Tundu Lissu: Walimu wasisimamie uchaguzi

Tundu Lissu: Walimu wasisimamie uchaguzi

Hiki ndicho wanapaswa kufanya, vinginevyo wataishia kuwalaumu walimu ambao wenyewe (walimu) hawajui wafanye nini.
Walitakiwa pia watuulize watu ambao tunaishi vijijini, ili tuwape ABC's! Maana maeneo mengi ya vijijini vyama vingi vya upinzani haviweki mawakala!

Kinachotokea siku ya uchaguzi, ni CCM kwa kushirikiana na uvccm (tii ai esi wetu wa Bongo hawa), na policcm; ni kuwashinikiza walimu (wasimamizi wa uchaguzi) kuwajazia wagombea wao kura, zikiwemo kura hewa za sisi ambao hatushiriki hilo zoezi!!

Na kwa sababu hakuna wakala wa chama cha upinzani kuhakiki hizo kura, mgombea wa CCM anapata kura kiulaini tu.

Sasa kwa uzembe kama huu, Lissu anapata wapi ujasiri wa kuwahukumu walimu pekee! Na wakati hata vyama vyenyewe tu vya upinzani vinahusika kwa uzembe wa kutoweka mawakala wao katika vituo vyote vya kupigia kura!!!
 
Sio waoga, mkurugenzi ni mwajiri wao, wanaweza Je kukataa muongozo wao, hii ni Sawa na wakurugenzi kusimamia uchaguzi, wakati Raisi ndio boss Lao.. Wacha tuone kama hukumu Ya kesi ya Bob wang we iliyotolewa na mahakama ys Africa iliyokataa na juu Shauri serikali khbadili sheria ya uchaguzi na kuwa toa wakurugenzi itatejekezwa.
Fact hata mkurugenzi anatumika
 
Ni kweli kabisa walimu ni waoga Sana Mimi nakumbuka wakati wa semina ya Sensa idadi kubwa ya wanasensa walikuwa walimu, tulikuwa tunaangushwa Sana kwenye madai mtu mwezi mzima hatujalipwa mkitaka kutoa malalamiko mnakuwa wachache Sana walimu ndiyo kabisa walikua wanatuhimiza tuvumilie tukama kulipwa tutalipwa ni watu wa ajabu Sana wamejengeka kisaikolojia kuvumilia Sana Kama mtumwa hawalalamiki waoga wa mwisho ktk watumishi nahisi ni kutokana na neno mwalimu anatakiwa awe mfano na mwenye tabia njema kwenye jamii
Hhhahaha hawa watu waoga kama kasuku [emoji1787]
 
Kiukweli hii kada inashda sababu ni nying...
1. Weng wa walimu n kutoka familia maskin sana...kifikra na kiuchumi
2. Naunga mkono kwasababu ya protocol zao sjui n waoga sana kuchukua hatua mwalim anaweza kutembelewa na mkaguz wa kanda shulen sku hiyo hata mchana hatakula anatetemeka ...
3. Serikali kuna kipindi walikuwa wanachagua failure's ndoo wakasomee ualimu wale cream walikuwa wanaenda kupiga fani zenye mashko.

NB: nilialikwa kama mgen KAHAMA kumuaga mkuu wa shule flan hafla ilifanyikia sehem inaitwa NITESH aseeee jamaaa walimu wanagombana kisa soda na bia...nliondoka kabla hata nusu ya sherehe haijafka..
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mkuu soda mbali sana sisi Kuna sehemu tulienda kuwagawia pipi kifua hizi mbona walipigana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Apambane kwanza kuhakikisha Tume Huru ya Uchaguzi inapatikana kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na ule mkuu wa 2025! Asisahau hii Tume ya sasa, watumishi wake wote wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa!!

Hivyo tatizo la uchakachuaji wa matokeo kwenye uchaguzi, halisababishwi na walimu! Walimu hawatangazi matokeo ya uchaguzi! Walimu wanafanya kazi za Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa miaka mingi, na kwa uaminifu mkubwa!! Mbona hatusikii kelele za kutoka kwa wadau wa elimu?

Tatizo la kuchakachua matokeo kwenye uchaguzi linafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwaachia makada wa CCM (Wakurugenzi wa Halmashauri/Miji/Manispaa, nk pamoja na Wakuu wa Wilaya, Mikoa, nk kusimamia/kuingilia hilo zoezi!
Hujielewi wewe, kura zinaanza kuibiwa huku chini na wezi wakubwa ni walimu.. Punguani we
 
Wew ni mpu.mbavu nani kakufundisha huo ujanja kama siyo walimu,Nani alikuwa anahimiza kupiga dawa vyoo vyenu vya shuleni ulipokojoa kwenye sakafu
Elewa hoja yake acha kumshambulia, kasema walimu walipigana Kwa kugombania soda Sasa hapo yupi chizi
 
