Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Au na wewe Ni mtu assiyejulikana
 
Unasema tu wewe yangekukuta wewe au mzazi wako ungejua uchungu alionao lisu
 
...maongezi baina ya watu wawili walioafikiana yatakuwa siri .... siri sirini
 
Tundu Lissu kama ni muadilifu aseme fedha za stahiki zake ni shilingi ngapi? Na je akilipwa atazipeleka kwenye charity gani? Walitangazia ulimwengu wote wako watu walifanya chariy kumeet gharama zake baada ya serikali kuzuia hizo stahiki zake. Analazimika kwa uungwana tu hizo stahiki zake anazo idai serikali kuzirudisha kwenye charity.
 
Alafu unaweza hisi tangia apigwe risasi akuwai kurudi Tanzania,kumbe alirudi na akatembea nchi nzima kufanya kampeni tena huku akuchimba mikwara.

Waswahili husema, mzigo wa mwenzio kwako ni kama furushi la sufi.

Au hili ndiyo lile gunia la chumvi sasa wanaoliongelea waswahili ambako kwako ni furushi la sufi tu ndugu?
 
Kwa JWTZ siamini, jamaa walivyo vizuri kwenye harakati zao wasingefanya kama vile ilivyofanywa, kwa JWTZ wasingefanya mission kwa mtindo hule wa kiboya kwa kiwango kile.

Ila yote kwa yote alipangalo Mungu hakuna wa kuliziwia, alikusudiwa Lissu auwawe ila kalenda yake hakusoma siku hile.
 
Lissu yuko sahihi haiwezakani tunaenda mwaka wa 5 hakuna hata suspect mmoja wa tukio hili anashikiliwa na tanpol.

Ila tukaja kuambiwa Mbowe anapanga mipango kulipua vituo vya mafuta na kuua viongozi ilhali hakufanya hata kimoja wapo .

Sasa najiuliza intelligence gani iliweza kugundua mipango ambayo haijafanywa ila ikashindwa kuwakamata watu waliofanya tukio .

Hao hao wa ofisi hiyo waliwahi kujichanganya kwa kauli zao ambazo kwa wenye akili tuligundua ni mtu/watu gani walikua nyuma ya shambulio hilo kwa sababu za kisiasa.
 
Mlelewa Ubelgiji anatafuta kila mbinu ili aendelee kupewa hela na Amsterdam
Hili na mimi ndio nilikua nataka kulisema haya yote anazuga tu pesa ya ukimbizi ya bure keshaiona tamu kuliko kurudi bongo. Asiwasingizie watu ubaya kikosi cha kujumuisha TISS, JWTZ na polisi kingemtaka kisingetumia risasi 36 na atoke mzima. Hao jamaa wa kazi risasi mbili tu angekua sasa hivi jina lake linatanguliwa na marehemu. waliompiga risasi hawajui anabahatisha ila watakua ni wahuni tu waliotaka kuivuruga nchi. Lisu anatafuta scapegoat ya kutorudi bongo mjanja sana huyu wakili msomiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
mwambieni arudi nyumbani, kuna harufu ya vita huko ulaya.
 
Anayetafuta Kiki alishambiwa ili kuuwawa. Imewekwa wazi kuwa laiti angeuwawa washambuliaji wasingekaa wafahamike milele.

Anayetaka Kiki hapo nani? Wewe au yeye?
Lissu anatafuta legitimacy ya kuendelea kuishi ubelgiji na hakuna lingine hapo.

Kila siku story ya risasi, watu tulikwisha achana na huo ukurasa.

Kuna wengi walidhurika na wapo wanasonga na maisha yao bila hofu.

Hapa tatizo liko kwa kina Maria Sarungi na Fyatu karume wanao host hiyo the space na kumfanya mwenyekiti kila siku.

Mnatuchosha bhana!

Lissu na Lema ni kama nyuki daima sio wa kukumbatiwa.
 
Anataka kuhakikishiwa usalama dhidi ya watu wasiojulikana ili arejee nchini.
 
Anata apate kauli thabiti kwamba atakuwa salama akirejea nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…