Mheshimiwa waziri, wizara yako Ina kipengele cha watu maalum. Naomba kujua watu maalum ni wepi haswa?
Pili, nafahamu pia wafanyabihashara wa kati na wamachinga ni mojawapo ya makundi yanayohudumiwa na wizara yako. Je, ni kwanini wananchi hawafahamu hili? Kwanini wasemaji wa wizara hawafanyi jitihada za kutangaza hili ili wananchi na hawa wafanyabihashara wajue hili?
Tatu, je wizara yako ina wanasheria ambao wanaoweza kuwasaidia kisheria wanawake na watoto hata kwa ushauri? Kama wapo, ni kwanini wewe na wasaidizi wako hua mnaelekeza wananchi wawasiliane na maafisa ustawi wa mikoa hata kama jambo linaonekana wazi kabisa linahitaji ushauri wa kisheria?
Nne, kwanini hapo wizarani hamzingatii maswala ya TEHAMA katika mawasiliano? Kwa hali ilivyo mnafikiri ni rahisi kila mwanamke kufika Dodoma kufata msaada hapo wizarani? Mheshimiwa ukiwa kama mwanamke nafahamu unafahamu hali halisia ya mwanamke akiwa na shida, kapigika na anahitaji msaada, mnatakaje wanawake wafike Dodoma na hawana hela ya guest wala nauli?
Tano, kwanini hamna desturi ya kufuatilia hatma ya mwananchi alieleta kero na kuhitaji msaada hapo wizarani kwenu? Mimi shemeji yangu alifikisha suala lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara (Mama wa Kizanzibar, very friendly), Katibu akamwelekeza kwa AfIsa aitwae Nandera.
Mwanzoni akafatilia ile issue (ambayo nina uhakika hiyo wizara inapaswa kufuatilia hilo jambo kwa ukaribu maana hapo ndio mahala pake), lakini mwisho wa siku mama yule aliachwa hewani. Yule Nandera wala huwa hapokei simu yake, na mpaka leo yule mama anateseka na watoto wake.
Wewe mwenyewe ulimwambia aende kwa Afisa ustawi anaitwa Denis, yule mama amenyanyaswa kijinsia, analea watoto mwenyewe, ameonewa, ninyi mnadhani wale watoto alionao anajenga taifa gani pale? Hivi Mheshimiwa ninyi hapo wizarani mnafikiri unyanyasaji wa kijinsia ni ubakakaji tu na ulawiti?
Mnafahamu kuna mambo yanazuilika ambayo hupelekea visa hivi vibaya kutokea? Mfano, huyo mama jinsi mmemuignore, akiamua kuwa malaya au mlevi, watoto wake si watageuka majambazi au mashoga? Ni taifa gani litakuwa linajengwa hapo? Unyanyasaji wa kijinsia upo wa aina nyingi, ni lazma muyafahamu hayo.
Sita, tueleze kuhusiana na juvenile court. Mheshimiwa waziri, unaionaje mahakama ya watoto? Je, ni sahihi watoto kuingizwa mahakama ambazo hizo hizo zinatumika na majambazi na majangili?
Mimi nilishuhudia kwa macho mtoto wa miaka saba, mama yake amewekwa lockup kwa amri ya Mheshimiwa Mwakisu, eti ili ampe baba mtoto simply because baba wa mtoto ana hela, hataki kuhudumia mtoto, baba hana mke ni anakesha bar tu na wanawake na shauri limesikilizwa upande mmoja.
Ustawi wa jamii, hawajachunguza sehemu mtoto anayopelekwa, lakini mtoto ametishwa asipoenda kwa baba, mama atafungwa. Na hakimu mwakisu pamoja na ustawi wanamtukana yule mama na kumfedhehesha mbele ya mtoto wake, mama analia kilio kikubwa sana hapo mahakamani.
Nimekupa mfano huo Ili uone jinsi ambavyo mfumo uliopo wa mahakama za watoto hauko sawa, na ustawi wa jamii haswa hapa Arusha una matatizo mno, unahitaji marekebisho ya haraka. Hakimu anaendesha kesi mathalan ya uhujumu uchumi then inafata ya mtoto. Mtoto yupo hapo nje na mama yake au baba, haya ni mazingira Gani tunawajengea watoto?
Saba, mfumo dune katika nchi yetu uko katika haki gani kwa sasa? Serikali imechukua hatua gani kupambana na kuhakikisha inamaliza mfumo dume? Unafahamu hata hawa viongozi wa chini huku kama Watendaji, Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya na Mikoa ni wafuasi wa mfumo dume? Kwenye Taasis za Umma haswa Polisi ndio usiseme.
Mheshimiwa Waziri imefikia hatua kiongozi mwanamke akitoa maamuzi hayafatwi, simply because she is a woman. Hapa kwetu tuliwahi kupata DC mwanamke ambae alikuwa mweledi sana, na hata sasa ni kiongozi mkubwa sana kwenye sekretariet ya chama tawala.
That woman had vision, lakini alipopanda na kuwa RC, DC aliekuja kuchukua nafasi yake alifuta mambo mengi na maamui mengi ya kiongozi yule. Sasa tuambie, wizara yako na serikali imejipangaje kuhakikisha mfumo dume unapungua ama unaisha kabisa? Kwa kuanzia kwa hawa viongozi waandamizi, je, kuna lolote mmewahi kufanya ili kuwaondolea zana ya mfumo dume katika uongozi wao? Mfumo dume ni mbaya na unadumaza taifa.
Nimeyasema hayo nikiwa na uchungu mkubwa sana.
Jumanne njema Mkuu.