Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Asante Mheshimiwa Dr. Gwajima kuungana nasi.

Kuna Hawa walemavu wanaotaabika na kuishi Kwa Kuomba omba mahali mbalimbali, Je hawatengewi bajeti na Serikali ya kuwahudumia?
 
Asante Mheshimiwa Dr. Gwajima kuungana nasi.

Kuna Hawa walemavu wanaotaabika na kuishi Kwa Kuomba omba mahali mbalimbali, Je hawatengewi bajeti na Serikali ya kuwahudumia?
Tatizo hapo ni Ulemavu au kuombaomba!?
 
Nakupongeza mushimiwa waziri kua karibu na wananch kwa kujiunga platform ya JF.

Pendekezo langu kwa kuzingatia thima ya wizara ya 'ustawi wa jamii' iwe na mikakati endelevu itayowezesha jamii ya watoto, wazee isipyopitia mazingira magum katika nyanja zote nikimaanisha mlengo wa haki na maisha yao.

Mfano kupitia ofisi za ustawi wa jamii kuwepo semina mashulen na hata sehem zitazofaa kuusiana na namna bora tunavyoweza kujenga jamii iliyo bora walau maafisa hawa wafanye ivyo mara 4 kwa mwaka katika maeneo yao.
 
Karibu sana dada mpendwa Muheshimiwa, mie nakujua na ninakukubali kwa kuwa wewe ni muwazi na mpokeaji mzuri wa maoni ya watu unaowahudumia katika maeneo yako ya kazi ulipo kwa wakati huo.

Kwa kuwa memba wa JF (japo wana JF tulibezwa kwa muda mrefu) na kwa jinsi ulivyokuwa unatujibu masuala tuliyokuuliza kwa ufasaha, uso kwa uso (pamoja palikuwa na Covid 19) na kwa weledi wa hali ya juu wakati tukiongelea afya katika ziara yako pale Muhimbili.

Sina mengi zaidi ya kusema, karibu sana, nimefurahi.
 
Karibu sana jukwaani. 'Kila kitu kiko fresh'. Tutaendelea kukupa inputs kadri zinavyojiri...
 
K
Tatizo ni Kuomba omba wakati tuna wizara Kwa ajili ya walemavu na inatengewa Bajeti Kila Mwaka Wa fedha.
Kuombaomba ni tabia ya mtu, si kila mlemavu ni ombaomba...kuondoa ombaomba wenye Ulemavu sio jukumu la Serikali pekee, ni juhudi zako mm na wewe! Kwako wewe Bw. Kichhoff anza na kuondoa fikra potofu kuwa walemavu ni watu wa kupew na Serikali! Serikali jukumu lake ni kiweka mazingira ya kuondoa vikwazo na kutoa fursa na kuwezesha watu wenye Ulemavu!
 
Mh. Daktari Dorothy Gwajima wewe ni mfano wa kuigwa na Mawaziri wote, nakupongeza sana na huwa nakufuatilia sana tangu ukiwa Waziri wa Afya. Nasema karibu sana kwenye michango na mada huru JF.

Ila kwa mfumo mzuri na endelevu weka page ya wizara yako maana huwezi jua kesho na kesho kutwa ukawa Waziri wa Sheria na Katiba

So dada yangu mpendwa acha kitu ambacho wana JF kila wakati tutakukumbuka maana umetukosha sana kwa kujitokeza hadharani. Mungu akubarjki sana sana.

Pia ukikutana na Naibu wako wa zamani Godwin Mollel usisahau kumwambia Sanya juu Naibili, Makiwaru - Kidire mpaka Kia Airpot hatuna barabara ya lami tangu dunia iumbwe.
 
Dada Doro asalaam aleykhum, mimi swali langu ni moja tu tena dogo sana.

Kila mwaka nasikia halmashauri zinatenga pesa za kuwakopesha walemavu na vijana. Kwa kweli sijawahi kuona hii disadvantaged group wakipewa mikopo, au niiweke hivi, hili kundi lifanyeje liweze kupata hiyo mikopo?
Mwisho nakupongeza kwa kutotajwa na CAG.
 
Karibu sana Mhe. Waziri, mimi nitachangia kwenye makundi maalum, na hapa nitajikita kwenye watoto wanaozaliwa na ulemavu wa akili, wengine wanaita mtindio wa ubongo.

