Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Wanaomuita wanajua kaishashinda ndio maana wanatafuta sababu tu. IJP anasema afike polisi Kilimanjaro. Barua afike polisi kaenda maalumu hiyo yote ni mashinikizo.
Hakuwa na flyover, sgr sticker, vituo vya afya, madaraja,wala kushinda corona hata siku moja hakupiga goti kuomba kura. Sasa hivi vyote anavyo na kavinadi miaka mitano kwenye vyombo vya habari lakini kaona havimsaidii kaamua kupiga goti.
Mwenzie anasubiriwa mpaka giza na umati mkubwa wa watu. Pale hakuna msanii wa kutumbuiza zaidi ya mziki wa DJ. Pale watu hawazuiliwi kutoka kama kule ukiingia inakuwa mateka. Mgombea akianza hutuba foleni ya kutoka inaongezeka kwani wanajua ndio mwisho wa burudani.
Huku kwa Lisu kusudio la wananchi ni Lisu mwenyewe akiongelea kuhusu ustawi wao haki zao na maendeleo yao.
Mie ni mlemavu wa kufungulia TBC1 Lisu hana coverage kubwa lakini cha ajabu wananchi wanajaa kwenye mikutano yake.
 
Teavher kwenye hili tulia na kulifuatilia vizuri... gukizungumzia utii wa sheria raia hakuna aliye juu ya sheria hata mmoja.. kwahiyo tunaposimamia sheria basi tusimamie kisheria... ndio maana hata kama mtu akitenda jinai kama atasumbuliwa bila sababu wakati wa kukamatwa kwake polisi anakua amevunja sheria..

Kwa suala la Lissu polisi ndio wamenza kuvunja sheria jee wao wapo Juu ya Sheria?

Na je Mkuu ukipokea wito wa Polisi kutaka wakakuhoji kwa nini haumnunuliagi OCD bia, utaenda?
 
Yaani wewe ndiyo una mashaka na uanasheria wa Tundu Lissu, inadhuru nini?
Umesoma alichojibu Tundu Lissu au ulikiruka kwa kuwa haumpendi?
Amesema hivi;
Barua ya Polisi siyo wito wa kirafiki ni tamko la kisheria.
Hapo amekiri jinsi utendaji wa Polisi ulivyo na nguvu kisheria lakini ili nguvu hizo za kisheria za jeshi hilo ambazo limepewa na sheria, ziwe ngyvu kweli na halali, nalo linapaswa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
Unapomtaka aende, anaenda vipi? Aende kwa kufuata wito uliotolewa kinyume cha sheria? Wito wa Kirafiki?
 
Amkamate jiwe kwanza anayetishia wapiga kura huko tunduma
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Kwa sheria ipi wewe?Acha kukariri desturi za kigaidi za Polisi.Kwa hio wewe sa hivi askari anaweza kukuta tu uende kituoni kumsalimia?
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
lisu kawashika pabaya
 
Haijalishi sababu.Ni lazima hata polisi anapokukakamata akutamkie kosa lako.Haweza kukwambia Maelezo utakuta Polisi.Hawezi kukupotezea muda.Kama anataka kukuhoji anakufuata wewe mahali ulipo na kukuhoji na iwapo kuna sababu ya kukuweka kizuizini ndo anatafuta kibali cha kukukamata.Watanzania amkeni msiwe kama mbuzi kwenye banda.
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Weka kifungu cha sheria kinachosema hivyo, usilete uCCM hapa na udikiteita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…