Nitaandika kwa kifupi tu, kuna case nimeshindwa kuipa suluhu nimeitwa kuleta amani kwenye nyumba ya hao wana ndoa.
Wewe ni mwanamke muislamu olewa na mwislamu mwenzako, na kama wewe mwanaume ni Mkristo owa Mkristo mwenzako.
Issue ni ngumu, Mkristo kaka mwanamke muislamu kipindi mahaba ndindindi, Sasa ndoa imejibu Watoto Wawili, mwanamke wote anadai ni Watoto wake na wote wanapenda madrasa za kiislamu.
Sasa sitaki mada hii iwe ni mihadhara au jukwaa la kukashifu dini nyingine, nimeweka hii mada ili kuitwa ushauri wa bure.
Ikiwa mwanamke na mwanaume mmekubaliana kuweka dini zenu pembeni na mfunge ndoa bomani basi jitahidini na swala Watoto mkubaliane wakizaliwa wafuate imani gani au mgawane vipi urithi wa imani kwa Watoto na kwa hali ya Sasa muandikishiane kisheria ili lisilete tabu baadaye.
Nawapenda sana Mama zangu na Dada zangu lakini ukweli uko wazi wao ndio tatizo, wanaume huwa hawana ligi za kijinga.
Nimewashauri acheni Watoto wakiwa adult wachaguwe imani wanayotaka ila mke wa ndoa anasema Watoto ni wake, ila kimoja kipengele cha school fees mke ndio anatambuwa kama Watoto wana baba.
Nimehairisha hii case namuomba Mungu anipe busara sijui muhafaka utapatikana vipi? Inasikitisha sana Watoto wadogo kuwaharibu kisaikolojia kurithi dini za wakoloni.
Kwakweli mnaotegemea kuowa au kuolewa na watu wa dini tofauti msilipuuze hili muandikishiane kwa Wakili kama mlivyofunga mkataba wa ndoa serikalini.
Wacha nipate kwanza lager zinipe hekima kulimaliza.