Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 966
- 6,019
- Thread starter
-
- #221
Ikikupendeza sms tafadhali kwenye 0765345777 kwa wepesi zaidi Ili kujua shida hasa Iko wapi nimpe mkuu wa Chuo husika. ShukraniUshauri wenu kwenu fuatilieni kozi ya social work ipo chini ya wizara yenu, kuna mauza uza mengi sana kwenye hii kozi kwa upande wa cheti na diploma,
Tumshukuru Mungu. Kila la heri kwako.Mheshimiwa ubarikiwe sana kwa huu uthubutu wa kusikiliza kero za wananchi.
Sidhani kama tunahitaji kuonbelewa kwenye sura. Tunahitaji kujumuishwa kwanza kwenye jina lililobeba wizara. Neno wanawake liondoke hapo libaki jinsiaSalaam. Ahsante kwa muda wako na maoni yako. Wizara hii ni ya Jinsia zote. Ndiyo maana sera mpya ya jinsia ya Mwaka 2023 ukurasa wa 22 unaongelea wanaume (male engagement). Ndiyo maana watoto wote chini ya miaka 18 inahusu jinsia zote. Labda useme umekwama wapi na ukakosa huduma gani tafadhali?
Shukran sana mama, Mungu akulipe wema kwa kutusaidia sie wanyonge. Nitafikisha salamu na kumpa namba atume ujumbe kwako. Ubarikiwe mkuu.Salaam. Ni kweli nilikuwa bize wala si uongo. Ndiyo naingia humu Leo baada ya siku kadhaa. Lakini pia, kwa dharura huwa Nina mbadala wa mawasiliano. Unaandika na kutuma ujumbe kwenda 0765345777 na copy 0734124191. Ahsante sana
Nimemfikishia ujumbe amefurahi sana mpaka amelia kwa furaha kwa jinsi ulivyompa matumaini. Kwa kweli huyu mwanaume ni shetani sana, inabidi achukuliwe hatua za haraka sana. Bila shaka binti atawasiliana na wewe kwa namba za sms. Asante sana mkuu.Kwanza pole nyingi kwa Binti huyu. Pia, huyu Binti kama ana mawasiliano mpe namba yangu ya simu anitumie ujumbe nitamuongoza akikwama.
Utaratibu rasmi ni, aende Dawati la jinsia polisi aandikishe maelezo. Pale atapewa mtaalamu wa ustawi wa jamii atasikiliza shauri hili na kuliongoza kwenye utaratibu.
Upo msaada wa kisheria pia, akihitaji atapewa.
Ahsante Sana
Niwie radhi kuchelewa kujibu, mambo huwa wakati mwingine yanakuwa mengi.
Maamuzi hufuata matokeo ya tafiti.Sidhani kama tunahitaji kuonbelewa kwenye sura. Tunahitaji kujumuishwa kwanza kwenye jina lililobeba wizara. Neno wanawake liondoke hapo libaki jinsia
KaribuniShukran sana mama, Mungu akulipe wema kwa kutusaidia sie wanyonge
Nitafikisha salamu na kumpa namba atume ujumbe kwako
Ubarikiwe mkuu
Sawa mheshimiwa. Basi anza mchakato huo. Kwanza naelewa kuwa suala hilo sio la tafiti bali kura. Mchskato wa kuondoa mfumo jike kwenye wizara yakoMaamuzi hufuata matokeo ya tafiti.
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,
Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.
Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.
Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.
Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.
Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).
Karib
Wala hakuna mfumo jike. Kwa sasa kiongozi idara ya jinsia ni mwanaume. Na idara hiyo inao wanaume wa kutosha tu.Sawa mheshimiwa. Basi anza mchakato huo. Kwanza naelewa kuwa suala hilo sio la tafiti bali kura. Mchskato wa kuondoa mfumo jike kwenye wizara yako
Namsubiri. ShukraniNimemfikishia ujumbe amefurahi sana mpaka amelia kwa furaha kwa jinsi ulivyompa matumaini,
Kwa kweli huyu mwanaume ni shetani sana, inabidi achukuliwe hatua za haraka sana
Bila shaka binti atawasiliana na wewe kwa namba za sms
Asante sana mkuu
Iitwe wizara ya jinsia na makundi maalum. Kitendo cha kuiita jinsia wanawake na makundi maalum tayari umeshaweka ubaguzi. Kwamba wanawake nao wanaingia kwenye jinsia na kwa wanawake.Wala hakuna mfumo jike. Kwa sasa kiongozi idara ya jinsia ni mwanaume. Na idara hiyo inao wanaume wa kutosha tu....
maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii ni vitu viwili tofauti nyie mnachanganya huku mkijua kabisaAmina, Shukrani
Ungemsaidia Mh.Waziri hizi asilimia ulizobainisha hapa umezipata wapi ,isije ikawa unazungumzia Takwinu za Familia yenu ,Halafu unafanya rejea kwenye masuala nyeti ya Kitaifa!Mheshimiwa Waziri Salaam
Wizara yako ni Nyeti sana kwa mstakabali wa nchi.
Naomba shugulikia haya yafuatayo
1. Changamoto ya Ndoa kuvunjika
Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na ukosefu maadili kuanzia kwa familia , jamii na hata kwenye Makundi ya utetezi wa haki za wanawake.
Asilimia 95 ya ndoa huvunjwa na wanawake kutokana na makundi ya wanaitwa marafiki na kufuata mkumbo wa makundi mabaya na hatimae mwanamke hukosa utii huanza uzinzi na kuvunja ndoa...Ongeeni na wanawake Wenzenu watambue nafasi ya waume zao.
2.. Wanawake kuzaa kwa upasuaji hili ni janga kubwa zaidi...kila hospitali unayooenda hasa Miji Mikubwa kila mwanamke amezaa kwa upasuaji..Hili suala ni la kibiashara haiwezekani kila mwanammke hasa Dar apasuliwe mwanamke huyo huyo ukimpeleka Songea anazaa kwa kusukuma.
Jamani hili linaharibu sana Wanawake sana...
Jina la Wizara limeinclude usawa wa jinsia?Wala hakuna mfumo jike. Kwa sasa kiongozi idara ya jinsia ni mwanaume. Na idara hiyo inao wanaume wa kutosha tu.