Tupe mkasa wako ulivyoishia kumuoa uliyedhani utapiga na kusepa

Tupe mkasa wako ulivyoishia kumuoa uliyedhani utapiga na kusepa

Miaka ya nyuma kidogo kuna jamaa yangu alienda mbeya huko vijijini ndani ndani kuna mishe gani sijui alikua anapiga huko. Sasa jamaa kutokana na hali ya kule baridi na nini akakamatia guluguja moja matata akawa anasogeza nalo siku kiaina. Mara paap.. likanasa ujauzito! Jamaa kapambana nalo sana litoe likagoma kabisaa na likaamua kuhamia geto anapokaa mshkaji likadai limefukuzwa kwao.

Jamaa kuona ivyo akaona isiwe tabu akali taimu akabeba vitu vyake vichache akaliachia geto yeye akarudi zake chuga maskani. Maisha yakaendelea kama kawaida jamaa akasahau kabisa kuhusu lile guluguja tukawa tunagombania magoli kitaa.

Siku ya siku tumekaa zetu kibarazani tunapiga stori mbili tatu na mwana mara tunaona polygon shape moja ina tumbo kubwaa inakuja uelekeo wetu. Kadri ilivyokua inatusogelea ndio mwana anazidi kuwa mwekundu maana jamaa alikua mweupe. Aisee jamaa hakuamini lile guluguja limekuja likiulizia mpaka likafika home!! Jamaa ndio kukalishwa na wazee pale akabanwa akakubali kweli yeye ni mhusika. Basi ikabidi jamaa awe mpole tuu na guluguja lake sasa atafanyaje? Mtoto amekuja kuzaliwa yaani ni fotokopi huulizi kitu. Mpaka leo tunavyoongea jamaa yuko na guluguja lake maisha yanaenda.
Jamaa kapata superwoman[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kosa lako ninaloliona hapa ni kumfata demu mwingine huku uko na mwingine. Nafikiri ulipaswa kuchagua moja tu. Kuwa na msimamo kuwa upo na huyu mwingine akatafute maisha mengine.
Hayo mengine ni makosa yake. Huwezi kukata tamaa sababu you are 29 na umeachwa. Wala kufika 30 sio sababu ya kufanya mwanamke hakubali mwanaume mradi katamka ndoa.
Pengine alipangiwa mwanaume bora kuliko wewe lakini pupa ikampeleka pabaya.
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kukaa ndani ya misingi ya dini au mila na desturi zetu. Otherwise effect kama hizi ni kubwa sana.
Hapa uliposema kakosea kutafuta demu mwingine huku anamwingine aseee unamuonea ki ukweli
 
Miaka ya nyuma kidogo kuna jamaa yangu alienda mbeya huko vijijini ndani ndani kuna mishe gani sijui alikua anapiga huko. Sasa jamaa kutokana na hali ya kule baridi na nini akakamatia guluguja moja matata akawa anasogeza nalo siku kiaina. Mara paap.. likanasa ujauzito! Jamaa kapambana nalo sana litoe likagoma kabisaa na likaamua kuhamia geto anapokaa mshkaji likadai limefukuzwa kwao.

Jamaa kuona ivyo akaona isiwe tabu akali taimu akabeba vitu vyake vichache akaliachia geto yeye akarudi zake chuga maskani. Maisha yakaendelea kama kawaida jamaa akasahau kabisa kuhusu lile guluguja tukawa tunagombania magoli kitaa.

Siku ya siku tumekaa zetu kibarazani tunapiga stori mbili tatu na mwana mara tunaona polygon shape moja ina tumbo kubwaa inakuja uelekeo wetu. Kadri ilivyokua inatusogelea ndio mwana anazidi kuwa mwekundu maana jamaa alikua mweupe. Aisee jamaa hakuamini lile guluguja limekuja likiulizia mpaka likafika home!! Jamaa ndio kukalishwa na wazee pale akabanwa akakubali kweli yeye ni mhusika. Basi ikabidi jamaa awe mpole tuu na guluguja lake sasa atafanyaje? Mtoto amekuja kuzaliwa yaani ni fotokopi huulizi kitu. Mpaka leo tunavyoongea jamaa yuko na guluguja lake maisha yanaenda.
Haaaa haaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sio wewe kweli haaa haaa guluguja lako?

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kumaliza chuo, nikatafuta kashule kujishikiza nikisubiri ajira ya nilichosomea. Kuna wiki nilikua mwalimu wa zamu, ukiwa zamu unakaa skuli hadi weekends jmos na j2.

