Tupeane updates za Ajira za Polisi 2024

Tupeane updates za Ajira za Polisi 2024

CCP Ni Kambi Mama Kwa Mafunzo Ya Jeshi La Polisi Pamoja Na Kuwa Ina Kambi Nyingine Mbili Zilizopo Kilimanjaro Pia Zinazoitwa KAMBAPORI Na KILELEPORI. .. CCP Ni Kambi Kubwa Kwa KWELII, Majengo Ya KUTOSHA Na Wakufunzi Waliobobea Kwenye Mafunzo.

Sifa Za Kutoboa Ni NIDHAMU Cha Kwanza, UVUMILIVU Ndo Jambo Mama Maana Nidhamu Lazima Itakuja Maana Wote Ni Watafutaji Na Lengo Ni Kumaliza Kozi Kazi Za Watu Ziendelee.

Kama Kawaida Kila Siku Mtaamka Saa 8 Usiku Mabio Almost Kilomita 7 Kuzunguka Kambi Nzima... Hamtakimbia Jumapili Tu Pamoja Na Siku Za Sikukuu Tu.

Mbali Na Mafunzo AFYA Ndo MTAJI Wako Muhimu Ili Umalize Mafunzo, Tunza Afya Yako... Vaa Viatu Vizuri Vyenye Soli Kubwa Chini.

Acha Kujionesha Mbele Ya Maafande, Acha Sifa Za Kutaka Kuonesha UNAA Mbele Ya Wenzio Na Maafande.

Ushirikiano Na Wenzio/Viongozi Wa Platoon/Kombania Ndo Itakufanya Umalize Kozi.

Hudhuria Fatiki/Kazi Zote Zilizopangwa Acha Kudoji Vipindi Mbalimbali


Mbaya Zaidi Lugha Za Matusi, Kupigana Na Kuibiana Ni Jambo Ambalo Huwezi Kusamehewa Kamwe Ni Kufukuzwa.

Mapenzi Mwiko Kambini... Uvumilie

Mengi Zaidi Tutajuzana... Mwenye Swali Lolote Anakaribishwa Nitajitahidi Kujibu Kadiri Navyoona Inafaa Bila Kupotosha Jambo.


Asante.
Afande,umetisha
 
Mbona hayo mambo kama jkt tuu aiseee nahisi kwa sisi wa jkt hapo kinachoongezeka ni masomo tni

Mbona hayo mambo kama jkt tuu aiseee nahisi kwa sisi wa jkt hapo kinachoongezeka ni masomo tuu
IPO HIVI,SIKU ZOTE MAFUNZO YA UASKARI(POLISI/MAGEREZA/JWTZ/ZIMAMOTO) HUWA YANAFANANA KWA ROBO TATU.YAANI 70% NI YALE YALE.UKITOKA JKT UKAENDA CCP,KIWIRA,AU KIHANGAIKO AU MAFINGA UTAKUTA MIPANGILIO YA MAFUNZO NI YALE YALE NA VINAFANANA.DRILL KOTE ZIPO,DARASANI HATA JWTZ WANAKAA AMBAPO NDO KUSOMA KIUELEWA ZAIDI SIO NGUVU.KINACHOONGEZEKA HAPO NI ILEEEE ELIMU YA JESHI HUSIKA,YAANI MFANO POLISI UTAJIFUNZA CRIMES KAMA UKAMATAJI..KUPAMBANA NA UHALIFU UPELELEZI..USALAMA BARABARANI..,MAGEREZA UTAJIFUNZA KUTUNZA WAHALIFU TABIA ZAO NA NAMNA YA KUWAKABILI,SASA UKIJA NJE YA DARASA UTAONA KUNA MAMBO YA MEDANI ZA KIVITA AMBAYO JKT,MAGER, POLISI,NK WANAYAPITIA.
 
IPO HIVI,SIKU ZOTE MAFUNZO YA UASKARI(POLISI/MAGEREZA/JWTZ/ZIMAMOTO) HUWA YANAFANANA KWA ROBO TATU.YAANI 70% NI YALE YALE.UKITOKA JKT UKAENDA CCP,KIWIRA,AU KIHANGAIKO AU MAFINGA UTAKUTA MIPANGILIO YA MAFUNZO NI YALE YALE NA VINAFANANA.DRILL KOTE ZIPO,DARASANI HATA JWTZ WANAKAA AMBAPO NDO KUSOMA KIUELEWA ZAIDI SIO NGUVU.KINACHOONGEZEKA HAPO NI ILEEEE ELIMU YA JESHI HUSIKA,YAANI MFANO POLISI UTAJIFUNZA CRIMES KAMA UKAMATAJI..KUPAMBANA NA UHALIFU UPELELEZI..USALAMA BARABARANI..,MAGEREZA UTAJIFUNZA KUTUNZA WAHALIFU TABIA ZAO NA NAMNA YA KUWAKABILI,SASA UKIJA NJE YA DARASA UTAONA KUNA MAMBO YA MEDANI ZA KIVITA AMBAYO JKT,MAGER, POLISI,NK WANAYAPITIA.
Mkuu wewe hapa ndo umeongea....
Maana kuna jamaa kaja kuongea mambo deep kihisia sana ety mara nidhamu mara jkt jau..

