Tundu Lissu: Ya Kujitoa Tanzania Mahakama ya Afrika

Tundu Lissu: Ya Kujitoa Tanzania Mahakama ya Afrika

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
FB_IMG_1575442225968.jpg


Hii habari ya Tanzania ya Magufuli kujitoa kwenye Mkataba wa Uanzilishi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Wananchi ni jambo kubwa sana. Ni ushahidi mwingine wa wazi wa utawala wa kiimla unaokanyaga haki za binadamu na za wananchi wetu.

Kwa Mkataba huo tuliouridhia siku za mwisho za utawala wa Rais Mkapa, wale wote ambao haki zao zilikuwa zinakiukwa na Serikali lakini wanashindwa kupata nafuu katika Mahakama zetu za ndani, walikuwa na haki ya kwenda kudai haki zao kwenye Mahakama ya Afrika. Sasa, mlango huo wa haki umefungwa na Rais Magufuli.

Zaidi ya kuthibitisha uimla wa Serikali yetu, uamuzi huo utatusababishia hasara kubwa ya kifedha na kiuchumi. Nitafafanua hili kwa undani.

Sisi Tanzania tumekuwa wenyeji wa Mahakama hiyo ya Afrika tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya kumi iliyopita. Kwa Mkataba kati ya Serikali yetu na AU, tuliipa Mahakama hiyo Ofisi za muda pale Makao Makuu ya TANAPA mjini Arusha kwa gharama yetu.

Aidha, tumeipatia Mahakama hiyo eneo la kujengea Makao Makuu yake karibu na Kisongo, Arusha; tumeijengea Makao Makuu hayo, na nyumba za kuishi Rais, Majaji na Msajili wa Mahakama hiyo. Chini ya Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na AU, gharama hizi zote zinabebwa na Tanzania.

Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na za Wananchi ulikubaliwa mwaka '81 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. Kumnukuu marehemu Profesa Ali Mazrui, Mwalimu alikuwa 'Africa's Titan on the global stage.'

Warithi wake, yaani Marais Mwinyi, Mkapa na Kikwete, waliendeleza kazi kubwa ya kidiplomasia iliyoachwa na Mwalimu. Waliifanya Tanzania, na Arusha, kuwa mwenyeji wa taasisi za kimataifa kama ICTR, EAC na Mahakama ya Afrika.

Na kwa sababu kuwa mojawapo ya 'miji mikuu ya kidiplomasia' ya barani Afrika, hata taasisi za kimataifa na kikanda zisizokuwa za kiserikali, kama vile Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki (EALS) na Chama cha Mawakili wa Afrika (PALU), nazo zimeweka Makao Makuu yao Arusha.

Diplomasia imara ina manufaa makubwa ya kiuchumi na kibiashara. Arusha na Tanzania imenufaika sana kiuchumi na kibiashara kwa kuwa na Mahakama ya Afrika na taasisi nyingine nilizozitaja.

Taasisi za kimataifa kama hizi na wafanyakazi wake zinaleta fedha za kigeni na kuchangia uchumi na biashara katika nchi yetu. Zinatumia bidhaa na huduma za kila aina ambazo zinalipiwa.

Kwa kuipa kisogo Mahakama hiyo ya Afrika, sio tu Rais Magufuli anaiambia Afrika na dunia kwamba Serikali yake haijali haki za binadamu za raia wake; bali pia anaukana urithi wa kidiplomasia wa Baba wa Taifa, na kukataa manufaa ya kiuchumi na kijamii yanayotokana na urithi. Sasa itabidi AU iamue kama bado kuna haja ya Arusha na Tanzania kuendelea kuwa mwenyeji wa Mahakama hiyo.

Profesa Palamagamba Kabudi, mhusika mkuu wa uamuzi huu, anapaswa kuwajibishwa kwa kutumbuliwa kabla hajaharibu heshima ya nchi yetu zaidi ya hili alilofanya.
 
Kwa bahati mbaya sana nchi inaongozwa na mtu ambaye hana uwezo hata kidogo wa kufanya evaluation of consequences, yeye huwa anatwanga tu ingawa ktk kutwanga kwake kuna mengine anafanikiwa ndo maana wengine wanasema ana uthubutu.

In fact siyo uthubutu ni kutokujali. Hata Aga Khan amesimamisha ujenzi wa chuo kikuu kikubwa Arusha kwa sababu yale makubaliano aliyokuwa ameyafanya Kikwete jamaa alivyoingia akayatupilia mbali consequently Arusha imekosa kunufaika kiuchumi na ujenzi wa chuo hicho. Yeye aliangalia manufaa ya kodi ya sasa hivi bila kuangalia miaka 20 - 30 ijayo Tanzania itakuwa inanufaikaje.
 
