Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Kuigomea polisi kufanya uchunguzi ni kinyume cha sheria; sasa sijui yeye ni mwanasheria gani. Wakati mwingine polisi wanaweza kutaka kukuhoji wewe kama shahidi kuhusu mtumhumiwa mwingine tofauti kabisa ambaye wanaweza kuwa na taarifa zake zaidi. Ni afadhali angejibu tu kuwa sasa hivi ratiba yake iko tight sana anaomba akutane na polisi katika muda mwingine siyo sasa kuliko kuweka jou hilo la kukaidi, kwani tayari ameshaweka ushahidi unaoweza kutumika dhidi yake; ndiyo maana nina mashaka sana na busara za Lissu pamoja na uanasheria wake. Hiyo kisheria ni kuizuia polizi kufanya kazi zake ammbalo ni kosa. Raia kuhojiwa na polisi ni sehemu ya majukukumu ya polisi kabla hawajamchukulia mtu hatua; yeye Lissu anaogopa nini kuhojiwa kama anajua yuko clean?
Wewe Kichuguu nakushauri ungeachana na mijadala inayohusisha Sheria na Siasa kwa kuwa huna uelewa then unajitutumua hovyo hovyo. Hapo juu umeandika pumba tupu.
 
Hebu ficha ujinga wako hapa, yani LISSU aogope kuhojiwa na hao form four failure.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Mwongo eti anaenda kukutana na mabalozi wakati anaenda kuhojiwa na tume ya maadili
Tume ya Maadili iko Dodoma Mabalozi bado wako Dar es Salaam ingawa Balozi zote zilipewa viwanja Dodoma mpaka leo haijulikani ngapi tayari zimehamia au zimeanza kujenga. Balozi nyingi hazipendi kujenga au zinaungana nyingi kujenga jengo moja ili nchi moja ikiamua kukatisha uhusiano na kufunga ubalozi jengo linaendelea kuwa la Balozi zilizobaki na ofisi zilizohamwa zinapangishwa kwa Ubalozi mwingine. Kuna Balozi nyingi zimejenga Dar haziwezi kujenga Dodoma itakuwa matumizi mabaya ya kodi za Raia wao. Rais wetu mpendwa kama kawaida alikurupuka kugawa viwanja kama njugu!
 
Ameandikiwa Mwenyekiti wake wa Chama. Sasa kama amfika hatua ya kukataa maagizo ya mwenyekiti wake wa Chama...Mh. Mbowe kama barua inavyomuelekeza mwenyekiti kufanya. Dharau kwa vyombo vyetu halali kisheria na kikatiba kama Polisi, ukweli zitamponza kisiasa. Acha aendelee 'kuota mapembe'!
 
Wewe Kichuguu nakushauri ungeachana na mijadala inayohusisha Sheria na Siasa kwa kuwa huna uelewa then unajitutumua hovyo hovyo. Hapo juu umeandika pumba tupu.
Mimi siyo mwanasheria wala mwanasiasa, lakini nina foundation nzuri sana kuhusu sheria kwa vile ninaishi mazingira ambayo ujuzi wa sheria ni wa muhimu sana. Kwa mfano polisi akikuwashia taa za rangi barabarani huwezi kukimbia ukidai kuwa hujaambiwa kosa lako; ukikimbia unakuwa umetenda kosa, na anaweza kukurushia risasa au kutafuta polisi wengine wakuzingire na hata kuangusha gari lako mtaloni kwani wakti huo tayari unakuwa ni mhalifu hata kama sababu waliyokuwa wanataka kukuuliza haikuwa inahusianiana na makosa yako binafsi. Simama umsikilize kwa nini kakuwashia taa za rangi, baada ya hapo ndipo uulizea uhalali wake kukusimamisha.

Polisi siyo mahakama, hawahukumu bali kazi yao ni kutafuta ushahidi, na raia anakuwa anavunja sheria kuwazuia polisi kutafuta ushahidi huo. Ukishashaingiza mambo ya sheria kwenye siasa basi unakuwa unapoteza watu wako, na pia kuvuruga jamii. hakuna uhusiano wowote kati ya sheria na siasa kwenye jamii timamu.
 
Tundu Lissu katika Ukurasa wake wa Twitter, ameweka Barua ya Polisi na kuandika Maneno haya "Wito wa polisi sio barua ya kirafiki, ni amri ya kisheria. Wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa. Barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama. Huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria. Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho."
View attachment 1587622
View attachment 1587514

Lissu kajiamdaa sana huku nje IGP usishangae Magu kanyamaza sana anaogopa mitego mikubwa ya mahakama, misaada hasa wakati huu wa kamera kila mahali. Familia zenu ndizo zitapata shida kama Makonda alivyokuwa hana kazi lakini ana zuio la familia nzima! Sasa msije kupelekwa na hao NEC kwenye makesi au vikwazo.