Yani jamaa ni kuponda jkt tuu
 
Yaaani kuhusu majina kutokea kwenye pdf Haina shida ila kutoboa kwenye interview ndo kipengere coz naskia apa kupita ni karibia wote walioomba Kwa usahihi issue kwenye interview tuuu
Hapo kwenye interview tutavunjana mbavu mpaka kieleweke
 
Kuna mda mnaambiwa muwe mna kloo sasa kipindi mna kloo unakuta mpo wengi hvo wanachotakaa muwe fasta hvo hapo ndo fimbo zinapoanza wanaoshika fimbo ni wale service man.

Naposema fimbo sio vigongo hapana ila ni mikwaju ya kawaida tu ila kwa lile wenge mnakua mnaogopa sana.

Mda huo unafanya yote upo na binduki yako..

Sasa ole wako badae bunduki yako ikutwe haina kifaa fulani.. oyaa weeeh utajutra
Au mkufunzi akufichie bunduki
 
Sasa ilo bogi si limeingia mwez wa12 sasa litatokaje mwezi huu? means yani wanatoka wamepiga kozi miez7!! Mbona kama sio kweli
Usiangalie bog limeingia muda gan asikudanganye mtu jeshini bog linaweza kupiga miez 9 lingne mwaka, lingne miez5 kulingana na uhitaji
 
Mbona kuna mishahara ya ajabu ajabu hivo..
Sasa mimi askari wa kawaidi si nitakua napata laki na nusu aisee
Hapa kuna orodha ya baadhi ya vyeo vya polisi nchini Tanzania pamoja na makadirio ya mishahara yao. Mishahara inaweza kutofautiana kulingana na kiwango cha uzoefu, elimu, na nafasi maalum za kazi:

### Vyeo vya Polisi na Makadirio ya Mishahara
1. Koplo (Constable):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 300,000 - 450,000 kwa mwezi

2. Koplo Mkuu (Corporal):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 350,000 - 500,000 kwa mwezi

3. Sajenti (Sergeant):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 400,000 - 550,000 kwa mwezi

4. Staff Sajenti (Staff Sergeant):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 450,000 - 600,000 kwa mwezi

5. Inspekta Msaidizi (Assistant Inspector):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 500,000 - 650,000 kwa mwezi

6. Inspekta (Inspector):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 600,000 - 800,000 kwa mwezi

7. Mkaguzi Msaidizi (Assistant Superintendent):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 700,000 - 900,000 kwa mwezi

8. Mkaguzi (Superintendent):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 800,000 - 1,000,000 kwa mwezi

9. Mrakibu Msaidizi (Assistant Commissioner):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 1,000,000 - 1,200,000 kwa mwezi

10. Mrakibu (Commissioner):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 1,200,000 - 1,500,000 kwa mwezi

11. Mrakibu Mkuu (Senior Commissioner):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 1,500,000 - 2,000,000 kwa mwezi

12. Kamishna Msaidizi (Assistant Commissioner of Police):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 2,000,000 - 2,500,000 kwa mwezi

13. Kamishna (Commissioner of Police):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 2,500,000 - 3,000,000 kwa mwezi

14. Kamishna Mkuu (Inspector General of Police - IGP):
- Makadirio ya Mshahara: TZS 3,000,000 na zaidi kwa mwezi

### Posho na Marupurupu
Mbali na mshahara wa msingi, polisi nchini Tanzania pia hupata posho na marupurupu mbalimbali, kama vile:

  • Posho ya Nyumba: Inategemea cheo na eneo la kazi, inaweza kuwa TZS 50,000 - 200,000 kwa mwezi.
  • Posho ya Usafiri: Inategemea cheo na aina ya kazi, inaweza kuwa TZS 50,000 - 150,000 kwa mwezi.
  • Posho ya Hatari: Kwa kazi zinazohusisha hatari kubwa, inaweza kuwa TZS 100,000 - 300,000 kwa mwezi.
  • Posho za Kazi za Ziada: Inategemea aina ya kazi na muda wa ziada, inaweza kuwa TZS 50,000 - 150,000 kwa mwezi.

Makadirio haya ni ya jumla na yanaweza kutofautiana kulingana na sera za ajira, bajeti ya serikali, na mabadiliko ya kiuchumi. Kwa taarifa za kina na sahihi zaidi, ni vyema kuwasiliana moja kwa moja na Jeshi la Polisi la Tanzania au kitengo cha utumishi cha polisi.
yaani mshahara wa msaidizi(superintendent) ndio unafikia private aa jwtz aisee 😂😂😂
 
Back
Top Bottom