Tundu Lissu: Ya Kujitoa Tanzania Mahakama ya Afrika

View attachment 1281260

Hii habari ya Tanzania ya Magufuli kujitoa kwenye Mkataba wa Uanzilishi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Wananchi ni jambo kubwa sana. Ni ushahidi mwingine wa wazi wa utawala wa kiimla unaokanyaga haki za binadamu na za wananchi wetu.

Kwa Mkataba huo tuliouridhia siku za mwisho za utawala wa Rais Mkapa, wale wote ambao haki zao zilikuwa zinakiukwa na Serikali lakini wanashindwa kupata nafuu katika Mahakama zetu za ndani, walikuwa na haki ya kwenda kudai haki zao kwenye Mahakama ya Afrika. Sasa, mlango huo wa haki umefungwa na Rais Magufuli.

Zaidi ya kuthibitisha uimla wa Serikali yetu, uamuzi huo utatusababishia hasara kubwa ya kifedha na kiuchumi. Nitafafanua hili kwa undani.

Sisi Tanzania tumekuwa wenyeji wa Mahakama hiyo ya Afrika tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya kumi iliyopita. Kwa Mkataba kati ya Serikali yetu na AU, tuliipa Mahakama hiyo Ofisi za muda pale Makao Makuu ya TANAPA mjini Arusha kwa gharama yetu.

Aidha, tumeipatia Mahakama hiyo eneo la kujengea Makao Makuu yake karibu na Kisongo, Arusha; tumeijengea Makao Makuu hayo, na nyumba za kuishi Rais, Majaji na Msajili wa Mahakama hiyo. Chini ya Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na AU, gharama hizi zote zinabebwa na Tanzania.

Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na za Wananchi ulikubaliwa mwaka '81 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. Kumnukuu marehemu Profesa Ali Mazrui, Mwalimu alikuwa 'Africa's Titan on the global stage.'

Warithi wake, yaani Marais Mwinyi, Mkapa na Kikwete, waliendeleza kazi kubwa ya kidiplomasia iliyoachwa na Mwalimu. Waliifanya Tanzania, na Arusha, kuwa mwenyeji wa taasisi za kimataifa kama ICTR, EAC na Mahakama ya Afrika.

Na kwa sababu kuwa mojawapo ya 'miji mikuu ya kidiplomasia' ya barani Afrika, hata taasisi za kimataifa na kikanda zisizokuwa za kiserikali, kama vile Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki (EALS) na Chama cha Mawakili wa Afrika (PALU), nazo zimeweka Makao Makuu yao Arusha.

Diplomasia imara ina manufaa makubwa ya kiuchumi na kibiashara. Arusha na Tanzania imenufaika sana kiuchumi na kibiashara kwa kuwa na Mahakama ya Afrika na taasisi nyingine nilizozitaja.

Taasisi za kimataifa kama hizi na wafanyakazi wake zinaleta fedha za kigeni na kuchangia uchumi na biashara katika nchi yetu. Zinatumia bidhaa na huduma za kila aina ambazo zinalipiwa.

Kwa kuipa kisogo Mahakama hiyo ya Afrika, sio tu Rais Magufuli anaiambia Afrika na dunia kwamba Serikali yake haijali haki za binadamu za raia wake; bali pia anaukana urithi wa kidiplomasia wa Baba wa Taifa, na kukataa manufaa ya kiuchumi na kijamii yanayotokana na urithi. Sasa itabidi AU iamue kama bado kuna haja ya Arusha na Tanzania kuendelea kuwa mwenyeji wa Mahakama hiyo.

Profesa Palamagamba Kabudi, mhusika mkuu wa uamuzi huu, anapaswa kuwajibishwa kwa kutumbuliwa kabla hajaharibu heshima ya nchi yetu zaidi ya hili alilofanya.
Wewe Tundu Lissu huonji sumu kwa ulimi? Kashughulikie demokrasia ndani ya Chadema kwanza ndo utoke nje
 
Huyu jamaa ana hasira sana na Waziri P. Kabudi hivi ni kwa nini? Binafsi sijawahi hata siku moja kumsikia P.Kabudi hata tu akitaja jina la Tundu Lisu lkn yeye Tundu Lisu kutwa nzima, yuko sooo obsessed na P. Kabudi, why??
Hiyo Wizara walikuwepo wengine pia mbona haukuwa obsessed nao?
Isitoshe kwa nini hamshambulii Waziri wa Sheria Mahiga ambaye Wizara yake ndiyo mhusika mkuu na aliyeongea kuhusu hilo swala ni Mahiga na siyo Kabudi, lkn Kabudi hakutoki kwenye mdomo wako, why?

