Tuongee Kifamilia leo, kama unataka kuoa au kuolewa na mna imani za dini tofauti jitafakari upya

Kamuulize mwanamke na hawa watoto ni kabila gani? Akikujibu kamuulize mwanamke hawa watoto ni kabila gani? Na kwa nini? Akikujibu maliza kesi.
 
Katika dini mwanamke hufuata upande wa mwanaume akikaidi ni uzembe wa mwanaume husika,
Hakuna hiyo kitu, kwa waislamu kwanza hapo hakuna ndoa haitambuliki kidini na watoto wanakuwa wa mwanamke.

Pili mwanamke ndiyo anakaa na watoto kipindi kirefu kwa hivyo by default watoto watakuwa wanafuata dini ya mwanamke (awe muislamu au mkristo).
 
sio hivyo,kwa jamii zetu za ki tz ni ngumu kukwepa kwa jinsi tulivyojichanganya,mapenzi ni upofu,hayaoni kesho...
Nilipo-bold

Hapo ndiyo penye tatizo,mkuu mimi naishi mji wenye imani tofauti tofauti kabla sijaowa nilikuwa na mahusiano na wanawake wa imani tofauti na walinifurahisha ila lilipokuja suala la kuanzisha familia kwanza niliizingatia sana imani yangu hata mke nilitafuta wa Imani yangu kwa sababu najua na naamini ndiyo ipo sahihi kutuongoza ktk maisha.

Haya mambo ya kusema mapenzi upofu yanaumiza na yanayumbisha sana familia iwe ni kwenye imani au kwenye mambo ya kawaida ya kimaisha hii kauli ni ya kuikemea siyo ya kuiendekeza.
 
Mheshimiwa ,
Hapo kunaonekana Kuna udhaifu upande wa mume kwa sababu ubini mzima (kabila & dini ) lazima zitokea kwa baba ....Kuna sababu kadhaa zinaweza kuchangia akachua kwa mama mfano mtoto alitelekezwa au hawakufunga ndoa (mwanamke hajaolewa alizalishwa tu)

Kwa hapo mwanaume ana madhaifu kwa vile alitamkiwa kumconfess huyo mke afuate kila kitu na imani yake tangu mwanzo .Hiyo ndo maana halisi ya kichwa cha familia
 
Asante mnoo kwa mleta mada.
Bahati mbaya sana kuna wachangiaji wengi hapa wa hii mada wameshindwa kumuelewa mleta mada. Hoja kuu hapo ya mleta ni namna gani ilipaswa huo mkwamo utatuliwe kwa kuepukwa kabla ya ndoa kufungwa. Nami nitachambua hapa.

1. Hata kama hao wanandoa wangeweka mambo yao kisheria wakati wa kuoana (kusema watoto wafuate dini fulani) bado huenda isingekuwa suluhisho kamili kwa kuwa, dini ni suala la moyoni unaotokana na utashi, na kwa mtoto hujifunza imani kama tabia za kuiga kutoka kwa mzazi/wazazi. Kama wazazi ni wafuasi wa dini tofauti, kwa mtoto kinakuwa kitendawili kigumu. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

2. Ni hatari kuwaza kuwa, watoto walelewe kibagani (bila kufuata dini yoyote) ili wakiwa wakubwa wachague dini watakayoitaka! Samaki mkunje angali mbichi.

Suluhisho la hayo matatizo ni nini? Ndoa za dini tofauti hazifai kwa malezi ya mtoto kiimani, ziepukwe.
 
Mkuu, naomba nikuongeze uwe jiko dogo maana sio kwa nondo hizo...๐Ÿ˜‚
 
Kwa watu wasio wasomi, wenye Elimu ya chini, wasio na exposure, au upeo mkubwa wa uelewa, mambo ya ndoa na tofauti za dini, huwapa shida sana.

Mke wa Khasim Majaliwa, PM wa sasa ni mkristo na hakuna shida, mkuu wa mkoa wa zamani wa Kagera, Abdulaman Babu, alikuwa Mkristo, jamaa alikua anamleta kanisani kila Jumapili, wewe unaoa mtu sio dini, kwanza Kuna unafki mwingi sana, unakuta wote ni dini moja, lakini mnamaliza hata mwaka bila kwenda kanisani au masjid, sasa dini ya nini.

Kila mtu aabudu kivyake, ubovu wa Waafrika, dini inapewa nafasi kubwa kwenye mausiano na familia!!
Uchumi ndio iwe kiapumbele, katika kutafuta pesa, hakuna dini, tafuta pesa saidia wasiojiweza huo ndio Uislam, Ukristo mzuri!! Sio unaaacha msichana mzuri kisa dini yake??!!!!
 
Maji ya chumvi na baridi huwa hayachanganyiki kwenye mkondo bahari mmoja..
 
hakuna hiyo kitu, kwa waislamu kwanza hapo hakuna ndoa haitambuliki kidini na watoto wanakuwa wa mwanamke.

Pili mwanamke ndiyo anakaa na watoto kipindi kirefu kwa hivyo by default watoto watakuwa wanafuata dini ya mwanamke (awe muislamu au mkristo).
Narudia tena mwanamke(wa dini yoyote) kukaidi kufata dini ya mwanaume ni uzembe wa mwanaume, short loud and clear,

Kwa huo mfano wako watoto wanatumia ubini upi?
 
Narudia tena mwanamke(wa dini yoyote) kukaidi kufata dini ya mwanaume ni uzembe wa mwanaume, short loud and clear,

kwahuo mfano wako watoto wanatumia ubini upi?
Hata wakitumia ubini so what? Imani ni kitu tafauti kabisa
 
Hiyo ligi kuisha mpka mmoja afe
Hata wafe wote bado haitasaidia.

Kumbuka kuna mmoja ambaye ndiye kwa asili tunaamini alipaswa awarithishe kile aliamini ni sahihi kwao (baba) na sasa ameshindwa wahusika wameshaenda anakoamini hakuwafai that's why tupo hapa tunajadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