Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Mh kubwa ombi letu sisi tunaomba jina la wizara ibadirishwe na kuwa Wizara ya Ustawi wa Jamii kwasababu unapoongelea makundi maalumu wazee na watoto hawa wote baba yao au mama yao ni ustawi wa jamii na tunaomba maendeleo ya jamii iende kwenye Wizara ya Mipango huko ndiko kunawafaa kwani huko ndiko wanaweza wakajadili kwa kina jinsi gani wataleta maendeleo kwa jamii kwa kupanga mikakati bora lakini sio huku huku tuna deal sana na matatizo ya watu binafsi na ndoa na wazee.

In general, matatizo yanayoikumba jamii na linapo kuja swala la kufanya linkage tutawatafuta hao maendeleo ya jamii kama tuna vyo watafuta wanasheria for the purpese client kupata haki yake tunaingiliwa kazi na maendeleo ya jamii.

Sisi kama maafisa ustawi wa jamii wanatubana kufanya kazi yetu ndio maana ata mikopo kwa walemavu hawapati walengwa badala yake wanapata watu hambao hawahusiki.

Hili nalo kero, lichunguze tena tumesema sana huku lakini hatusikilizwi
 
Hongera sana Madam Doroth Gwajima.

Binafsi nakupongeza kwa uamuzi huu uliochukua kama kiongozi wa wizara hyo.

Kushirikisha wadau wa mitandao ya kijamii katika kutoa MAONI ili kuweza kuboresha huduma.
 
Karibu sana Mh/Dkt Gwajima kupitia wizara uliyopewa maoni yangu na ushauri ni kupitiwa upya mipango mikakati kwa watu wenye makundi maalumu hususani katika nyanja ya Ajira,usawa na huduma za kijamii ,uwepo wa uwezeshaji na semina kama awamu iliyopita
 
Hongera Sana kwa kujiunga na mtandao pendwa wa JF,natumia kupitia kwako wanaJF watajifunza mengi haswa kwenye wizara yako.Karibu Sana mheshimiwa🙏
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member...
Asante mungu kwa nafasi hii,

Mh waziri mke wangu alishakata taraka tangu 2019 na bado tunaishi pamoja hadi leo nikiamini ni mke wangu wa ndoa, na mm nimekutana nayo mwez januari mwaka huu na sijamwambia ila naumwa mawazo na sina Amani juu yake huyu mtu,n ikichukua hatua gani katika hili nisionekane kutenda ukatili?

Nimeihifadhi hii nyaraka kwa faida zangu na hajagundua kama nishaiona na niko nayo,nifanyeje?
 
Asante mungu kwa nafasi hii,,,,mh waziri mke wangu alishakata taraka tangu 2019 na bado tunaishi pamoja hadi leo nikiamini Ni mke wangu wa ndoa,na mm nimekutana nayo mwez januari mwaka huu na sijamwambia ila naumwa mawazo na Sina Amani juu yake huyu mtu,nikichukua hatua gani katika hili nisionekane kutenda ukatili???nimeihifadhi hii nyalaka kwa faida zangu na hajagundua Kama nishaiona na niko nayo,nifanyeje?
Hatua ni kuonana na Afisa Ustawi wa eneo lako tafadhali ngazi ya wilaya au mkoa, tafadhali usifanye ukatili, inawezekana kufikia ufumbuzi wa amani. Iwapo utakwama popote kwenye hatua hizo usisite kuwasilisha kwa msaada zaidi. Shukrani
 
Mh Waziri karibu sana Jamii forum....hakika hili ni jukwaa la kupata taarifa nyingi sana kutoka kwa jamii.

Ombi langu kwa wizara yako.

Mh Waziri huku vijijini watoto wa Shule za msingi na sekondari wanabakwa sana na kuozeshwa mapema mnooo. Ila huwezi kusikia kwa sababu ya tabia zao za kumalizana kienyeji kwa kulipana pesa kama faini.

Nipo hapa Samilunga -Maligisu wilayani Kwimba mkoani Mwanza karibu na mkoa wa Simiyu wilaya ya Maswa kata ya Jija.

WASAIDIENI MABINTI KWA KUWEKA DAWATI LA JINSIA MASHULENI AU KWENYE OFISI ZA KATA.
 
Dokta Dorith Gwajima, angalieni sana kesi za ubakaji zinazotokea kwenye jamii, nyingi haziripotiwi na hata zikiripotiwa wazazi na taasisi huyamaliza kimya kimya bila kujua kuwa mbakwaji ameathirika kisaikolojia hivyo inahitajika juhudi kumjenga na kumrejesha kwenye hali yake ya kawaida. Wengi waliobakwa baada ya kesi zao kumalizwa hakuna anayehangaika nao tena, huachwa hivyo hivyo wajizoelee, hii ni hatari hawa ndo hugeuka kuwa wahalifu wakubwa duniani.

