Tuombe Mungu sana watoto wetu wasijekuwa kama mwijaku maana huku alipofikia inasikitisha

Hayo ni yale unayoyajua kua anayafanya na anapata hayo unayosema anamiliki.Huoni labda kuna mengine huyajui na yanafanywa naye,ilimradi apate sifa kua ana mafanikio?
Kuna ambao wanafanya mapenzi pia kinyume na maumbile ili muwasifie kua wana mafanikio,sijasema Mwijaku ni mmoja wao.
 
Nimekuelewa sana.

Ukipitia comment utaona hali halisi ilivyo kwa sasa.

Kaamua yeye awe hivi aweke chakula meza, familia wale.

Ndio maana wengine na sie twaona sawa, maana nayo I nahitaji juhudi si kila mtu anaweza fanya hivyo.. Mfano wewe.
 
Unamzidi nini mwijaku,
anamaisha mazuri kuliko wewe, mwijaku usimwone anafanya ujingwa , huo ujinga kalipwa hela nzuri tu
 
Hizi ni tabia za watu wa pwani, ndiyo huwa ''wanafanya kazi'' kwa kutumia mdomo. Ndiyo maana maeneo hayo hayana maendeleo. Hata Tanzania sasa hivi uongozi umejikita kwenye huu utamaduni wa ''kutenda'' kwa kutumia midomo. Bila shaka hii haiwezi kuwa ndiyo future ya Tanzania sembuse generation. Ni mapitio ya muda tu kwani huwezi kudanganya watu wote kwa muda wote. Nchi haiwezi kuendeshwa kwa maneno na ukweli utadhihirika baada ya muda.
 
Kweli vyote anavyo ila pata picha vijana wote au kijana wako anakuwa na mtizamo wa uchawa kama Mwijaku.

Kuna jamii nyingine zimekuwa na maendeleo sababu ya watu walio bora ,sababu marole model walio wazunguka wanafanya vitu vya maana kwa kutumia akili na talent zao na si kujipendekeza mf China. Sometimes China unaweza ukaona wanakosea ila kwa kufilter content za Tiktok na kuondoa vitu vya kipuuzi na kuviacha vya maana,ila ukitizama impact ya social networks ktk kujenga kizazi kilicho bora na chenye mitizamo chanya kwa maendeleo ya jamii China wapo sawa.

Machawa siku hizi wapo mpaka sehemu za kazi,wanawadidimiza wengine kisa yy ni chawa wa boss.Mfano kama huyo Mwijaku kwa tabia yake Kisha chafua Image ya Tanasha akatishia kumpeleka kwa Pilato akaomba Msamaha, juzi kachafua Image ya KP kampeleka mahakamani wameombana msamaha yameisha, hivi huoni huyu jamaa ni mtu wa hovyo,pamoja na hivyo anavyo vimiliki maana yupo tayari kuwaharibia wengine ili yeye atrend.
 
Kizazi cha ovyo

Ova
 
Wenye akili tunafahamu hapo wanaolengwa ili waharibike na kuwa na Taifa la mafala ni Sisi, watoto na wajukuu zetu kwa kutumia Mwijaku, na chawa wengine kama chambo! Inaitwa LARGE SCALE SOCIAL DECEPTION, mnaswagwa kushabikia ujinga huku mambo muhimu yenye manufaa wanaachiwa wachache

 


Kwa kweli inasikitisha mno.
Angesoma chuo kingine kingesemwa kuwa kinatoa products za Sawa na zero brain.
Lakini kumbe hata Udsm kumbe inatoa mafafa miaka hii ??! 🤔🤔🤔
Yaani hata ambae hajaenda Shule kabisa hata darasa la kwanza ako na afadhali.
Ni huzuni kwa kweli
 
WAtoto wengi watakuwa kama yeye tena zaidi yake. Maana kwa sasa elimu na weledi tumeitupa uchawa ndiyo unalipa. Watu wasiokuwa na elimu wanapewa kipaumbele watu kama Steve Nyerere wanaweza kuonana na namba moja wakati waziri wake anahangaika.
Sasa vijana wachague nini? Kuwa wasomi na wenye weledi bila pesa au kuwa machawa pro max wapate pesa? Jibu baki nalo wewe mwenyewe.
 
Kuna watu wazima humu ambao nao tayari akili zao zimeshaharibika.

Sidhani kama kuna mzazi angependa mwanae awe chawa wa mwenzake.

Sijui tunajenga jamii ya aina gani.
 
Siyo watakuwa...washakuwa

Ova
 
Jifananishe wewe mwenyewe Kwanza na Mwijaku kwenye mafanikio.
Laiti angefanya Mzungu mngesifu
 
Jifananishe wewe mwenyewe Kwanza na Mwijaku kwenye mafanikio.
Laiti angefanya Mzungu mngesifu


Mafanikio kwa kujitoa utu wako ?
Kwani maana ya mafanikio ni nini labda ?!
Kuwa na material things pekee ?
Tafuta kujua zaidi aisee.
Heshima na utu ndio mafanikio ya kwanza kwa binadamu mengine yanafuata.
 
Huenda ni miongoni ambao katika Safari yao ya masomo ni Watu wa kudesa mwanzo mwisho.
Ni huzuni kwa kweli .
Ndio maaana wasomi wengi ni waoga kupita kiasi.
Hawajui kujenga hoja, kuuliza maswali, kujibu hoja wala kujielezea.
Wengi ni watu wa kubumba tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…