Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

😅😅😅😅 amerudi DAR....
Tunduma ni Moja ya sehemu rahisi sana kupata mtaji Kwa mgeni, ukifika sehemu kama muajiriwa Mungu akakufungulia njia ukaoata mtajiL lazima uangalie wapi ulianzia Maisha urudi ukaendeleze ulivyoacha mwanzoni, Dar ukienda ukiwa tayari umejipanga utapapenda. Broe nenda Kariakoo wale Wakinga wote wamepata Mitaji Tunduma then ndio wakahamia Dar es salaam. Maeneo ya miji kama Tunduma ukipata Hela inabidi uhame miji kama hiyo watu wote wanajuwana nani kapata Hela nani yupo Juu, Hivi vitu vinaleta Wivu na Wivu unaelekea kuanza kuwendwa Kwa Wahanga , kukwepa hayo unajiondoa taratibu
 
Bro hata zikiwa vzr meli zote lzm zifike dsm Ndio karibu kulko msumbiji

Angalia hta ramani ya china to dsm na china to mozambiq
Hujui hata unachoongea.

Kutoka Beira-Lubumbasi ni jirani kuliko Dar-Kubumbashi.

Kutoka Beira-Lusaka ni jirani kuliko Dar-Kusaka

Kwa hiyo only advantage ipo Sasa hivi ni usalama mdogo njia ya Msumbiji, miundombinu Duni ya Barabara na uwekezaji mdogo hapo Beira Port.

Mwisho tunakoelekea hizo Changamoto zikitatuliwa umuhimu wa Tunduma utapungua.

Na Kwa taarifa tuu ni kwamba kabla Zimbabwe haijaharibiwa na Mugabe,Wazambia walikuwa wanafuata mizigo Yao Harare baada ya uchuykiharibika pande Ile ndio wakageukia Tanzania na ndio chanzo Cha Tunduma kukua haraka miaka ya kuanzia 2010 Hadi Sasa.
 
Ongeeni yooote, mwisho wa siku kwa Tanzania hii hakuna sehemu yenye mzunguko mkubwa wa pesa kama Kariakoo hata ukiweka mahaba yako ila uhalisia utabaki kuwa kama ilivyyo. Ukishangaa uuzwaji wa bidhaa kwa bei nafuu Tunduma, nenda Katoro na Geita kwa ujumla na ni miji ambayo haiko mpakani ila kuna bidhaa zina either bei nafuu kama Kkoo au sawa na Kkoo lakini mwisho wa siku bado wafanyabiashara wanapahitaji Kariakoo.
Sahihi TRA 2022 walikusanya kodi kariakoo bilioni 300 je Tunduma walikusanya ngapi?
 
Mzunguko wa pesa Tunduma ni wa kiwango Cha juu🤣🤣🤣
Kama haupo hapa kwenye orodha hii basi hamna hela huko
 
Zile deal za Black market upande wapili nyuma ya frame za Viatu ule upande unazalisha sana Madoni Kila mwezi kwenye deal za:-
Vipodozi.
Vitenge.
Mafuta ya Kula.
Sukari.
Sigara .
Mbegu za Mahindi / Zamsed.
Mafazeti used kutoka Zimbabwe, South Africa.
USD ;- zinatoka Congo na unazipata upande wapili, Pombe za Viroba, na Pombe za vichupa vidogo wanauza Bei ya Tshs 1000/= na Viroba vinaanzia 250-500 maeneo ya Black na Iboya.
Kuna matajiri wanspiga Hela kwenye Biashara ya kubadilisha Fedha, yeye ana Supply fedha Kwa Vijana jioni anarudishiwa na Faida , Hao wanaitwa wenye Visima , mtu ana Supply hata billioni Moja Kwa Vijana wake 30 wanaokwenda kutafuta Dolla Hadi Congo.
Kuna Wababe kwenye Biashara ya Mafuta ya Petroleum kupeleka upande wa Zambia Kuna Yule Msomali wa Petroafrica mwenye upara aliwakamata sana wa Zambia.
Kuna Yule Tajiri wa Valentine Bar ya Pale Boarder na Valentine night club Jamaa anajimbiza sana kaanzia kwenye Bar Hadi kushika soko la Viatu Hadi Kumiliki Kusoma pale Kisimani.
Yupo Dubai Tyre Jamaa anakimbiza sana kwenye biashara ya Tyre Sasa amehamia kwenye Mafuta Bei zake za Tyre ni kama Dar es salaam. Yupo yule Manyanya ameshika biashara za maduka balaa pale Boarder piya yeye ndie amehamia kwenye vituo vya Mafuta, Wapo Hawa Jamaa wa Olympic petroleum anauza Mafuta Kwa wholesale Kwa Bei ya Depot'.
Mjii wa Tunduma una Bank zaidi ya Sita, Petrol Station zaidi ya Hamsini, lodge na Bar zimetapaka Kila baada ya nyumba mbili or tatu,
we ndio umeielezea tunduma kwa mapana.ni mji ambao unamalori mengi kuliko miji yote tz ukitoa dar.kiti moto ni kama kuku tu huku.lodge hujaa kalibu siku zote.ni mji mmoja upo bize sana.kumkuta mtu ameshika million 30 mkononi na yupo kwenye msongamani wa watu nijambo la kawaida kabisa.ni boda machachali kuliko zote tz.naikubali sana tunduma

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Huu uzi ilikuwa niuandike muda mrefu kwa mambo niliyojionea kwenye mji wa Tunduma. Kwa ambao hajawahi fika Tunduma wanaweza kudhani ni ka-mji kadogo ambacho kipokipo tu. Kwa sisi wa Arusha tulikuwa tunaamini Namanga ndo mji mkubwa zaidi wa mpakani kwa Tanzania kumbe kuna Tunduma.

Kinachonifanya niandike ni biashara kubwa iliyoko Tunduma. Ule mji wa mpakani kwa mjasiriamali mdogo ni sehemu sahihi ya kwenda kusoma ramani. Uchangamfu wake unaendana sana na Kkoo tofauti ikiwa ni ukubwa tu. Ila wafanyabiashara wa nguo Tunduma wanawezaje kuuza nguo za jumla kwa bei sawa na ya Kariakoo? Baadhi ya wafanyabiashara huuza bei chini hata kuliko Kariakoo. Kimahesabu imekaaje hii? Hata vitu vingine jamaa wako fair.

Kimsingi Tunduma ni boda kubwa zaido bongo yenye fursa nyingi sana.
Wafanyabiashara wa Tunduma wengine wanaagiza mzigo Toka china na Dubai, ni wachache wanakuja kuchukulia dar. Mji ule unahudumia wakongo na wazambia Kwa kiasi kikubwa sana
 
Kkoo habari ingine mazee
Africa inasemekana Ethiopia ndo Wana soko linakaribiana na kkoo
Tunduma mbona hotel za maana hazifiki hata 10?..
Anyway Tunduma ni mji wa magendo toka Enzi za Nyerere
watu tunaongelea bei kuwa chini na tunaongelea bolder sio miji mikuu.kwa hyo na wewe kwa uzoefu wako unataka kulinganisha mji wa tunduma na dar.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom