Ndugu wanabodi mimi naomba kupendekeza kama kunaweza kupatikana taasisi yoyote iwe ndani au nje ya nchi yenye kuheshimika na kuaminika isiyo na upande wowote basi tuialike iwaite mezani serikali na chadema ili kuondoa hizi chokochoko zinazowndelea.
Serikali inaweza kudharau na kuona kana kwamba hawa wanaoongea ongea ni kakikundi kadogo ambako hakana nguvu sana hivyo katadhibitiwa tu.
Nikumbushe tu kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha inaweza kuwa kweli ni wachache lkn kile wanacho kitaka kina mantiki kwa kiwango gani?
Ni muhimu sana kupunguza hiyo tension kwa kuongea kuliko kutumia mbavu na maguvu.
Nakumbushia hata mapinduzi ya Tunisia yalianza na kijana mmoja aliyechomewa toroli lake.
Nimalizie na busara za mwl Nyerere alipoambiwa kwamba kwa nini anaondoka wakati wasiomtaka ni wachache tu!?
Alijibu NAONDOKA KWA SABABU SITAKI KUSUBIRI WANAONIPINGA WAWE WENGI.
Tasisi husika inatakiwa iwe huru kweli. Ni jambo jema, kwani wanasiasa wakiwa wengi sehemu/kwenye chombo husika hapo ndani mabishano yatakuwa yale ya katiba mpya, kuvutia upande wa mhusika mpaka jambo livurugike.
Naamini kama serikali na chama tawala zingekuwa zinafanyia kazi maoni chanya ya waangalizi wa kimataifa kila baada ya uchaguzi, tungekuwa sehemu nzuri sana.
Cha muhimu ni:
1: Wale wenye masilahi ya kisiasa wahimili tamaa na kibri cha kibinadamu na kuona kuwa hayo waliyonayo yanatoka kwa wanaowaongoza. Huwezi kuwashinda unaowaongoza kwa kuwasukuma wasikokutaka, ni suala la muda tu.
2: Watambue thamani ya Umoja kati ya muongoza na waongozwa. Huwezi kusimika AMANI ndani ya roho zinazougulia maumivu ya ukosefu wa HAKI za msingi.
3: Kuondoa figisu inahitaji:
(i) kupata watu ambao kwa miaka 10-15 ijayo hawana na hawatakuwa na mpango wa kuwa kwenye siasa/uongozi au pia waunganishwe na wale waliotumikia nchi kwa uaminifu na wamepumzika/si wanasiasa bali kwenye uongozi wa kitaaluma.
(ii)Uwakirishi sawa wa vikundi mbalimbali hitajika au taasisi zilizosajiriwa za kitaaluma na wananchi wa kawaida. mfano: TLS.
(iii) Wanasiasa wakubali kukaa pembeni au wawe na uwakilishi sawa mfano, mtu mmoja toka kila chama kama mwakilishi. Watu wasiozidi 100 wakiwa na mchanganyiko wa upeo wa kisheria ndani yake, wakae na kutupatia dira ya haya yote kwa wakati.
Ndani ya miezi miwili haya mambo yamekwisha na mengine kufanyiwa kazi baadae kwani hakuna cha kuvumbua bali kupanga kwa kuzingatie wenzetu huko duniani wanafanyaje na sisi letu tulifanyeje kwa manufaa ya wote kuendana na wakati tulionao.
Mambo muhimu:
1: Tume ya uchaguzi: kwa sasa
2: Sheria za uchaguzi: kwa sasa
3: Katiba: baadae
NB:
Ni rahisi kuona kuwa sisi hayatuhusu au haiwezekani mabaya kutukuta, lakini mbuyu ulianza kama mchicha(lugha ya picha), hivyo ni vyema kufanyia kazi kasoro hizi kwa mkutadha wa uhai wa taifa letu. Tusijekukumbuka shuka wakati kumekucha.