Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Aisee, kulikuwa na mmoja huyo alipata kuitwa Olengavuti Losujaki aka Chief (RIP) pande za Ilboru. Ni mmasai pekee mpaka sasa niliyemuoa akiwa na sauti ya bezi.

Aisee huyu jamaa ilikuwa usiombe ukutane ama upambanishwe naye kuwa umetenda kosa. Utaomba ardhi ipasuke.
 
musoma tech(alliance) kulikuwa na mwl.mikomangwa alikuwa ni noma.. lakini alikomeshwa baada kupigwa mimba mabinti zake wawili
Dah mkuu rolla, umenikumbusha mbali mikomangwa akikusonta na kale kakidole kake kalikopinda na kakidevu....ujue umepatwa siku hiyo. Discipline master
 
Katika shule/chuo hakosekani mwalimu msumbufu na ambaye huwafuatilia sana wanafunzi hata ktk mambo madogo madogo na kuwapa adhabu za ajabu ajabu.

Leo nataka tuwakumbuke walimu hawa pamoja na kujikumbusha vituko walivyowahi kuvifanya.

Mimi shuleni kwetu Mara Sekondari kulikuwa na mwalimu mmoja aliyeitwa Jigge. Basi siku moja kuna wanafunzi walitoroka kwenda mjini bila ruhusa. Na kibaya zaidi, walipokuwa huko mjini wakafanya fujo na kuharibu mali za wananchi.

Taarifa zao zikafika shuleni. Ilikuwa jioni na kiza kilikuwa kimeanza kukolea. Mwalimu Jigge akapiga kengere. Wanafunzi wote tuliokuwepo shuleni tukakusanyika bwaloni na akaanza kuchuka roll call.

Ili kumkomesha mwalimu huyu, pamoja na kuwanusuru wale wanafunzi 'wahalifu' waliokuwa wamefanya tukio mjini, wanafunzi wakapanga kuzima umeme main switch na kumpopoa kwa mawe. Ghafla tu, umeme ulipozimika, mwalimu alichomoka kama mshale na kutokomea kizani. Wanafunzi walimtupia mawe lakini, kwa ile speed aliyochomoka, hakuna jiwe lililompata. Ana bahati sana.

Ila nyie Mara sec mlikua manunda sana bila kama akina mwl Jigge mngewapanda kichwani
 
Namkumbuka sana huyo jina lake aliitwa Pastory Mikomangwa aka mikoma-G, alikua msukuma na mabinti zake walikua weupe pee. Alikua akikutana nawe kule mjini au baruti anakukariri sura na akija shule kesho yake lazima akukamate paredi.

"musoma shule ya sekondari, ufundi Tanzania ..." wimbo wa shule nimeukumbuka mwanzo wake
Alikua hakujui jina lakini anakusonta kukunyoshea kidole chake kile kilichopinda kama antena ya analogy tv
 
SINGE HIGH SCHOOL Babati kuna ticha alikuea anaitwa Njiku the animal a.k.a PANGEA alipewa hilo jina kutokana na kugawanyika meno yake kugawanyika [emoji23][emoji23][emoji23] aiseeh jomba alikuwa anababua asikutie kwenye 18 zake utajuta hajuagi mtu kujitetea aiseeh miaka ile tunasoma aliwai piga mtu mpaka akazimia.
 
Charles Lupemba enzi hizo Lutengano High school 2008-2010 alikuwa akikuona na demu aliyemkatalia atakuchafua assembly kuwa ni mshika mapembe,kwa sasa yuko songea st.patrick sijui nako anaendeleza ujinga huo
 
Primary- Mwalimu Walisimba, mnoko huyu balaa
O-level- Kilawa B., huyu ni aibu
A-level- Mama Kitembe, Man Shida na Kihongosi, hawa dunia ilikua salama bila uwepo wao,
Chuo- Maseminar leader karibu wote wakiongozwa na Sabato Nyamsenda, Prof. Nyirabu alibana nusu nicarry.
Man Shida na Kihongosi ni balaa
 
Back
Top Bottom