Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu


wabongo pia hua tuna tabia ya kupangiana jinsi ya kuishi
kwa mfano mimi ni mtu mkimya, na muda mwingi kichwani nina matatizo yangu, najikuta mkimya na sisalimii watu sometime ,hii huwafanya watu kusema nalinga


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwanini haujashtaki mkuu
 
kipnd chetu mlokoz ndo alikua jau sn

Nakumbuka Mlokoz alikuwa na Teacher mmoja anaitwa Lutwaza, ana tumbo kubwa hivi, dah hawa jamaa walitufanya tuishie mchikichini aisee yaan ukichelewa tu, ni shidaa, zinapigwa fimbo kama anauliwa nyoka. Ila kutoka miaka ya 90 kuja 2000 mwanzoni, Teacher mtata alikuwa Mchwa, dah! huyu kila aliyesoma Azania miaka ya 90 kuja 2000 huwa anamkumbuka
 
Nimesoma na jamaa mmoja jina la kistaa nicolyner alikuwa social prefect mzumbe sec Ila bdo hajatoka kimziki ila kuna dogo anajiita jozzination anaimba nyaturu trap atatoka mda sio mrefu mtamsikia kwa hewa akitamba.
 
Barnaba ila Acha kudanganya uma kuwa ulifika sec tena siku ya mtihani wa Taifa ukatoroka ili kwendavkufanya odition THT, niongo wapo wanaokujua ambao ulisoma nao mkwawa Premary kigogo
Wanasema shule yenyewe uliacha Kati hukumaliza ndg
Ila Ruge alikupika na akakupanga ukiwa maarufu sema hivi kuhusu Elimu yako ili kulinda heshima

Wasanii acheni uongo kuhusu Elimu zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami nichangie huu Uzi! Shule ya msingi nimesoma na Happy Magese ( aliwahi kuwa miss Tz) Shule inaitwa Kiwandani kule Mtibwa, alinizidi madarasa 5 ! Alikuwa anacheza sana Netball! Sekondari - Mafinga sec siku hizi inaitwa JJ Mungai nilisoma na Rashidi Abdala Makwilo a.k.a Chidi benz mtoto wa Ilala! Pia mkuu wa wilaya ya Kinondoni Daniel Chongole tulikuwa nae Mafinga sec!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngozye ukikaa vibaya unakula bonge la mkofi!!

5 PCM mwanangu mashola kakutana mlangoni na ngozie, akala bonge la mkofi! Dk 2 shavu loote alama ya mkono.
Oy kaveli mwanao mashola yuko wapi skuizi ..kitambo sana
 
Nimesoma na mdogo ake Millard ayo...umbwe sec - moshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…