Tupeane connection za mashamba/viwanja vya gharama nafuu

Tupeane connection za mashamba/viwanja vya gharama nafuu

kwenye kununua eneo umakini unatakiwa sana kuna sehemu bagamoyo bei ndogo lakini eneo ni la serkali japo watu wanaishi
Bagamoyo ni balaa sana, kuna Nafco, kuna RAZABA na kuna National park ya Sadaan, na kuna Ranch, na kuna mafisadi waliojitwalia mipori pia.
 
Wapi huko mkuu?
samahani nilisahau kueleza location, hiki kipande kipo kijiji cha Marogoro, Mkuranga. Ukitaka kwenda huko unapitia Vikindu, Vianzi, Mfuru Mwambao kisha marogoro. Unaweza pitia Kisarawe II, Dsm zoo, Mwasonga mpaka hapo.
 
SHAMBA SHAMBA SHAMBA..!
lipo Barabara ya Mlandizi-Bagamayo kijiji kinaitwa Sunguvuni,linapakana na kiwanda kipya cha Hill water,namanisha mpaka wake ni ukuta wa kiwanda.
Zipo heka 5 linauzwa lote MILLIONI 37.
N.B HAKUNA DALALI MIMI NDO MWENYE SHAMBA.
 
samahani nilisahau kueleza location, hiki kipande kipo kijiji cha Marogoro, Mkuranga. Ukitaka kwenda huko unapitia Vikindu, Vianzi, Mfuru Mwambao kisha marogoro. Unaweza pitia Kisarawe II, Dsm zoo, Mwasonga mpaka hapo.
Aisee umenikumbusha Shungubweni we Mzee. Wale Mbuzi bado wapo eee?
 
Hello wanajukwaa,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Naomba tupeane connection za maeneo ambayo kuna viwanja au mashamba makubwa kwa bei nafuu kwaajili ya uwekezaji au ujenzi.

Mimi binafsi niko Dar, natamani sana kupata eneo au shamba lenye rutuba nzuri angalau ekari 10 pembezoni mwa jiji au katika mkoa wa Pwani kwa gharama ya wastani wa milioni moja (1,000,000Tsh) ili nikajichimbie huko nilime na kufuga. Maeneo ninayopendelea ni kama Kisarawe, Chanika (ndanindani huko), Bagamoyo, Wilaya ya Kibaya, Mkuranga n.k.

Asanteni
We pwani kwa hela ya nyanya hiyo huwezi ,, cha kukushauri njoo Lindi ubebe ekari mia kwa iyo hela
 
Nauza shamba langu lipo mkoa wa pwani wilaya ya chalinze kijiji cha Kibindu lina ukubwa wa heka 20 pia lina banda la kufugia mifugo.

Jirani kuna uchimbaji wa madini pia

Price: 6M
 
Watu wa viwanja Arusha na Dodoma mko wapi?
 
Mkamba ni kuzuri kwa kilimo, mvua mara mbili kwa mwaka, ukitaka kwenda huko, pitia Mkuranga, ukifika Mkiu unaingia kulia, ndani ndani huko. Changamoto ni manpower, kwa kilimo ndo kwenyewe.
Huko ndo kwetu saaaasa. Mkamba kizapara, mbulani mpka kibudi.
 
Back
Top Bottom