED ambaye amepewa mamlaka na Tume ya uchaguzi kusimamia huo uchaguzi! Sasa katika hali ya kawaida, kuna mwalimu au mtendaji mwenye ujasiri wa kumkatalia Bosi wake akimu assign kazi ya kusimamia huo uchaguzi, na pia kuhakikisha ccm inashinda?

Anachotakiwa kufanya Kamanda Lissu kwa sasa ni kuangalia ni kwa namna gani serikali ya ccm itakubali uchaguzi kuwa huru na wa haki!! Na siyo kupiga tu kelele na kutoa matamko ya kufikirika. Watu wanataka vitendo! Na siyo maneno mengi.

Hakuna sheria inayosema uchaguzi usimamiwe na DED.
 
Lisu apunguze kuvuta bange
Unavyobugia wewe bangi, unadhani watu wote wapo hivyo? Watu wenye akili nzuri kama Lisu huwa hawagusi bangi. Mtu akiwa anabugia bangi anakuwa hana akili, sawa kama ulivyo wewe sasa hivi.
 
Ninamshukuru sana Lissu kwa kauli zake za kihuni zinazoongeza kura za CCM kwenye uchaguzi. Naanza kuona Yericko Nyerere alikuwa sahihi kusema Lissu hafai hata kuongoza tawi la CHADEMA ngazi ya kitongoji.

..kuna vijana wengi wamehitimu elimu ya juu wako mitaani wanaweza kutumika kusimamia uchaguzi.

..waalimu wao tayari wana ajira, sio sahihi wawanyime nafasi vijana wenye uhitaji zaidi wa fursa za kusimamia uchaguzi.
 
Lisu anaongea kimamlaka sana!na anajua hasa nini kinaendelea!yaani deep down ana baraka ya watanganyika waliopo CCM wanaohisi Sasa Mali zao zinauzwa na kizimkaz!

Tangu CCM ya mama iliposhindwa uchaguzi wa chadema Lisu kushinda ni dhahiri yeye ndio star wa siasa zetu!
Kwani ni mbali basiiii🤣 tusubiri
 
Mbona anafulia mapema hiviii......hana sera
 
..kuna vijana wengi wamehitimu elimu ya juu wako mitaani wanaweza kutumika kusimamia uchaguzi.

..waalimu wao tayari wana ajira, sio sahihi wawanyime nafasi vijana wenye uhitaji zaidi wa fursa za kusimamia uchaguzi.

Lakini Kusimamia uchaguzi siku 2 haifuti hali yao ya kukosa ajira
 
..Hata kusimamia uchaguzi ni fursa ambayo vijana wahitimu elimu ya juu wanaistahili, na wanapaswa kuichangamkia.
Fursa ya siku 1 haibadilishi maisha ya ukosefu wa ajira....
 
Fursa ya siku 1 haibadilishi maisha ya ukosefu wa ajira....

..siku moja vs siku sifuri.

..hata wakati wakipewa mafunzo ya taratibu za uchaguzi wanaweza kupewa posho.

..kuwatumia waalimu kusimamia uchaguzi ni kuwazibia fursa wahitimu wa elimu ya juu ambao hawana ajira.
 
Wakitoka hapo uchaguzini wanatudi mtaani kulala?? Wachangamke fursa zipo za kutosha mitaani
 
Wakitoka hapo uchaguzini wanatudi mtaani kulala?? Wachangamke fursa zipo za kutosha mitaani

..baada ya kusimamia uchaguzi vijana wanaweza kuchangamkia fursa nyingine zitakazojitokeza.

..jambo la msingi ni kuhakikisha hatuwazibii fursa vijana wetu waliohitimu elimu ya juu.
 
..baada ya kusimamia uchaguzi vijana wanaweza kuchangamkia fursa nyingine zitakazojitokeza.

..jambo la msingi ni kuhakikisha hatuwazibii fursa vijana wetu waliohitimu elimu ya juu.
Basi waanze kuzichangamkia leo hiii.
 
Back
Top Bottom