Tundu Lissu: Walimu wasisimamie uchaguzi

Tundu Lissu: Walimu wasisimamie uchaguzi

Shda hawapendi kuambiwa ukwel wanaona tuna wa diss but ...life lao soo powa walio weng...nina jamaa angu yupo lake zone alikuwa headmaster hizi school mpya kawa mwalim wa kawaida kisa analala bar had anasahau j3 kwenda school...yaaan n full stresss..
Ukiona ticha ana gari basi ni vitz na IST nako spana mkononi [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Upinzani ni kujipanga from now na wasimamizi wao loyal nadhan kila kituo kikiwa na usimamizi mzuri na kura zikiwa nyingi mbona watashindwa kupindua matokeo ila wakiendelea kulialia ss watakua wanawaangalia uku wanagonga cheers
 
Walitakiwa pia watuulize watu ambao tunaishi vijijini, ili tuwape ABC's! Maana maeneo mengi ya vijijini vyama vingi vya upinzani haviweki mawakala!

Kinachotokea siku ya uchaguzi, ni CCM kwa kushirikiana na uvccm (tii ai esi wetu wa Bongo hawa), na policcm; ni kuwashinikiza walimu (wasimamizi wa uchaguzi) kuwajazia wagombea wao kura, zikiwemo kura hewa za sisi ambao hatushiriki hilo zoezi!!

Na kwa sababu hakuna wakala wa chama cha upinzani kuhakiki hizo kura, mgombea wa CCM anapata kura kiulaini tu.

Sasa kwa uzembe kama huu, Lissu anapata wapi ujasiri wa kuwahukumu walimu pekee! Na wakati hata vyama vyenyewe tu vya upinzani vinahusika kwa uzembe wa kutoweka mawakala wao katika vituo vyote vya kupigia kura!!!
Kwanini walimu wa kubali kujaza kura hewa?? What is wrong is wrong no matter Kuna ombwe kiasi gani
 
Sio waoga, mkurugenzi ni mwajiri wao, wanaweza Je kukataa muongozo wao, hii ni Sawa na wakurugenzi kusimamia uchaguzi, wakati Raisi ndio boss Lao.. Wacha tuone kama hukumu Ya kesi ya Bob wang we iliyotolewa na mahakama ys Africa iliyokataa na juu Shauri serikali khbadili sheria ya uchaguzi na kuwa toa wakurugenzi itatejekezwa.
Ww n falaaa sn jibu hoja unaleta hadith...za kichoko hapaa unagongwa ..kwann lisu hatak walim
..kwann walim wanazaraulika sn
..swala la kufundshwa sio hawa walim wa kileo mafala kama ww
we mjinga mmeulizwa yeye alipokuwa mbunge walisimamia akina nani? kwani hao akina lisu hawanaga mawakala kwenye vituo?
 
Haya ndiyo matatizo ya kuwa na jinsia isiyo eleweka. Uwezo wako wa kufikiri umekwisha kabisa.
Kwahiyo tuhuma juu ya walimu kuiba kura nizauwongo?? Nina majambazi wengi mitaani (walimu) wote husema waliiba kura Sasa wewe unaekaa Kwa shangazi yako hapo mwalimu wa shule ya Msingi mikuyuni unakula ugali wa wanafunzi umeshiba unakuja kututapisha apa, oya tetea wengine sio walimu, walimu ni majuha mapunguwani yaliyolaniwa
 
we mjinga mmeulizwa yeye alipokuwa mbunge walisimamia akina nani? kwani hao akina lisu hawanaga mawakala kwenye vituo?
Mpaka upinzani atangazwe basi ujue ccm wameiba kura na hazijatosha tena mpaka vurugu za wananchi zitokee vinginevyo huwa hawatangaziwi ushindi
 
Akili za walimu ndo kipimo cha uwezo wa kufikr wa hii nchi , ni kundi moja miyeyusho Sana Lina mindset za ajabu mno
Walimu ndio wamekufanya uweze kuandika neno "mindset" leo unawata waajabu mno! katiba hiyo iliyopo ni ibara gani imetamka kuwa walimu watasimamia uchaguzi?. Tusiwalalamikie walimu wakati vyama mbadala vinapata hela za ruzuku lkn haviwezi kuwalisha mawakala wao vituoni, kwanini wasirubuniwe na wenye fedha! Mnawagombea udiwani,kijiji, mtaa uchumi wao taaabani mnategemea kushinda na mfuko umetoboka?
 
Kwahiyo tuhuma juu ya walimu kuiba kura nizauwongo?? Nina majambazi wengi mitaani (walimu) wote husema waliiba kura Sasa wewe unaekaa Kwa shangazi yako hapo mwalimu wa shule ya Msingi mikuyuni unakula ugali wa wanafunzi umeshiba unakuja kututapisha apa, oya tetea wengine sio walimu, walimu ni majuha mapunguwani yaliyolaniwa
Wewe tayari umeshachanganywa na vile vifua vya akina Ali Kiba, Diamond Platinumz, na Harmonize! Siyo bure.
 
