CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,296
- 12,972
Una kumbukumbu hatari. Yule Andunje.........ila umemsahau Kiganja
Yaah namkumbuka, Kiganja yaan saiv alivyopoa acha. SIjui umri, naye alikuwa moto wa kuotea mbali.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Una kumbukumbu hatari. Yule Andunje.........ila umemsahau Kiganja
Ossoro UDSM
Ossoro UDSM
Ossoro.....
old moshi ticha anaitwa kinunda asee kwanza akiingia tu class unahisi kampuni ya fegi imeungua. Ila yuko deep sana kwenye math.
Hahahaha! Yaani hata sipati picha jinsi huyo mwalimu alivyokuwa akiwabutua hayo amateke!
Umenikumbusha Mwalimu Pius wa shukleni kwetu Mara Sekondari enzi zile za 1990's. Mwanafunzi ukifanya kosa, alikuwa hana haja ya kukukimbiza--yeye alikuwa akiokota fungu la mawe na kuanza kukutungua nayo--jitihada zako za kuyakwepa ndio 'msalie mtume' wako--ukikosea kukwepa, ngeo zinakuhusu! Yaani full movie nikikumbuka enzi zile. hahahahaha!
Katika shule/chuo hakosekani mwalimu msumbufu na ambaye huwafuatilia sana wanafunzi hata ktk mambo madogo madogo na kuwapa adhabu za ajabu ajabu.
Leo nataka tuwakumbuke walimu hawa pamoja na kujikumbusha vituko walivyowahi kuvifanya.
Mimi shuleni kwetu Mara Sekondari kulikuwa na mwalimu mmoja aliyeitwa Jigge. Basi siku moja kuna wanafunzi walitoroka kwenda mjini bila ruhusa. Na kibaya zaidi, walipokuwa huko mjini wakafanya fujo na kuharibu mali za wananchi. Taarifa zao zikafika shuleni. Ilikuwa jioni na kiza kilikuwa kimeanza kukolea. Mwalimu Jigge akapiga kengere. Wanafunzi wote tuliokuwepo shuleni tukakusanyika bwaloni na akaanza kuchuka roll call.
Ili kumkomesha mwalimu huyu, pamoja na kuwanusuru wale wanafunzi 'wahalifu' waliokuwa wamefanya tukio mjini, wanafunzi wakapanga kuzima umeme main switch na kumpopoa kwa mawe. Ghafla tu, umeme ulipozimika, mwalimu alichomoka kama mshale na kutokomea kizani. Wanafunzi walimtupia mawe lakini, kwa ile speed aliyochomoka, hakuna jiwe lililompata. Ana bahati sana.
Namkumbuja Credo Celestine IFM, Mtaalamu wa Quantitative Techniques
mwl donge mwenge high xul,mwl kitoko tarime high xul,mwl malilika korogwe primary xul kahama,mwl doto old shy
Namkumbuka mkuu wa shule Kaishozi wa DODOMA SECONDARY miaka ya 92-96 sita msahau kwa wale waliosoma DOM SEC natumaini watamkumbuka alikuwa kama anapasha kwanza weed then ndiyo anaingia kazini.
Mwaka jana nienda Dodoma kuna rafiki yangu alikuwa anaenda kutoa mahari wakati tunahangaika kupata mshenga ghafla aliingia kwenye kikao na akapendekezwa kuwa mshenga ambapo alikubali alichokifanya alipiga konyagi ndogo 2 na akaenda kuchukuwa kanzu yake tayari kwa kazi ya kuwa mshenga ajabu tukiwa ukweni wakati wsjumbe wengine wanaongea yeye alikuwa anauchapa usingizi haha haaaa nilicheka sana ilipofika wakati wake akakurupuka na kuanza kuongea watu si vicheko kwani inaonekana hakujua yanayoendelea hata huvyo baadaye mambo yalienda sawa.
Tulipopata fursa ya kusalimiana nilimkumbusha hasa siku aliponipa adhabu ya kukata bonge la mti then nikate viapande vya kuni nikaakataa so talifurahi sana.