Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Hapo anakosea sana, Lissu unafanya makosa ya kijinga, unavunja sheria kwa makusudi ili ufanye ubishi, unafundisha watu kutoheshimu sheria.

Wewe umeshaamua kuwa lazima uwashe moto nchini na uvunje amani. Haitakubalika, lazima utii amri na sheria, unapoonewa tutakupigania, lakini ukionea tutaka sheria ichukue mkondo wake.
Kavunja Sheria gani hapo Sasa,au polisi wanaiuhujumu ccm ili izidi kuchukiwa na wananchi Kama ni hivyo sawa
 
Ameandikiwa Mwenyekiti wake wa Chama. Sasa kama amfika hatua ya kukataa maagizo ya mwenyekiti wake wa Chama...Mh. Mbowe kama barua inavyomuelekeza mwenyekiti kufanya. Dharau kwa vyombo vyetu halali kisheria na kikatiba kama Polisi, ukweli zitamponza kisiasa. Acha aendelee 'kuota mapembe'!
Soma vizuri barua imeandikwa kwa mwenyekiti wa Chana siyo chama.

Pili kwa akili yako ndogo kama samaki unataka kutushawishi na sisi tuwe mambulula kama wewe kuwa polisi tena policcm wako juu ya sheria?
 
Tundu Lissu katika Ukurasa wake wa Twitter, ameweka Barua ya Polisi na kuandika Maneno haya "Wito wa polisi sio barua ya kirafiki, ni amri ya kisheria. Wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa. Barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama. Huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria. Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho."

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro
View attachment 1587622
View attachment 1587514
Jamani jamani Lissu ni moto hakuna Wa kuuzima tujifunze kutoka kwake mmmh kweli Mungu ametuletea Mtu
 
Hapo anakosea sana, Lissu unafanya makosa ya kijinga, unavunja sheria kwa makusudi ili ufanye ubishi, unafundisha watu kutoheshimu sheria.

Wewe umeshaamua kuwa lazima uwashe moto nchini na uvunje amani. Haitakubalika, lazima utii amri na sheria, unapoonewa tutakupigania, lakini ukionea tutaka sheria ichukue mkondo wake.
Toa uzezeta wako hapa
 
Nauliza jamani.
Hiyo barua imeandikwa na kupelekwa kwa.
Mwenyekiti wa.

"Chana cha Democrasia na maendelea"

Ndio nani huyo mwenyekiti wa
Chana?

Yaani Chana kama Chana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Aliyekuwa anachapa atakuwa alikuwa anafokewa, kachapia balaah 😀
Hiyo chana ya ndizi??

Everyday is Saturday...............................😎
 
2013 member mmoja "Synthesizer" alichangia haya.....



Sipatani sana na wanasiasa kwa sababu moja kuu; wengi wao wamekithiri kwa uongo na ahadi za udanganyifu, kuanzia wenyeviti wa mitaa, wabunge, mawaziri au hata maraisi. Nionyeshe mwanasiasa asiye mdanganyifu nitakuonyesha mtu asiyestahili kuwa mwanasiasa.

Chukulia Kenyatta kwa mfano, raisi wa sasa wa Kenya.

Wakati wa kampeni za uraisi alitoa ahadi kwamba kuwa na kesi ICC si hoja, kwani akifanikiwa kuwa raisi atashirikiana na ICC kikamilifu ili kumaliza suala la tuhuma za ICC dhidi yake - tuhuma nzito kabisa zinazohusu mauaji ya watu wasio na hatia.

Baada ya kuwa raisi Kenyatta ameanza kuimba nyimbo tofauti kabisa; kwanza alianza kampeni ili nchi za Afrika kwa ujumla zijitoe ICC. Hakufanikwa katika hili. Na sasa maraisi wa Afrika katika mkutano wao huko Ethiopia wameamua kuliandikia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakiomba/wakidai kwamba mtu anapokuwa madarakani kama raisi asishitakiwe katika ICC!

Natumaini busara ya wale wanaokaa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la sasa ni ya kiwango cha juu kuliko wale walioliandikia ombi/dai la kutaka maraisi waliopo madarakani wasishitakiwe ICC.

Ukitafakari ombi la maraisi wa Afrika, utaona kwamba wanachomaanisha hawa viongozi wa bara langu la Afrika ni kwamba, kukiwa na kiongozi dikteta na muuaji, aruhusiwe kuendelea kuua tu asishitakiwe hadi atakapoacha madaraka ya uraisi.

Pia, hadi sasa nashindwa ni mtu gani mwenye busara kamili anaweza kujitetea kwamba eti ni Waafrika pekee wanaoshitakiwa ICC, sio wazungu. Mtoto wa shule ya msingi? Hivi ni kwa jinsi gani maraisi wa nchi wanaweza kujitetea kwamba mbona wazungu wanaua kama sisi Waafrika lakini hawapelekwi ICC? Khaaa!!! Kwa hiyo, kwa busara zenu enyi waheshimiwa maraisi, mnaona kwamba ili kusawazisha hili kinachohitajika ni kuwaruhusu maraisi wa Kiafrika waue bila kushitakiwa kama wanavyofanyiwa maraisi wa kizungu?