Na Zanzibar mwaka huu itawalipukia. IGP ujue unaweza ukababwikwa kesi ya kimataifa ikakusubiri mpaka utoke madarakani halafu serikali haitakuwepo kukutetea.
 
Polisi Tanzania, ilipokubali kutumika imeamua kujidhalilisha na kujiongezea chuki ya bure kabisa toka kwa wananchi!

Siro, Tanzania siyo CCM CCM pekee tumia akili hata kidogo! Unanunua kesi isiyokuhusu kabisa
 
Mimi siyo mwanasheria wala mwanasiasa, lakini nina foundation nzuri sana kuhusu sheria kwa vile ninaishi mazingira ambayo ujuzi wa sheria ni wa muhimu sana. Kwa mfano polisi akikuwashia taa za rangi barabarani huwezi kukimbia ukidai kuwa hujaambiwa kosa lako; ukikimbia unakuwa umetenda kosa, na anaweza kukurushia risasa au kutafuta polisi wengine wakuzingire na hata kuangusha gari lako mtaloni kwani wakti huo tayari unakuwa ni mhalifu hata kama sababu waliyokuwa wanataka kukuuliza haikuwa inahusianiana na makosa yako binafsi. Simama umsikilize kwa nini kakuwashia taa za rangi, baada ya hapo ndipo uulizea uhalali wake kukusimamisha.

Polisi siyo mahakama, hawahukumu bali kazi yao ni kutafuta ushahidi, na raia anakuwa anavunja sheria kuwazuia polisi kutafuta ushahidi huo. Ukishashaingiza mambo ya sheria kwenye siasa basi unakuwa unapoteza watu wako, na pia kuvuruga jamii. hakuna uhusiano wowote kati ya sheria na siasa kwenye jamii timamu.
Umetoa mfano ambao nadhani maudhui yake hayafanani na jambo tunalojadili hapa, kwa hiyo sitaufanyia consideration.

Umesoma hiyo barua ya polisi? Kimsingi haikidhi vigezo vya kuitwa wito wa polisi achilia mbali 'kosa' wanalo muitia.

'Matamshi aliyotoa kwenye kampeni', hili moja kwa moja linaangukia kwenye maadili ya uchaguzi na ninaamini Lissu hajalizungumzia simply kwa kuwa 'wito' haujakidhi vigezo kisheria huwezi kuzungumzia content yake kwa kuwa inakuwa null and void automatically.

Unafahamu kama Lissu ni Mgombea urais na kuwa yuko kwenye kampeni na ina muda fixed? Kwa 'wito' huo ambao hauanishi jinai yoyote, huoni ni kujaribu kuvuruga kampeni zake na kuingilia haki yake ya kimsingi ya kugombea ambayo inakuja mara moja tu baada ya miaka mitano?
 
Lissu kuwa mgombea urais hakumfanyi kuwa yuko juu ya sheria! Matamshi ya kwenye kampeini yanayovunja sheria hayawezi kuachwa bila kushughulikiwa na vyombo vya sheria kwani ni kuamini kuwa kwa vile yeye ni mgombea basi anaweza akavunja sheria bila kushughulikiwa na hivyo yuko juu ya sheria!

Nobody is above the law!!!!!!. Unless Lissu na wewe mna imani tofauti
 
Hakuna sehemu nimesema Lissu kuwa mgombea kunamfanya awe juu ya sheria.

Nimeeleza kuwa barua haiainishi jinai yoyote bali inasema kwa 'matamshi aliyotoa kwenye kampeni' kosa ambalo nadhani kama lipo basi lingeripotiwa kwenye tume ya maadili ya uchaguzi na si polisi.

Kosa lolote linalo husiana na ukiukaji wa kampeni na taratibu za uchaguzi yanashughulikiwa na tume ya maadili ya uchaguzi kama ambavyo yule Mahera alieleza kuwa Lissu ameshtakiwa kwenye tume ya maadili ya uchaguzi kwa matamshi aliyotoa kwenye mikutano yake.

Wote tumeshasikia kwenye TV kwamba IGP kaamuru Tundu Lissu aende kuripoti kituo cha polisi Moshi. IGP ambaye ndiye top alisisitiza kwamba hiyo ni amri toka kwa IGP. Hiyo ni taarifa ya habari.

Masaa mawili baada ya taarifa ya habari ikasambaa mitandaoni barua ya kumwita Tundu Lissu akahojiwe kwa matamshi yake kwenye shughuli zake za kampeni.

Saa moja baadaye Tundu Lissu amejibu kwenye Twitter yake kwamba wito wa polisi siyo barua ya kirafiki, wito ni amri ya kisheria inayopaswa kueleza kosa unaloitiwa. Kwamba barua yenyewe ameandikiwa mwenyekiti wa CHADEMA na siyo yeye Tundu Lissu na haijaeleza kosa.

Hivyo yeye kama Tundu Lissu ataendelea kesho (leo) na ratiba yake ya mkutano na mabalozi.