Kingine, try to Broad your harizon kuhusu matukio ya kujiua yanayozidi kuongezeka. Nchi nyingine zimewekeza sana kwenye maswala ya afya ya akili lakini hata leo sijui kama una idadi ya wanasaikolojia ulionao nchini, yani toka ngazi ya kijiji hadi taifa hili ni tatizo kubwa kama taifa inabidi tulichukulie kwa umakini.

Asante.
 
Kuna wanawake wanafanya biashara ya kuuza miili Yao na hili ni suala ambalo linachochea maadili kuporomoka

Serikali kupitia wizara iliyo chini yako naomba ije na mkakati wa kuwasaidia mitaji hawa wanawake na wasichana na sio kuwakamata na kuwadharirisha mbele ya vyombo vya habari.

Karibu Arusha mheshimiwa yaani maeneo ya kaloleni imekuwa ni kero sana na tunaogopa watoto watajifunza huu ujinga na kuona ni kitu cha kawaida.
 
Karibu Daktari. We're exceedingly honored having you here.
 
Hakika, kwa uzito wa Wizara uliyoibeba, na majukumu makubwa ya mustakabali wa nchi, uliyonayo ,Hongera! Umeweka mfano mzuri, hiyo ni ishara ya uongozi, Karibu tena

Ningependa uanzie hapa kwani nafikiri kuna mazuri ya kubeba.

Again, Hongera.

===========

Vilevile ni washauri uongozi wa hapa JF waweke uzi huu kama Utambulisho(ni ushauri tu) halafu wawaanzishieni Jamvi maalum.
 
Mhe. Waziri Daktari D. Gwajima hongera kwa kazi hasa ya kuinua ustawi wa jamii na makundi maalum

1. Baada harakati za kunyanyua maendeleo jinsi ya wanawake zilizoanza miaka karibu miaka 25 iliyopita na kufanikisha wanawake kupata haki zao nyingi na kuondolewa kwa unyanyasi mwingi aliokuwa anapata mwanamke, sasa hivi ni muda muafaka kwa Serikali kuweka nguvu kubalance na kuwaonya wanawake na kuwachukulia hatua kali wanawake wanaotafsiri vibaya haki za wanawake kwa kuanzisha vitendo vya kunyanyasa wanaume hasa kwenye ndoa kwa kusingizio haki za wanawake. Wanawake wengi wanakiuka haki na mikataba ya ndoa kwa kisingizio sheria na haki zinawalinda .

Wanawake waonywe kuhusu haki na sheria za ndoa, wanawake waache kujiamulia uhuru wa kujichagulia aina ya maisha kuishi akiwa ndani ya ndoa na familia zilindwe.

Ni marufuku mke kujiamulia kuishi nje ya nyumba yake kwa kigezo chochote kila bila ruhusa ya mume wake, wanawake wasisitizwe haki ya usawa haimaniishi matengano au mwanamke atalea watoto peke yake kwa sababu uchumi unamruhusu.

Waelimishwe Haki za Binadamu na haki za watu zinahitaji kulea na kujenga familia watachangia kwa usawa kulinda maslahi ya familia,kulinda na kuwaelimisha watoto wao.

2. Ifanyike jitahada mpya ya kuwaelimisha wanawake na wasichana waliolimika kuwa mwanamke kuimarika kiuchumi sio kigezo cha kuleta matendo kwa matendo atakayotaka haki ya talaka, kubatilishwa kwa ndoa na mateso kwa watoto kukosa malezi ya mama na baba.

Yapo mengine ya kujenga nitafanya jitahada ya kukutafuta maana hayo ni kikazi zaidi nikishindwa kukupata nitakutumia sms.

Nakutakia kazi njema.
 
Bila Shaka huu ni ujasiri wa kutosha! Karibu sana , hapa utaoata facts, umbea, majungu, fitna. Kila kitu!
Ngoja nianze Kwa kukudokeza tu, idadi ya Maafisa Ustawi ya Jamii, ni ndogo mnomno, angalieni namba ya kutatya hili, ona wadau wanavyo shauri.
Mh Waziri karibu sana Jamii forum....hakika hili ni jukwaa la kupata taarifa nyingi sana kutoka kwa jamii.

Ombi langu kwa wizara yako...
 
Bila Shaka huu ni ujasiri wa kutosha! Karibu sana , hapa utaoata facts, umbea , majungu, fitna ... Kila kitu ,!
Ngoja nianze Kwa kukudokeza tu...idadi ya Maafisa Ustawi ya Jamii,ni ndogo mnomno,angalieni namba ya kutatya hili, ona wadau wanavyo shauri ...
[emoji28] ahsante Sana, nawasoma wote maoni yenu halafu nitarejea baadae
 
Back
Top Bottom