Tupendekeze taasisi neutral yenye kuheshimika ili iwaite mezani Samia na CHADEMA kutuliza hali!

Ndugu wanabodi mimi naomba kupendekeza kama kunaweza kupatikana taasisi yoyote iwe ndani au nje ya nchi yenye kuheshimika na kuaminika isiyo na upande wowote basi tuialike iwaite mezani serikali na chadema ili kuondoa hizi chokochoko zinazowndelea.

Serikali inaweza kudharau na kuona kana kwamba hawa wanaoongea ongea ni kakikundi kadogo ambako hakana nguvu sana hivyo katadhibitiwa tu.

Nikumbushe tu kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha inaweza kuwa kweli ni wachache lkn kile wanacho kitaka kina mantiki kwa kiwango gani?

Ni muhimu sana kupunguza hiyo tension kwa kuongea kuliko kutumia mbavu na maguvu.
Nakumbushia hata mapinduzi ya Tunisia yalianza na kijana mmoja aliyechomewa toroli lake.

Nimalizie na busara za mwl Nyerere alipoambiwa kwamba kwa nini anaondoka wakati wasiomtaka ni wachache tu!?

Alijibu NAONDOKA KWA SABABU SITAKI KUSUBIRI WANAONIPINGA WAWE WENGI.
Unataka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akae na Chadema kwa ajili ya mgogoro gani? Yaani mtu anavunja Sheria eti akae na viongozi? Huyo ni wa kushughulikiwa!!
 
Acha kutupotezea muda..kwani CHADEMA ni nani kwenye hii nchi?
 
Unataka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akae na Chadema kwa ajili ya mgogoro gani? Yaani mtu anavunja Sheria eti akae na viongozi? Huyo ni wa kushughulikiwa!!
Tatizo haliko kwenye kuvunja sheria ukishamuonea mtu tarajia reaction ya aina yoyote na hiyo huwa haitabiliki inaweza kuleta madhara makubwa zaidi
 
wakishakaa kwenye vikao waanze kudai posho, waende mahakamani na kesi wakishindwa walipe gharama za kesi
 
WAcha tuone hao CHADEMA wachukuwe serikali kwa njia wanazozijua wao za mkato ,si wanatafuta wananchi wa kuwasapoti katika kutimiza malengo yao,

Ila wito kwa wananchi watazameni hawa viongozi wa Chadema kama mnavyotazama mpira wa kombe la dunia , hawa kwa sura zao wakipata uongozi wa Nchi wananchi mtalia kilio cha mbwa mdomo juu.
Viongozi wa Chadema hawajapata uongozi wanavaa nguo za mgambo ,sasa wakishapindua nchi si watavaa maguo ya SNIPERS.

Ni bora wananchi walivyowaachia mpira wao pale Kariakoo , Viongozi wamo ndani ya magari ya bei mbaya wakihamasisha wananchi wajiunge nao ili pakitokea la kutokea wao wakimbie wawaache wananchi wakipambana na polisi ,yaani Chadema wanajifanya wana akili sana ,ila wananchi wa Tanganyika wameshituka zamani.

Ni vizuri hawa viongozi wakaonesha mfano ,timu ya viongozi wa Chadema na magwanda yao ya mgambo wakajipanga na kufanya maandamano hadi iKulu , ,nafikiri safu ya uongozi wa Chama iliyowahi kufanya maandamano ni CUF ,na pia waliwahi kuitisha maandamano ya Nchi nzima na wananchi wakaitikia.
Hupaswi kupima mambo kwa mrengo huo utakosea sana hata tunatamani tuwe na mfumo wa kuchagua ambao kiongozi anafanya kazi kwa kuwaheshimu sana anaowaongoza kuliko huu wa sasa ambapo mtu anajua hata akiwadharau sio ninyi mlio muweka
 
Mama Samia hawezi kupoteza muda wake wa kuhudumia watanzania kukaa mezani kuongea na hao wahuni kina Lissu na Heche wanaomwita kwa dharau Mama Abdul. Hao wakae chini waongee na John Mrema ndo size yao.
Kama ulikuwa hujui labda nikuelimishe kidogo ukisha kuwa kiongozi huwi Mungu mtu ni jukumu lako kukaa na kuwaaikiliza wote walioko chini yao kwani sehemu ya kodi yao inakulipa mshahara na umeapa kuwatumikia bila ubaguzi
 
Kazi kwenu, mkiweka ugoko tunaweka jiwe
Ni muhimu sana papatikane suluhu kwa bahati nzuri suluhu yenyewe si jambo zito sana.
Ni kwamba huu uwanja wa uchaguzi ulevo sio uwanja umeinama hadi kipofu anaona.
 
Kama ulikuwa hujui labda nikuelimishe kidogo ukisha kuwa kiongozi huwi Mungu mtu ni jukumu lako kukaa na kuwaaikiliza wote walioko chini yao kwani sehemu ya kodi yao inakulipa mshahara na umeapa kuwatumikia bila ubaguzi
Sio kwa kulazimishwa na kilaza kama wewe. Kasome ibara ya 46 ya katiba ya JMT ili ujue Rais halazimiki kufuata ushauri wa yeyote.
 
Rais halazumishwi na mtu katika kutekeleza majukumu yake lkn ana wajibu wa kuwasikiliza watu kwani sio dictator bali ni kiongozi
 
Ndugu wanabodi mimi naomba kupendekeza kama kunaweza kupatikana taasisi yoyote iwe ndani au nje ya nchi yenye kuheshimika na kuaminika isiyo na upande wowote basi tuialike iwaite mezani serikali na chadema ili kuondoa hizi chokochoko zinazowndelea.

Serikali inaweza kudharau na kuona kana kwamba hawa wanaoongea ongea ni kakikundi kadogo ambako hakana nguvu sana hivyo katadhibitiwa tu.

Nikumbushe tu kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha inaweza kuwa kweli ni wachache lkn kile wanacho kitaka kina mantiki kwa kiwango gani?

Ni muhimu sana kupunguza hiyo tension kwa kuongea kuliko kutumia mbavu na maguvu.
Nakumbushia hata mapinduzi ya Tunisia yalianza na kijana mmoja aliyechomewa toroli lake.

Nimalizie na busara za mwl Nyerere alipoambiwa kwamba kwa nini anaondoka wakati wasiomtaka ni wachache tu!?

Alijibu NAONDOKA KWA SABABU SITAKI KUSUBIRI WANAONIPINGA WAWE WENGI.
Washika matonge hawatakuelewa kwasababu hawajawahi kuiona nguvu ya umma ya kitanzania , na Ndiyo maana wakiaambiwa tutakinukisha wanakuambia kama hunuki utakinukishaje?
 
Back
Top Bottom