Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
- Thread starter
-
- #21
Upo sahihi, first born ana jina la kibantu, huyu ni mvulana mkubwa Sasa ana haki ya kupiga kura, wa Pili ana jina neutral linatumiwa na dini zote za Abraham.Majina inabidi wapewe yale neutral
Adam /Nuhu/Musa
Sophia/Rehema/Zawadi
Hilo ni rahisi baba yake kutumia madhehebu nje ya dhehebu lake la Katoliki kama Mimi.Au wakifa wazikwe vipi
Ufupi wa barnaba na akili zake sawaBarnaba amebadili dini na kuwa muislam.
Mara nyingi watoto hufauata dini ya mama ,maana muda mwingi mama ndiyo mlezi wa watoto hivyo atawajenga zaidi kwenye dini yake.
[emoji109][emoji109][emoji109]Katika dini mwanamke hufuata upande wa mwanaume akikaidi ni uzembe wa mwanaume husika,
Hii kesi simple tu, kwani watoto ni wa baba? Au mama? Huyo anayetambulika kuwa ndie mwenye watoto ndo wafate dini yake.Nitaandika kwa kifupi tu, kuna case nimeshindwa kuipa suluhu nimeitwa kuleta amani kwenye nyumba ya hao wana ndoa.
Wewe ni mwanamke muislamu olewa na mwislamu mwenzako, na kama wewe mwanaume ni Mkristo owa Mkristo mwenzako.
Issue ni ngumu, Mkristo kaka mwanamke muislamu kipindi mahaba ndindindi, Sasa ndoa imejibu Watoto Wawili, mwanamke wote anadai ni Watoto wake na wote wanapenda madrasa za kiislamu.
Sasa sitaki mada hii iwe ni mihadhara au jukwaa la kukashifu dini nyingine, nimeweka hii mada ili kuitwa ushauri wa bure.
Ikiwa mwanamke na mwanaume mmekubaliana kuweka dini zenu pembeni na mfunge ndoa bomani basi jitahidini na swala Watoto mkubaliane wakizaliwa wafuate imani gani au mgawane vipi urithi wa imani kwa Watoto na kwa hali ya Sasa muandikishiane kisheria ili lisilete tabu baadaye.
Nawapenda sana Mama zangu na Dada zangu lakini ukweli uko wazi wao ndio tatizo, wanaume huwa hawana ligi za kijinga.
Nimewashauri acheni Watoto wakiwa adult wachaguwe imani wanayotaka ila mke wa ndoa anasema Watoto ni wake, ila kimoja kipengele cha school fees mke ndio anatambuwa kama Watoto wana baba.
Nimehairisha hii case namuomba Mungu anipe busara sijui muhafaka utapatikana vipi? Inasikitisha sana Watoto wadogo kuwaharibu kisaikolojia kurithi dini za wakoloni.
Kwakweli mnaotegemea kuowa au kuolewa na watu wa dini tofauti msilipuuze hili muandikishiane kwa Wakili kama mlivyofunga mkataba wa ndoa serikalini.
Wacha nipate kwanza lager zinipe hekima kulimaliza.
Hujavaa muhusika, mfano hai kwangu mwenyewe WiFi yako aliwahi kutafuta shule ya mmoja ya Watoto wetu, ada ndefu sana na hakunishirikisha, lakini akawa na busara akanieleza wazi ada ya shule niliyotaka Mimi nilipe kule amount hiyo hiyo yeye ataongezea 2 M kwa kila mwaka.Katika dini mwanamke hufuata upande wa mwanaume akikaidi ni uzembe wa mwanaume husika,
Yani ktk dini hainaga kujadili me ni kichwa, mfano wako uko tofauti na madaHujavaa muhusika, mfano hai kwangu mwenyewe WiFi yako aliwahi kutafuta shule ya mmoja ya Watoto wetu, ada ndefu sana na hakunishirikisha, lakini akawa na busara akanieleza wazi ada ya shule niliyotaka Mimi nilipe kule amount hiyo hiyo yeye ataongezea 2 M kwa kila mwaka.
Iwe una hoja nzuri.Yani ktk dini hainaga kujadili me ni kichwa, mfano wako uko tofauti na mada
Mkuu issue ni nzito kuliko unavyoichukulia wewe.Hii kesi simple tu,kwani watoto ni wa baba ? au mama?,huyo anayetambulika kuwa ndie mwenye watoto ndo wafate dini yake.
Hakuna akili, wala hayupo sahihi, mambo ya imani hayana neutral, kwamba nusu muislam na nusu mkristo, hilo halipo, wakifa watazikwaje? Dini ya baba tu, finish.Upo sahihi, first born ana jina la kibantu, huyu ni mvulana mkubwa Sasa ana haki ya kupiga kura, wa Pili ana jina neutral linatumiwa na dini zote za Abraham.
Wewe una akili sana, nitaangalia post zako kwa makini ili kupata muhafaka wa hii kadhaa.
hiyo ndiyo point.imeisha hiyo.[emoji109][emoji109][emoji109]
Watoto wote Wawili wanatumia ubini wa baba yao na Kabila ni baba yao.Kesi nyepesi sana mtoto anaitwa jina la baba au mama
Kama jina la ukoo wa baab ndio anatumia hao watoto basi ni dhahiri hao ni watesu sio wa mtume
Pole sana mkuu, kwa kuumiza kichwa, kuna mzee mmoja alikuwa na watoto wa kike wengi na waliolewa, mmoja aliolewa na waarabu waislam, yule mzee ni wakristo pure, sasa siku mtoto wake aliyeolewa na waarabu akija kumsalimia huku amevaa majuba, yule mzee alikuwa haongei kitu ila tu anatokwa na machozi, hasemi chochote, mpaka yule mtoto wake anapoondoka, sitasahau nikikumbuka najiskia vibaya sana..Mkuu issue ni nzito kuliko unavyoichukulia wewe.
Ngoja niwe wazi ili unielewe kuna vitu sitaki kuviandika humu ili mada isije kugeuka kuwa ya kashfa za kidini.
Ila kwa ukweli wa nafsi yangu kama mwanaume ni Mkristo kuwa makini sana kuowa bomani mwanamke mwislamu ambaye kwao kuna dini dini sana.
Waislamu wao wao hawatambui ndoa kati ya Mwanamke wa kiislamu na mwanaume asiye mwislamu, kwahiyo Watoto wanatambuwa ni wa mama bila kujali mmefunga ndoa bomani.
Sasa ndugu zangu waislamu wasikatae kula nyama ya nguruwe Halafu mchuzi wanakunywa, kama uislamu inatambuwa mtoto ni wa mama basi baba asiulizwe lolote kuhusu matunzo na ada za mtoto, wao wawe ni sex partners tu kwenye hiyo ndoa yao ya bomani.
Sio hivyo, kwa jamii zetu za ki tz ni ngumu kukwepa kwa jinsi tulivyojichanganya, mapenzi ni upofu, hayaoni kesho...Wakati mwengine ushamba wa wanawake au kuwa mtu asiyewaza mbali,hili jambo ni hatari sana inatakiwa mtu akitaka kuanzisha familia ajue anachokifanya wengi huwa hawazingatii hilo.