Kama wewe ni mjanja mbona ulishindwa hata tu kusoma instructions vizuri mlizopeana Mbowe na ukapatwa na risasi?
Kwani Mahiga ndiye aliandika barua kujitoa kwenye hiyo mahakama ya Afrika?!

Aliyeandika barua zote ni waziri wa mambo ya nje huyo huyo Kabudi, sasa alaumuwe Mahiga kwa lipi?!

Watu wanajiuliza iweje Mahiga aseme Tanzanua haijajitoa, wakati kuna barua tayari iliyoandikwa na Kabudi ya kujitoa?

Analaumiwa muhusika kwa uhusika wake.

Au wewe pia hujaiona hiyo barua ya kujitoa mahakama ya Afrika iliyosainiwa na Kabudi?
 
Nijuavyo mimi mhusika ni Waziri wa Sheria, hivyo angetajwa hapa!
 
Yaani Tundulisu Leo hii umeshasahau kua ulishawahi sema Nyerere alikua Dikteta?leo hii kwakua unataka kuizungumzia Kujitoa kwaTanzania katika mahakama hii na kuiweka Serikali hii ya JPM katika kundi hilo la udikteta umesha Sahau msimamo wako wa mwanzo juu ya Baba wataifa.
Najua serikali imejitoa kwa sasa katika mahakama iyo kwasababu za kiufundi ila sinashaka siku za baadae itarudi kushilikiana ba mahakama iyo.
Nyerere hakuwa malaika na kwa maana hiyo ndio maana hatunaye tena leo hii, kama binadamu mwingine yeyote ana negatives na positives zake vile vile.

Sababu za kiufundi ni zipi hizo ambazo leo zipo na labda kesho zisiwepo. Sio kweli hizo ni propaganda tu hii nchi kwa sasa haitaki utawala wa haki. Period.
 
Nijuavyo mimi mhusika ni Waziri wa Sheria, hivyo angetajwa hapa!
Ujuavyo wewe, na hata mimi. Lakini aliyeandika barua kujitoa ambayo iko humu JF ni waziri wa mambo ya nje, ambaye ni Kabudi. Huyo Mahiga hakuhusiswa na ndiyo maana alikanusha ile taarifa, nadhani naye hakuwa anafahamu kwamba Kabudi keshaandika barua na Tanzania imeshajitoa.
Badala yake yeye ajasema waliomba mapendekezo fulani ambayo hakuyataja kama requirement, wakati siyo kweli.

Ujuavyo wewe na mimi, lakini ukweli hauko hivyo. Ushahidi wa barua ya kujitoa iliandikwa na Kabudi.
Na iko humu JF kwa reference yako. Hivyo ni sahihi Kabudi kutajwa siyo Mahiga.
 
Kwa hiyo greda likija kuvunja nyumba yako utaenda kumshitaki dereva wa greda au Halmashauri iliyomlipa kutekeleza? Hivi mtu anayejitapa kuwa ni Msomi kama Tundu Lisu atashindwa kuona uhusika wa Waziri wa Sheria hapo hadi asimshirikishe kabisa kwenye lawama zake?
 
Tindu Lissu yeye anaishi kwa Mabeberu ila hakauki kiusema vibaya nchi yetu
Kwani ukiishi kwa mabeberu ndo unafungwa mdogo.wabongo wangapi wako ughaibuni na wanaongea.mange kimambi Yuko tz mbona aliwachota watu wengi Tena wenye akili zao.Acha hizo mabeberu wakati ndomawategemea hata mnawaza kuishi huko ila mmeshomdwa
 
Lissu is our next president, huyu jamaa sio tu kwamba ni baba la sheria lakini kwenye taaluma ya kiuchumi pia yuko sawa, Wtz msisite hili jabali likigombea urais mkalimiminia kura zenu kwa mzo, hii ni hazina.
Amesoma commercial pia a level hge
 
Kwa hiyo greda likija kuvunja nyumba yako utaenda kumshitaki dereva wa greda au Halmashauri iliyomlipa kutekeleza?
Kwanza una deal na dereva asitekeleze huo unyama, hizo halmashauri unaweza kuzionea kuna maagizo kutoka juu.

