Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
14,624
Reaction score
20,666
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.

Hajaweka wazi nini haswa hoja yake. Ni kama mtu mwenye wasiwasi usiokwisha kwa vigezo vya mwanzoni mwa maongezi haya.

Inaweza kuwa ni muendelezo wa siasa za mitandaoni, hataki kutoka midomoni mwa watu kirahisi hivyo inambidi aongee hata kama anachokiongea ukikipima hakina undani sana.
 
Huyu bwana alishambuliwa kwa nia ya kumwua.

Kwa hakika angeweza kuuwawa.

Kauli kuwa upelelezi hauwezi kukamilika bila yeye kuwapo hazina ukakasi?
 
Huyu bwana alishambiwa kwa nia ya kumwua.

Kwa hakika angeweza kuuwawa.

Kauli kuwa upelelezi hauwezi kukamilika bila yeye kuwapo haina ukakasi?
Huyu bwana ni mlalamikaji wa kiwango cha PHD. Kama Rais kafunga safari mpaka Belgium na akataka waonane, ni lazima nia yake iwe ni njema.

Akumbuke kuwa rais ni taasisi yenye watu wengi nyuma wenye majukumu mbalimbali. Hivyo aondoe wasiwasi aliokuwa nao.

Kufariki kwa JPM kumaifanya taasisi ya urais iwe na mabadiliko makubwa. Aondoe shaka.
 
Ni jambo la kawaida kwa kila raia mwenye mashaka na usalama wake kutoa taarifa na kuhakikishiwa ulinzi kwa mujibu wa sheria.

Kuna ugumu gani kwa Mama Samia kama mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kumhakikishia mhanga huyu usalama wake kwa mujibu wa sheria?
 
Back
Top Bottom