Walimu ndio wamekufanya uweze kuandika neno "mindset" leo unawata waajabu mno! katiba hiyo iliyopo ni ibara gani imetamka kuwa walimu watasimamia uchaguzi?. Tusiwalalamikie walimu wakati vyama mbadala vinapata hela za ruzuku lkn haviwezi kuwalisha mawakala wao vituoni, kwanini wasirubuniwe na wenye fedha! Mnawagombea udiwani,kijiji, mtaa uchumi wao taaabani mnategemea kushinda na mfuko umetoboka?
Walimu akili zao haziwatoshi ndio maana wote ni masikini, sijawahi kuona msomi akawa mwoga
 
nimeshiriki mambo ya kisiasa toka 2000 nilikuwa mpiga kura(nililazimisha japo umri ulikuwa haujatimia)95 nilifuatilia sana mgombea uraisi ambaye sikwenda kwenye mkutano wake walikuwa lipumba wa cuf ulifanyika mchana nilikuwa shule....mingine yote nilihudhuria siasa ikanichota mahaba upinzani (cdm)...nimeshiriki chaguzi wakala na usimamizi usaidizi vipindi tofauti wakati wa lowasa na wakati wa lisu.....wakati wa lowasa sikuona wameiba vip au kuna wizi sehemu gani..labda wawe wazembe kwenye kujumlisha huko wilayani au mkoani ila alishindwa kabisaaawapinzani walipigwa nje ya wanja..ushahidi kwenye sanduku....watu walishawishiwa kwa fedha au maneno usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura(hakuna wizi kwenya chumba).wakati wa magu sikuiingia ndani ya chumba nilikuwa na majukumu njee karani mungozaji...mwitikio wa watu ulikuwa mdogo sanaa(mnakumbuka ile hali kipindi hicho) kituo kilikuwa na wapiga kura 400 waliojitokeza kama 100 tu...na vituo vyote vilivyokuwa jirani hali ilikuwa hivyo....wengine hata hao 100 hawakufika kuna kituo jirani walipata watu76 kati ya 380... matokeo yalipotangazwa oviusly ccm ndio walikuja kupiga kura walishinda ila figure zikapikwa(ndio wizi niliouona) au udanganyifu... kama kweli mmepata wapiga kura na wamepiga na mna mawakala safi wizi unatokea wapi?
 
Amesema walimu wote niwaoga wanatishwa na kuperekeshwa na wakurugenzi kuiba kura za wananchi .

======

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kabla ya Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ujao, kuna haja kufanya kila linalowezekana kubadili katiba ili kuwaondoa walimu kuusimamia.

Amesema mabadiliko wanayoyataka katika mfumo huo wa uchaguzi ni pamoja na kuhakikisha walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi.

Lissu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Shirati, mkoani Mara ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya chama hicho iliyopewa jina la Oparesheni +255#KatibaMpya inayofanywa na viongozi wakuu wa chama hicho nchi nzima.

“Pendekezo langu ni kwamba kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka ujao na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, tufanye lolote linalowezekana tubadilishe Katiba na mfumo wa uchaguzi.

“Kama tusipofanya linalowezekana kuhakikisha kwamba walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi tena kama ilivyo kwa nchi nyingine, na kama ambavyo imependekezwa na wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa ambao wanaangalia uchaguzi wetu, mjue kwamba uchaguzi huo utakuwa kama wa 2020.

“Tusipofanya linalowezekana kubadilisha Katiba na kuwa na Tume huru ya Uchaguzi badala ya hii iliyopo sasa, tujue yatatokea ya 2020. Tusipotengeneza sheria na Katiba inayokataza watu kupita bila kupingwa, mjue enguaengua haitoisha,” alisema.

Lissu alisema kudai Katiba Mpya pamoja na kubadilishwa mfumo wa uchaguzi ni jukumu la kila mtu na si la CHADEMA pekee.

“Lazima tulazimishe kufanyike mabadiliko katika eneo hili, na kama tusipolazimisha tumekwisha. Na hilo ni jukumu letu sote. Tutengeneze vuguvugu la kitaifa nchi nzima kuhakikisha hatuendi katika uchaguzi ujao bila Katiba Mpya.
Kwa kikokotoo hiki. Tundu acha walimu wasimamie uchaguzi. Hiyo nimekuibia siri
 
Apambane kwanza kuhakikisha Tume Huru ya Uchaguzi inapatikana kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na ule mkuu wa 2025! Asisahau hii Tume ya sasa, watumishi wake wote wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa!!