Hili la kujitoa Mahiga unamoonea, Muhusika ni Kabudi na ushahidi upo, mshikwa na ngozi ndiye mwizi.

Labda ungeomba Kabudi aadhibiwe kuingilia mamlaka ya wizara isiyo muhusu.

Mwanasheria mkuu na Mahiga wote hawakuhusika kwenye hili.

Inawezekana ni maagizo kutoka juu.
 
Ukikuta nyumba ipo chini utaenda kwa dereva? Isitoshe unaujua vizuri utaratibu wa kujitoa ulivyo? Yaani nani anahusika na nini katika Serikali? Nani anayeamua, jukumu la nani katika mchakato mzima wa nchi kujitoa?
 
Huyu jamaa ana hasira sana na Waziri P. Kabudi hivi ni kwa nini? Binafsi sijawahi hata siku moja kumsikia P.Kabudi hata tu akitaja jina la Tundu Lisu lkn yeye Tundu Lisu kutwa nzima, yuko sooo obsessed na P. Kabudi, why??
Hiyo Wizara walikuwepo wengine pia mbona haukuwa obsessed nao?
Isitoshe kwa nini hamshambulii Waziri wa Sheria Mahiga ambaye Wizara yake ndiyo mhusika mkuu na aliyeongea kuhusu hilo swala ni Mahiga na siyo Kabudi, lkn Kabudi hakutoki kwenye mdomo wako, why?

Kama wewe ni mjanja mbona ulishindwa hata tu kusoma instructions vizuri mlizopeana Mbowe na ukapatwa na risasi?
Kwa sababu kapudi hana akili anadharirisha taaluma ya sheria
 
Ukikuta nyumba ipo chini utaenda kwa dereva? Isitoshe unaujua vizuri utaratibu wa kujitoa ulivyo? Yaani nani anahusika na nini katika Serikali? Nani anayeamua, jukumu la nani katika mchakato mzima wa nchi kujitoa?
Ukiikuta chini huendi kokote nchi hii, ndiyo maana ya kujitoa mahakama ya Afrika, kwamba hata ukionewa na hizi mahakama zetu usiende kokote, yani ukikomolewa usubiri kufa tu.

Swala la kujiunga kama nchi linahusisha bunge, na kujitoa ilipaswa iwe hivyo, maana ni swala la kitaifa na wabunge ndio wawakilishi wetu.

Waziri wa sheria na katiba na mwanasheria mkuu ndio wahusika wakuu wenye dhamana ya hili.

Lakini nchi yetu haiko hivyo, utaratibu ni tatizo letu la msingi.

Sasa keshaamua Kabudi kwamba tunajitoa mahakama ya Afrika na Waziri wa sheria ba katiba ndugu Mahiga na hata mwanashera mkuu wa serikali hawana taarifa, na ni sawa tu maana ndivyo tunavyokwenda.

Tuliwai ambiwa kuna mihimili merefu na kuna mirefu zaidi, kwa hili unatafuta nini tena, mchawi?!

Limeshaamuliwa na iko hivyo, tuzoee tu.

Usimpende Lisu, lakini kubali kawama ziende kwa Kabudi.

Ndiye muhusika mkuu kwenye hili.
 
Lissu is our next president, huyu jamaa sio tu kwamba ni baba la sheria lakini kwenye taaluma ya kiuchumi pia yuko sawa, Wtz msisite hili jabali likigombea urais mkalimiminia kura zenu kwa mzo, hii ni hazina.
kura hatutazimimina labda risasi
 
View attachment 1281260

Hii habari ya Tanzania ya Magufuli kujitoa kwenye Mkataba wa Uanzilishi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Wananchi ni jambo kubwa sana. Ni ushahidi mwingine wa wazi wa utawala wa kiimla unaokanyaga haki za binadamu na za wananchi wetu.

Kwa Mkataba huo tuliouridhia siku za mwisho za utawala wa Rais Mkapa, wale wote ambao haki zao zilikuwa zinakiukwa na Serikali lakini wanashindwa kupata nafuu katika Mahakama zetu za ndani, walikuwa na haki ya kwenda kudai haki zao kwenye Mahakama ya Afrika. Sasa, mlango huo wa haki umefungwa na Rais Magufuli.

Zaidi ya kuthibitisha uimla wa Serikali yetu, uamuzi huo utatusababishia hasara kubwa ya kifedha na kiuchumi. Nitafafanua hili kwa undani.