Awamu ya tano inasema kwamba miruzi mingii........, yaani haya ma-demokrasia, ma-haki za binadamu yenu nk ukiyaendekeza saana yanawacheleweshea wananchi wako maendeleo.
 
Asante Lissu kwa ufafanuzi huu tunakumisi sana uwakilishi wako Bungeni.
Kweli, hapa ndipo kuna tofauti - yaani mnakuwa na level moja ya elimu lakin mwenzako anakuzidi mbali mno kiuwezo. Jana Azam TV Habari kuna mwanasheria mmoja alifafanua jambo hili lakini aiseee....kweli Lissu wewe uko extra miles away..... ni hazina kwa taifa letu.
 
Wasaidizi wake wanaogopa kumshauri, atawatumbua, amejaa ubabe sana wakujiona anajua kila kitu, hataki kusikiliza wengine, ndio maana hata watangulizi wake anaona hawakufanya chochote. Na ni ipi sababu ya msingi waliyoitoa kuhusu tz kujitoa huko?, au ndio mmeona watu wanakimbilia huko kudai haki zao mkaona muwafungie milango ya huko pia, coz hao hamuwezi kuwaweka mfukoni kama mlivyofanya kwa mahakama zetu za ndani!.

Hizo pesa za kigeni tutakazopoteza hapo zingelisaidia taifa kwa mengi, yeye akadhani zitaishia mifukoni mwa wakazi wa Arusha, wish kuona hiyo mahakama ingekuwa imejengwa kanda ile, sijui angefanyaje!
 
Huyu jamaa kabakiza tambo za mtandaoni tuu..

Kisutu inamsubiri muhabarisheni makamanda
 
Huyu jamaa ana hasira sana na Waziri P. Kabudi hivi ni kwa nini? Binafsi sijawahi hata siku moja kumsikia P.Kabudi hata tu akitaja jina la Tundu Lisu lkn yeye Tundu Lisu kutwa nzima, yuko sooo obsessed na P. Kabudi, why??
Hiyo Wizara walikuwepo wengine pia mbona haukuwa obsessed nao?
Isitoshe kwa nini hamshambulii Waziri wa Sheria Mahiga ambaye Wizara yake ndiyo mhusika mkuu na aliyeongea kuhusu hilo swala ni Mahiga na siyo Kabudi, lkn Kabudi hakutoki kwenye mdomo wako, why?

Kama wewe ni mjanja mbona ulishindwa hata tu kusoma instructions vizuri mlizopeana Mbowe na ukapatwa na risasi?
 
Awamu ya tano inasema kwamba miruzi mingii........, yaani haya ma-demokrasia, ma-haki za binadamu yenu nk ukiyaendekeza saana yanawacheleweshea wananchi wako maendeleo.

Maendeleo unayaona katika mtazamo finyu wa barabara na reli! hayo si maendeleo peke yake kuna maendeleo ya kijamii kwa mfano katika miaka ya hivi karibuni tumewaelimisha baadhi ya makabila wakaacha kutahili wanawake hayo ni maendeleo ya kijamii. Sasa kama tunajenga barabara tuu huku watu wanaendelea kukatana visim....... hayo yatakuwa ni maendeleo ya upande mmoja wa vitu bila maendeleo ya watu. Ni mfano mdogo nimekupa.
 
emalau,

Ha ha ndio maana Agha Khan wanaanza ujenzi wa chuo chao hapa katikati ya mawasiliano tower na jengo jipya la psssf (sam nujoma/makabuni road) itakuwa kaingia hofu na hana hela anajenga viwanja tuu asinyang’anywe
 
Tindu Lissu yeye anaishi kwa Mabeberu ila hakauki kiusema vibaya nchi yetu
Kutoa maoni kimutadha nibkuisema bibaya nchi?,kama kuna maamuzi yasiyo sahihi yasiyo na yija kwa jamii yasisemwe?pia katiba imetoa fulsa ya kumoa raia wa nchi kutoa maoni yake ,hutaki aiseme serikali kama inakosea?
 
Lissu akiongea uwa anaeleweka kirahisi sana kuzidi wale wa degree 4

Magufuli udicteta wake mwisho wake utakuwa wa aibu kubwa sana
Ni kwasababu unamsoma Kwa macho ya bashasha, ungewasoma wengine hivyo hivyo, ungewaelewa.
 
Back
Top Bottom