Sasa jumamosi hiyo akaja huyo binti. Aliwahi soma hapo kabla sijaja, kaja kufata vyeti vyake.. nkamwambia vyeti vinakaa ofisi ya mkuu, na mkuu yupo siku za kazi. Nikachukua namba kwamba jumatatu kabla hajaja nimcheki kama mkuu yupo au laa.

Siku ile ile nkaanza mtongoza kwa simu. Na wakati huo plan yangu ilikua nipite tuu maana nilikua na mchumba wangu nesi ambae nasubiri nipate ajira rasmi nioe.

Siku nyingine ya kazi kaja kuchukua cheti, jioni kapitia geto, ingawa alininyima mzigo kisa bado mapema.. ila weekend inayofata alikuna geto na akanipa mzigo.

So nikawa na mademu wawili rasmi. Tatzo likaanza, nkaona namna anavonihendo huyu denti, ni tofauti na mchumba wangu nesi.
Denti akawa so romantic, ananiita mume wangu, ananijali mno. Basi nkawa naendelea kumla. Ghafla mimba hii hapa. Na nilijiwekeaga kwamba sitakuja kutoa mimba yangu. Nkasema usitoe ntaitunza.

Nahisi kwao walimshawishi ahamie maana nkaona anahamishia kimoja kimoja. Siku akija geto anaondoka baada ya siku 3, mara wiki mara akahamia mazima..

Nkafanya process za posa, nkalipa mahali, akajifungua sahv dogo ana 4yrs. Mwaka jana 2019 nmefunga nae ndoa. Na sahiv ni mama k.

Back to nesi, ile me kuoa ilimvuruga sana. Sababu anasema alikataa wengi kisa alikua na uhakika na mimi. Age ilikua imesonga alkua na 27yrs ile 2017. Mwaka jana nilipofunga ndoa yeye akiwa na 29yrs akagive up kuhusu kuolewa, akaamua atafute mtoto.. katka kutafuta mtoto akakutana na jamaa kumbe ni hiv +. So nesi nae akaukwaa. Mimba akipata zinatoka. Hadi sahv bado hajapata.. (Hizi story nazipata kwa shosti yake ambae me ni rafiki)
Sasa hii nayo ni ya kusimulia?
 
huwa natongoza dem bila kumwambia neno "nampenda" na ninamla naachana nae bila kumuita jina "mpenzi" hata siku moja
Mara ya mwsho nimeachana na dem kisa aliniuliza mimi ni nani kwako? Ase nikashindwa kutamka kuwa yeye ni "mpenzi wangu" nikawa najizungusha tu namwambia Kwan wewe hujui ni nan kwangu? Had tukagombana kisa sitak kumwambia yeye ni mpenzi...

Kwahiyo kwa kifup hiyo hali unayo iongelea sijawahi kukutana nayo

Mkuu bado unahezea watoto wa watu kama kamari
 
Mkuu Clinker belite nimesikitishwa sana na feedback yako kuhusu nesi,imeniuma mno,,but anyway hatujui mengi,ila as far as am concerned nimeona hujataja kama nesi alikuwa na tatizo lolote kwenye uhusiano wenu,

hivyo naomba uutambue ukweli huu ufuatao,kwenye Maisha huwa kuna kanuni,kanuni za Maisha ambazo hazijaandikwa mahala popote lakini zipo na zinafanya kazi,na zina majibu yasiyobadilika kamwe nenda uendako,duniani pote.

KAMWE USICHEZE NA HISIA ZA MTU nimeandika kwa herufi kubwa na nikabold kuonesha msisitizo,

mkuu hii ni mbaya sana,hakuna ambaye amewahi kucheza na hisia za mtu aliwahi kubaki salama hata mara moja labda afe

hivyo na wewe mkuu,kama kweli nesi wa watu hakufanya kosa lolote kwenye mahusiano yenu na feedback ndo hiyo unayotupa as if hukuwa wa kwanza kuyavunja mahusiano yenu,nahofia sana kinachokuja huko mbeleni kwako.(unless otherwise story iwe tofauti na hukuiweka wazi hapa)
Mkuu nmekupata.. lakini kosa nililofanya hapo si kutomuoa nesi. Sababu hata ningeamua kumuoa nesi ningetesa hisia za huyu mama kijacho aliyeshika mimba yangu. So sikua na option..

Kosa nililofanya ni kutokua mwaminifu na kuanza kucheat na mwanamke mwingine. Hilo nalikubali.

Na kosa jingine nadhan members wengi humu hawajanielewa ni namna nilivosimulia.. as if ni kitu poa. Nakiri usimuliaji haujakaa sawa. Lakini si kitu poa, na nesi nipo nae fresh na iliniuma saana situation aliyopitia.
 
Back
Top Bottom