Sisi Tanzania tumekuwa wenyeji wa Mahakama hiyo ya Afrika tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya kumi iliyopita. Kwa Mkataba kati ya Serikali yetu na AU, tuliipa Mahakama hiyo Ofisi za muda pale Makao Makuu ya TANAPA mjini Arusha kwa gharama yetu.

Aidha, tumeipatia Mahakama hiyo eneo la kujengea Makao Makuu yake karibu na Kisongo, Arusha; tumeijengea Makao Makuu hayo, na nyumba za kuishi Rais, Majaji na Msajili wa Mahakama hiyo. Chini ya Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na AU, gharama hizi zote zinabebwa na Tanzania.

Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na za Wananchi ulikubaliwa mwaka '81 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. Kumnukuu marehemu Profesa Ali Mazrui, Mwalimu alikuwa 'Africa's Titan on the global stage.'

Warithi wake, yaani Marais Mwinyi, Mkapa na Kikwete, waliendeleza kazi kubwa ya kidiplomasia iliyoachwa na Mwalimu. Waliifanya Tanzania, na Arusha, kuwa mwenyeji wa taasisi za kimataifa kama ICTR, EAC na Mahakama ya Afrika.

Na kwa sababu kuwa mojawapo ya 'miji mikuu ya kidiplomasia' ya barani Afrika, hata taasisi za kimataifa na kikanda zisizokuwa za kiserikali, kama vile Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki (EALS) na Chama cha Mawakili wa Afrika (PALU), nazo zimeweka Makao Makuu yao Arusha.

Diplomasia imara ina manufaa makubwa ya kiuchumi na kibiashara. Arusha na Tanzania imenufaika sana kiuchumi na kibiashara kwa kuwa na Mahakama ya Afrika na taasisi nyingine nilizozitaja.

Taasisi za kimataifa kama hizi na wafanyakazi wake zinaleta fedha za kigeni na kuchangia uchumi na biashara katika nchi yetu. Zinatumia bidhaa na huduma za kila aina ambazo zinalipiwa.

Kwa kuipa kisogo Mahakama hiyo ya Afrika, sio tu Rais Magufuli anaiambia Afrika na dunia kwamba Serikali yake haijali haki za binadamu za raia wake; bali pia anaukana urithi wa kidiplomasia wa Baba wa Taifa, na kukataa manufaa ya kiuchumi na kijamii yanayotokana na urithi. Sasa itabidi AU iamue kama bado kuna haja ya Arusha na Tanzania kuendelea kuwa mwenyeji wa Mahakama hiyo.

Profesa Palamagamba Kabudi, mhusika mkuu wa uamuzi huu, anapaswa kuwajibishwa kwa kutumbuliwa kabla hajaharibu heshima ya nchi yetu zaidi ya hili alilofanya.
Hivi mtu akiamua juu ya mali yake wewe inakuuma nini? Maana umeshakili kuwa tanzania ni ya Magufuli "Tanzania ya Magufuli"
 
Ukiikuta chini huendi kokote nchi hii, ndiyo maana ya kujitoa mahakama ya Afrika, kwamba hata ukionewa na hizi mahakama zetu usiende kokote, yani ukikomolewa usubiri kufa tu.

Swala la kujiunga kama nchi linahusisha bunge, na kujitoa ilipaswa iwe hivyo, maana ni swala la kitaifa na wabunge ndio wawakilishi wetu.

Waziri wa sheria na katiba na mwanasheria mkuu ndio wahusika wakuu wenye dhamana ya hili.

Lakini nchi yetu haiko hivyo, utaratibu ni tatizo letu la msingi.

Sasa keshaamua Kabudi kwamba tunajitoa mahakama ya Afrika na Waziri wa sheria ba katiba ndugu Mahiga na hata mwanashera mkuu wa serikali hawana taarifa, na ni sawa tu maana ndivyo tunavyokwenda.

Tuliwai ambiwa kuna mihimili merefu na kuna mirefu zaidi, kwa hili unatafuta nini tena, mchawi?!

Limeshaamuliwa na iko hivyo, tuzoee tu.

Usimpende Lisu, lakini kubali kawama ziende kwa Kabudi.

Ndiye muhusika mkuu kwenye hili.

Utaratibu wa kujitoa ukoje? Ndiyo simpendi Tundu Lisu!
 
Back
Top Bottom