Kwa kuwa kwenye jamii zetu watoto hawa hawakosekani kwa sababu mbalimbali wazazi na walezi wa watoto hawa, ukiachilia mbali changamoto za malezi wanazozipitia huko majumbani kwao, pia kumekuwa na changamoto kubwa kwenye shule za watoto hawa.

Madarasa ya watoto hawa, ambayo yapo kwenye shule za kawaida, kiukweli hayako kwenye mazingira mazuri kiusafi, vifaa, walimu wa kutosha na wenye uzoefu nk.

Huwa natafakari sana kwamba ni kwa nini madarasa haya kwenye hizi shule, kwa kuwa huwa siyo mengi (2 - 3 rooms) kwa nini yasipewe kipaumbele kwa kuwa na vifaa vyote muhimu, walimu wenye taaluma na hawa watoto, majengo bora nk?

Tena ukitilia maanani kwamba hata wenye shule binafsi wenye haya madarasa ya watoto wa mahitaji maalum ni wachache sana hapa nchini, ni vema serikali ikalibeba hili jukumu Mhe. Waziri na hata ikibidi kuwa na shule pekee za watoto wenye uhitaji maalumu ambazo zitakuwa na mchanganyiko na chuo au study za kazi.
 
Mheshimiwa mm naomba muandae program maalum itakayoendeshwa kitaifa kusaidia mashirika binafsi kiuwezo. Mengi yanavurunda tu
 
Ahsante Sana, nimepokea. Na kwa mawasiliano zaidi ya ushirikiano kwa maendeleo na ustawi wa jamii unaweza kunifikia kwa ujumbe kwenye 0734124191 au 0765345777 (tuma ujumbe nitakusoma). Ubarikiwe. Tunahitaji umoja wa jamii kwa maendeleo na ustawi wa jamii [emoji120]
Nakupongeza mh. Waziri umefanya jambo la kipekee kabisa ambalo Mawaziri wengi wamelishindwa, hongera sana, naomba waziri wa ardhi naye aige hili, kwani ni njia rahisi zaidi ya kuwasiliana na watanzania wale ambao sio rahisi kukufikia, hasa katika kupata ushauri, maoni, malalamiko na mengi ya aina hii.
Hongera Dr. Gwajima.
 
Asante mungu kwa nafasi hii,

Mh waziri mke wangu alishakata taraka tangu 2019 na bado tunaishi pamoja hadi leo nikiamini ni mke wangu wa ndoa, na mm nimekutana nayo mwez januari mwaka huu na sijamwambia ila naumwa mawazo na sina Amani juu yake huyu mtu,n ikichukua hatua gani katika hili nisionekane kutenda ukatili?

Nimeihifadhi hii nyaraka kwa faida zangu na hajagundua kama nishaiona na niko nayo,nifanyeje?
Hili nalo ni la waziri? Nenda kwa padri au sheikh mkamalize huko
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Kuna shule moja ( ya Serikali ) Kawe nyuma tu ya Kituo cha Polisi ina Mwanafunzi Shoga na anajiuza mno kwa Wanaume Kijiweni Kwake nyuma ya Kituo cha DalaDala cha Ukwamani jirani na Fundi Computer maarufu hapo aitwae Badi.

Kila la Kheri.
 
Mh. Dr. Doroth Gwajima, nakupongeza sana kwa kufungua account yako hapa JF. Bila shaka yoyote utapata maoni na maswali pia ambayo natumaini yatajenga na kukusaidia kuboresha huduma za Ustawi wa Jamii Nchini!
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Mheshimiwa Gwajima D, kule PM kuna ka ujumbe kako.
 
Nimefurahi kuona waziri ukishiriki mijadala na wananchi. Hongera sana Dr.
 
Kuna shule moja ( ya Serikali ) Kawe nyuma tu ya Kituo cha Polisi ina Mwanafunzi Shoga na anajiuza mno kwa Wanaume Kijiweni Kwake nyuma ya Kituo cha DalaDala cha Ukwamani jirani na Fundi Computer maarufu hapo aitwae Badi.

Kila la Kheri.
Duuuh hii hatari sana.
 
Back
Top Bottom