Hivyo tatizo la uchakachuaji wa matokeo kwenye uchaguzi, halisababishwi na walimu! Walimu hawatangazi matokeo ya uchaguzi! Walimu wanafanya kazi za Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa miaka mingi, na kwa uaminifu mkubwa!! Mbona hatusikii kelele za kutoka kwa wadau wa elimu?

Tatizo la kuchakachua matokeo kwenye uchaguzi linafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwaachia makada wa CCM (Wakurugenzi wa Halmashauri/Miji/Manispaa, nk pamoja na Wakuu wa Wilaya, Mikoa, nk kusimamia/kuingilia hilo zoezi!
NECTA imewakataa walimu wa msingi kusimamia mtihani wa la saba. Hii necta Waliona mbali
 
Kuna wakati wapinzani wanahusika moja kwa moja na hiki kinachoendelea kwenye uchaguzi.

Kwanza wanatambua fika Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo siyo huru! Na inateuliwa na Mwenyekiti wa chama tawala! Lakini cha kushangaza hawagomei uwepo wa hii tume.

Pili, Wapinzani wanatambua fika wasimamizi wakuu wa huo uchaguzi ngazi ya Wilaya ni Wakurugenzi wa Halmashauri! Na ambao wote ni makada wa chama tawala! Na hawa wamepewa mpaka mamlaka ya kuwatangaza washindi (Madiwani na Wabunge)!!! Bado wameridhika tu!

Tatu, vyama vyote vya siasa vinatakiwa kuweka mawakala wao kwenye kila kituo cha kupigia kura! Lakini cha kushangaza hawa mawakala wa vyama vya upinzani utawakuta maeneo machache tu ya mjini! Ukienda vijijini, unakutana na mawakala wa chama tawala pekee! Sasa katika mazingira ya kizembe kama haya, utashindwa kweli kuibiwa kura!!!

Na badala ya kupigana dhidi ya adui wa kweli, wanakimbilia kwa walimu ambao wanafanya hiyo kazi ya usimamizi kwa maelekezo ya wasimamizi wakuu waliowateua (Wakurugenzi wa Halmashauri, na ambao ni makada wa chama tawala)!!!!! Kama siyo kichekesho ni nini hiki!!
Mkuu ni wewe au umepokonywa simu anatumia chizi?? Hujui mawakala wa upinzani huwa wanatolewa na polisi Kwa nguvu kwenye chumba cha kupiga kura?? Ukionekana hutaki rushwa unasimamia kura vizuri za upinzani zisiibiwe unaambiwa una vurugu unasukumwa nje, sasa kusema vituo vingi havina mawakala wa upinzani nakuona hujitambui
 
Amesema walimu wote niwaoga wanatishwa na kuperekeshwa na wakurugenzi kuiba kura za wananchi .

======

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kabla ya Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ujao, kuna haja kufanya kila linalowezekana kubadili katiba ili kuwaondoa walimu kuusimamia.

Amesema mabadiliko wanayoyataka katika mfumo huo wa uchaguzi ni pamoja na kuhakikisha walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi.

Lissu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Shirati, mkoani Mara ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya chama hicho iliyopewa jina la Oparesheni +255#KatibaMpya inayofanywa na viongozi wakuu wa chama hicho nchi nzima.

“Pendekezo langu ni kwamba kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka ujao na kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, tufanye lolote linalowezekana tubadilishe Katiba na mfumo wa uchaguzi.

“Kama tusipofanya linalowezekana kuhakikisha kwamba walimu na watumishi wengine wa serikali hawasimamii uchaguzi tena kama ilivyo kwa nchi nyingine, na kama ambavyo imependekezwa na wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa ambao wanaangalia uchaguzi wetu, mjue kwamba uchaguzi huo utakuwa kama wa 2020.

“Tusipofanya linalowezekana kubadilisha Katiba na kuwa na Tume huru ya Uchaguzi badala ya hii iliyopo sasa, tujue yatatokea ya 2020. Tusipotengeneza sheria na Katiba inayokataza watu kupita bila kupingwa, mjue enguaengua haitoisha,” alisema.

Lissu alisema kudai Katiba Mpya pamoja na kubadilishwa mfumo wa uchaguzi ni jukumu la kila mtu na si la CHADEMA pekee.

“Lazima tulazimishe kufanyike mabadiliko katika eneo hili, na kama tusipolazimisha tumekwisha. Na hilo ni jukumu letu sote. Tutengeneze vuguvugu la kitaifa nchi nzima kuhakikisha hatuendi katika uchaguzi ujao bila Katiba Mpya.
Walimu ni kundi oga sana ktk utumishi wa umma wanatumika na ccm kwa kuwa ni waoga na maskini wa kipato

Laiti wangejua nguvu yao tungeshapata ukombozi zamani
 
Back
Top Bottom