Kimsingi ngoma ilitakiwa iishie hapa kwani makosa ya kampeni, kama kweli yapo au kauli kwa mgombea yeyote hayashughulikiwi na polisi.

Nimesema kimsingi ngoma ilitakiwa iishie hapa. Lakini kuna tetesi kwamba hata polisi wenyewe wanajua wamechemka. Wote wanajua sheria inayotawala ni ya uchaguzi na siyo makosa ya jinai.

Pamoja na kujua hayo yote bado mkakati wa kumkamata Tundu Lissu uko palepale na atakamatwa.

Wakishamkamata hawatamfanyia jambo lolote baya ila watakuwa wameshapata kipimo kwamba ukmuonea Tundu Lissu mwaka huu kitatokea nini hapa nchini na jumuiya ya kimataifa itafanya nini.

Maana kiukweli wote hatujajua ukimgusa Tundu Lissu kinatokea nini.

Tusubiri hadi saa 10 jioni tuone yanayokuja
Atakamatwa na kila kitu kitakua kawaida tu!
 
Yaani kumshika lissu kipindi hiki ambacho uchaguzi unaendelea ni sawa na kuwasha moto ndani ya nyumba yako mwenyewe. Polisi na NEC wanajitafutia matatizo ambayo sio ya lazima. Kibaya zaidi NEC na IGP hawajui hata sheria zao wenyewe na wanaita watu kama vile polisi ni sehemu ya ulevi au NEC ni sehemu ya kwenda kuongea ongea na watu.

Lissu ni mtu mmoja lakini inawezekana 50% ya Watanzania wako nyuma yake ni makosa makubwa kumchukulia lissu kama mtu wa kawaida tu.

lakini Lissu akiwauliza hao Polisi ambao hawajapata hata mtu aliyempiga risasi hakuna kesi, mshitakiwa sasa ni mjinga gani ambaye ataamini ukiwaacha misukule kwamba Polisi hata kazi yao imewashinda
 
Kwa hiyo kauli za Lissu ni mbaya ila za kalio anasema mkichagua wa vyama vingine haleti maji ni nzuri?
Nchi kwa double standard inashangaza sana, hawa polisi hivi wote ni form four failure? au wote brainwashed tu? Sometimes tukiitwa monkeys tunajifanya na hasira ila tabia hizi ni za nyani
 
Hakuna sehemu nimesema Lissu kuwa mgombea kunamfanya awe juu ya sheria.

Nimeeleza kuwa barua haiainishi jinai yoyote bali inasema kwa 'matamshi aliyotoa kwenye kampeni' kosa ambalo nadhani kama lipo basi lingeripotiwa kwenye tume ya maadili ya uchaguzi na si polisi.

Kosa lolote linalo husiana na ukiukaji wa kampeni na taratibu za uchaguzi yanashughulikiwa na tume ya maadili ya uchaguzi kama ambavyo yule Mahera alieleza kuwa Lissu ameshtakiwa kwenye tume ya maadili ya uchaguzi kwa matamshi aliyotoa kwenye mikutano yake.
Jibu lako linarudi kwenye maana hiyo ya kuwa kwa vile Lissu ni mgombea, basi yeye yuko juu ya sheria. Lolote atakalofanya la kuvunja sheria za nchi hailiwezi kuchunguzwa na vyombo vha sheria vilivyopo bali tume ya uchaguzi tu: myopic view of the law hata kama unadhani wengie hatujui sheria. Polisi hawajasema Lissu ana jinai yoyote ndiyo maana wanataka kumhoji kuona kama kweli kuna suspicion ya jinai au la; wanaoamua kuwa Lissu kavunja sheria za jinai ni mahakama siyo polisi.
 
lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Hiyo sheria ni kwa balozi wa nyumba 10
 
Kuigomea polisi kufanya uchunguzi ni kinyume cha sheria; sasa sijui yeye ni mwanasheria gani. Wakati mwingine polisi wanaweza kutaka kukuhoji wewe kama shahidi kuhusu mtumhumiwa mwingine tofauti kabisa ambaye wanaweza kuwa na taarifa zake zaidi. Ni afadhali angejibu tu kuwa sasa hivi ratiba yake iko tight sana anaomba akutane na polisi katika muda mwingine siyo sasa kuliko kuweka jou hilo la kukaidi, kwani tayari ameshaweka ushahidi unaoweza kutumika dhidi yake; ndiyo maana nina mashaka sana na busara za Lissu pamoja na uanasheria wake. Hiyo kisheria ni kuizuia polizi kufanya kazi zake ammbalo ni kosa. Raia kuhojiwa na polisi ni sehemu ya majukukumu ya polisi kabla hawajamchukulia mtu hatua; yeye Lissu anaogopa nini kuhojiwa kama anajua yuko clean?
Sasa barua wamemwandikia Mwenyekiti wa Chama ama Lissu?barua hyo inamakosa mengi Ya kiufundi...

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom