Nchi yetu imepata laana kubwa awamu hii. Nina hakika hakuna wakati Taifa letu liliwahi kupata uongozi usio na maono, na primitive, kama awamu hii.
Hivi mtu mwenye hekima, utawezaje kusema wazungu wanatuletea chanjo ili tufe?
Chanjo za polio, tetenasi, kifaduro, kifua kikuu, ndui, surua, wote tumechanjwa, watoto wetu wanachanjwa, tena kea kusaidiwa bure. Hakuna hata chanjo moja ambayo Tanzania inalipia.
Madawa aghali kama ya cancer, kifua kikuu, HIV, yote tunasaidiwa bure. Mbona hajawahi kuyakataa?
Hiyo tiba ya moyo anayotembea nayo, walitengeneza Chato? Dawa tunazotumia mahospitalini, zinatengenezwa Chato? Magari anayotumia, yanatengenezwa Chato?
Kwa kweli huyu mtu ni laana kubwa kwa Taifa. Wakati wote ni kuropoka mambo ya ajabu! Amepewa hela za msaada kupambana na Covid 19, akapeleka kwenye uchaguzi, halafu anawadanganya wajinga kuwa tumefanya uchaguzi kwa mara ya kwanza kwa pesa zetu wenyewe. Hizo oesa za msaada zingeweza kununua mashine nyingi za kuwasaidia wagonjwa kupumua, hata wagonjwa ea magonjwa mengine, zingeweza kuboresha huduma za afya kwa kununua vifaa tiba ili kuondoa tatizo kubwa lililopo sasa ambapo hospitali nyingi kwa sasa na vituo vya afya, imekuwa ni majengo badala ya huduma za afya.
Sent using
Jamii Forums mobile app