Mtu hadi unachaguliwa kuwa raisi wa nchi yako bado unakosa busara juu ya basic principle kwamba "two wrongs will never make a right?" Just unbelievable.

Kama kweli maraisi wangu wa Afrika wangekuwa na nia na busara ya kutaka kujadili kutoshitakiwa na ICC maraisi waliopo madarakani, wangejadili na maswali yafuatayo;

  • ICC ifanyeje basi, pale raisi dikteta na muuaji yuko katika nchi ambayo katiba yake haina ukomo wa kugombea uraisi (kama Zimbabwe, Uganda nk)? Je, ICC isubiri hadi huyo raisi atakapokufa ndio imfungulie mashitaka?
  • Je, kwa kutaka maraisi waliopo madarakani wasifunguliwe mashitaka ICC, maraisi wa Afrika watakuwa tayari pia kuhakikisha katiba za nchi zote Afrika zina ukomo wa vipindi vya uraisi, viwili visivyozidi miaka mitano kila kimoja?
  • Je, ikiwa maraisi wa Afrika wanataka raisi aliyepo madarakani asifunguliwe mashitaka ICC, watakubali kwamba mtu yeyote mwenye tuhuma za mauaji asiruhusiwe kugombea uraisi katika nchi yeyote, eidha kabla hajawa raisi au kutogombea muhula mwingine ikiwa yeye ni raisi tayari? (kwa mantiki hii Kenyatta asingegombea uraisi Kenya kwa kuwa alikuwa na tuhuma tayari, au asiruhusiwe kugombea uraisi awamu ya pili)
Haya ndio mambo ya msingi ambayo kama kweli maraisi wetu wangepaswa kuyajadili. La sivyo wanaongea vitu ambavyo vinapoteza muda si wetu tu bali hata wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na binafsi nawasikitikia hao waliowachagua kuwa maraisi. Wanatutia aibu sisi Waafrika wengine kudai mambo yanayolinda usalama wa wana Afrika yaondolewe kwa sababu za ki Abunuwasi kama wanazozitoa.

Changamoto kubwa sana inayoyakabili mataifa masikini duniani na kufanya washindwe kuendelea ni nyingi ya akili ndogo kupewa mamlaka makubwa, kwa njia ya kura au kuteuliwa.
Thanks Quote Reply
Report
Bila ICC,pia hofu ya kunyimwa misaada wallah nakuapia Hawa wakoloni weusi wangechinja watu usiku na mchana.Watawala wa kiafrica umuwakilisha Lucifer 100% sababu wengi ni washirikina furaha yao Ni kuwatoa kafara waafrika.Hakuna mtawala wa kiafrica ambae ana mikono Safi ambae ajauwa watu wote.Kuna link Kati ya watawala wa kiafrica na kumwagwa damu.Sioni mtawala yeyeto wa kiafrica ajauwa watu.Waafrika waliouliwa na watawala wa kiafrica Ni wengi Sana kuliko hata idadi ya waafrika waliouliwa na wakoloni weupe.Thus wanataka Kinga ya kutokustakiwa ili wamalize watu, furaha yao Ni kuona machozi ya watu.
 
Inabidi watu waelewe maana ya "HAKI" ni nini, na Tundu Lissu anatoa somo zuri sana.

Watu wamezoea kunyimwa haki kinyume cha sheria kwa sabau ya "UJINGA". Kutojua haki zao.

Kwa hiyo imekuwa ni kawaida kusikia polisi akikohoa tu, watu wanajiharishia hata kama ni wao haki zao ndizo zinazovunjwa.
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Hapana wito wowote polisi lazima uendane na sababu ya kwa nini wanakuitia. Wale ni Law enforcers lazima wakueleze Sheria uliyovunja ili ukatoe maelezo
 
Tundu Lissu katika Ukurasa wake wa Twitter, ameweka Barua ya Polisi na kuandika Maneno haya "Wito wa polisi sio barua ya kirafiki, ni amri ya kisheria. Wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa. Barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama. Huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria. Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho."

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro
View attachment 1587622
View attachment 1587514

Khaaa, ila Tundu kichwa tukubali, once you want to argue/interact with him, jipange, otherwise atakuaibisha hadharani.. 😅, He knows exactly what he is doing, but amekuja kipindi kibaya, JPM will win ingawa kwa my early prediction si kwa kura nyingi like i was thinking, meaning will win with narrow margin, but anything is possible under the Sun, never rule out this guy..!! 😅 CCM tumejipanga kisawa sawa..!!
 
Lisu tii Amri kwanza utahoji badae, acha kulumbana na mamlaka..
 
Back
Top Bottom