Yawezekana kabisa ulichosema ikawa kweli, hebu tuambizane hao ambao siyo waoga walisha fanya jambo gani la maana ambalo unaweza kusimama mbele ya watu ukasema kundi hili limefanya hiki kwa manufaa ya umma. Uchaguzi husimamiwa na Mkurugenzi niambie kama umefanikisha hilo la kumfanya asiwe msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la halmashauri yako, kama Hilo la kumuondoa Mkurugenzi ambaye unafahamu kabisa ni mteuliwa wa Rais limekushinda unataka walimu ndiyo waweze! Speaking of poverty, hata kuwa na mtazamo kama wako ni umaskini mkubwa kuliko umaskini wa kipato, kama walimu ndiyo Tanaka maskini kwa mtazamo wako basi tungekuwa tumezungukwa na matajiri. Don't vent your frustrations on teachers, don't make them a punching bag. Vipi wakati wanaengua wapinzani na CCM kupita bila kupingwa 2019 (Serikali za mitaa) na 2020 (general election), walimu ndiyo walihisika, ulifanya nini wewe kama wewe kama siyo kuufyata (pardon my french). Kama mnaamini walimu ndiyo sababu ya upinzani kushindwa then you have a long way to go.
Halafu eti walimu wanagombania soda! Nayo umeona great thinker uje utuandikie hapa.
Acha ujinga ipo hivi,, walimu huwa wanashiriki kwenye uwizi wa kura
 
Wala Mimi siyo Mwalimu, Ila imenikera sana kutukana walimu wote waliotufundisha na kutufikisha hapa tulipo, wew fikiria mtu ulikuwa hata hujui njia ya chooni, kamasi unapaka kwenye Shati, boxer huna Leo hii unaona hao watu ni wajinga, ukiona mtoto umeanza kumkashifu mzazi wako badala ya kumsaidia ujue akili yako bado haijakusaidia,busara ni kwamba unapaswa kumsaidia kama huwez kumsaidia muache usianze kumkejeli
Walimu ni wajinga tu kama wewe
 
Pole mwalimu ....umeandka vtu vng but..uliona mgomo wa kariakoo?? Shda kada inakuwa na watu inferior sana... Wanaoamin bila ualim hakuna maisha...na ndo mana weng maskin sana..... classmate wangu mmoja n mwalim wa primary huu mwaka wa 10 hana hata baiskeli ....jitahidin msiwe watu wa kutumiwa...japo mnaaminishwa mwajiri wenu ni DED sio kweli ....angalia leo zle tabulets ndoo mnakuja nazo had bar maana ile nayo imekuwa kama ID ya kumtambua mwalim NI LAZMA WALIMU WENGI MU CHANGE FIKRA ZENU...
Licha ya hivyo mwambie hata madaktar wamewahi kugoma
 
Unaweza kuoneaha wap walimu wametukanwa???? Nina marafk weng sana walimu...na hata ssta angu n mwalimu lkn ana life gumu munooo.....ukiona unajadiliwa ujue una tatzo sehem...walimu ku affiliate CWT na ccm n kawaida..walimu kutokuwa na umoja...walim wa leo kumwogopa mkurugez ...walim kuchomeana imekuwa kawaida lzm wabadilike...mimi bora mtoto wangu asomee hata ufugaji wa nyuki sio kada hii kwa Tanzania...
Upo sahihi kaka
 
Amesema walimu wote niwaoga wanatishwa na kuperekeshwa na wakurugenzi kuiba kura za wananchi .

======

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kabla ya Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ujao, kuna haja kufanya kila linalowezekana kubadili katiba ili kuwaondoa walimu kuusimamia.

Amesema mabadiliko wanayoyataka katika mfumo huo wa uchaguzi ni pamoja na kuhakikisha walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi.

Lissu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Shirati, mkoani Mara ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya chama hicho iliyopewa jina la Oparesheni +255#KatibaMpya inayofanywa na viongozi wakuu wa chama hicho nchi nzima.

“Pendekezo langu ni kwamba kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka ujao na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, tufanye lolote linalowezekana tubadilishe Katiba na mfumo wa uchaguzi.

“Kama tusipofanya linalowezekana kuhakikisha kwamba walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi tena kama ilivyo kwa nchi nyingine, na kama ambavyo imependekezwa na wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa ambao wanaangalia uchaguzi wetu, mjue kwamba uchaguzi huo utakuwa kama wa 2020.

“Tusipofanya linalowezekana kubadilisha Katiba na kuwa na Tume huru ya Uchaguzi badala ya hii iliyopo sasa, tujue yatatokea ya 2020. Tusipotengeneza sheria na Katiba inayokataza watu kupita bila kupingwa, mjue enguaengua haitoisha,” alisema.

Lissu alisema kudai Katiba Mpya pamoja na kubadilishwa mfumo wa uchaguzi ni jukumu la kila mtu na si la CHADEMA pekee.

“Lazima tulazimishe kufanyike mabadiliko katika eneo hili, na kama tusipolazimisha tumekwisha. Na hilo ni jukumu letu sote. Tutengeneze vuguvugu la kitaifa nchi nzima kuhakikisha hatuendi katika uchaguzi ujao bila Katiba Mpya.
Uchaguzi wa haki kabisa CCM haitoboi
 
Back
Top Bottom