Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

kwani tabora wapo waisilamu peke yake?taja mkoa wilaya au kijiji wakirisito au kanisa walipo jenga shule maji hosipitali barabala kisha watu wakawa wananufaika ukiweza taja vijiji waakoishi wakirito tu
Ukifika maeneo walifikia wamisheni wa Kikristo kuna maendeleo mazuri kupita maeneo walikofikia Waarabu Waislamu.
Walijenga Hospitali Vyuo na Secondali kwa ajiri ya wananchi wa pale.

Waarabu wao walijaza Musikiti tu basi.
Mfano Ndanda, Lituhi, Peramiho, huko kusini.
 
Huwa nawaambia vijana KUWA msipotoshwe na waarabu KWA kushika Dini wakati wao wanashika uchumi na huo uislamu umebaki kama utamaduni siyo dini tena kwao!

Nawaambia wakati nyie masikini mmekalia elimu akhera wenzenu wanakomaa na elimu za computer,udaktari,geology,Biashara na no na KUWA matajiri!!

Pole VIJANA!
 
Uislamu unaongoza kwa maendeleo ?

1.Taja idadi ya vyuo vikuu vya kiislamu hapa Tz.
vio vilivio jengwa na makanisa ndio ni vingi vina faida gani hasa kwa nyiyi wakirito? unaweza nitajia wakiristo wanao soma bule au kutibiwa ? je unajua kuwa serikali inawapa ruzuku kutoka kwenye kodi yetu? unasifia mali za watu ambazo azikusaidii wewe wala ndugu zako,hapa nikipo ni songea natoka nyasa walipo wakirito wengi nilicho kiona huku ni makanisa tu kazi yake kubwa kuwapola hela wakirito wenzao wasio jitambua lakini wakirito wengiwao huku wamepauka haswa ukirisito hauna faida katika jamii tufaoti na unyonyaji
 
Jamaa kwa misikiti wana bidii kiukweli. Kitaani kwetu misikiti ipo minne. Ya maskini waafrika upo wanapaita Kibrateni, waarabu nao wanao wa kwao mzuri kuliko Kibrateni. Afu kuna wa wapemba wanavaa suruali "njiwa" nao wameujenga siku sio nyingi. Walinunua nyumba mbili kibabe wakazivunja kujenga msikiti.
Pembeni ya msikiti kulikuwa bar wakanunua nyumba kibabe wakavunja wakajenga madrasa humo watoto wanajifungia na wengine hatujuagi wanapotoka waanaishi hapo hapo na Mwalimu wao. Kuna fimbo balaa hapo madrasa, watoto wanakula bakora hataree.
Wajenge ila waache ubaguzi kwenye misikiti. Maskini waafrika wanasali Kibra, Matajiri wanasali "Msikiti wa waarabu" wale wenye imani kali wana msikiti wao.
 
Kwani hakuna Mashehe Wachawi ?

Utapeli upo popote, ndio maana mmemfukuza Shehe wenu wa Mkoa shauri ya Utapeli.

Ninachosema Uislamu ndio Upinga Kristo.
Mfano halisi ni huko Pemba.

Dini ya Uislamu ilianzishwa ili kupinga Ukristo tu Basi.

Huku kitabu chenu kikikopi na kupotosha mafundisho na wahusika wa kwenye Biblia.

Hebu Jiulize
Pamoja na Qurani kuandikwa na Waislamu Waarabu wa Maka na Madina.
Mhusika pekee aliyetajwa kwenye Qurani ni Muhamadi.

Wahusika wengine wote ni Wayahudi wa kwenye Biblia.
Ukiondoa maneno na wahusika wa kwenye Biblia Qurani inabaki tupu kabisa.
Kama Gazeti tu.
Pamoja ya yesu kuwa muisrael ila dini yenu imetokea Italy na uingereza sio Israel .


Nyie ni matapeli taasisi za wazungu kijana fanya kutubu acha kufuata wazungu
 
Kuna kijiji chaitwa Njopeka kiko kati ya Jaribu na Mkiu.
Kiko karibu na Kiwanda cha Vigae na Vioo

Ile sehemu misikiti ni mingi sana, wenyeji hawataki pale pajengwe guest house kwamba zitasababisha uzinzi eneo hilo, hiyo yafanya watu walale jaribu au mkiu au kimanzi
 
Ivyo vyuo hapo vyote takataka kama vyuo vya kata hamna cha maana..siwezi kusoma.

Unaongelea vyuo wangapi wanafaulu wanashindwa kulipa ada..Hapa ni ishu za kusaidiana tunajua majority wengi ni maskini sasa utakwamua vip .

Ivyo kweny list narudia ni takataka Tena havina kitu kabisa..
Vyuo local sana hivyo

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Wasiowaislam wanajenga hospital za kuhudumia watu wote wewe unasema za kuhudumia waislam...Hamuwezi kufanikiwa kwa mawazo hayo

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
First priority ya Muislam ni Muislam mwenzake popote pale na ktk hali yoyote ile.

Muislam mkiwa ktk hatari wewe na Muislam mwenzake hata kama wewe upo karibu yake na ni rahisi zaidi kwa wewe kuokolewa itambidi kwanza aende kwa yule hata kama nafasi ya yeye kuokolewa ni ndogo ajaribu akishindwa ndiyo akurudie.

Upendo wanaousema ni baina yao wao kwa wao usiyekuwa muislam silimu kwanza ndo na wewe wakujali.
 
kwani tabora wapo waisilamu peke yake?taja mkoa wilaya au kijiji wakirisito au kanisa walipo jenga shule maji hosipitali barabala kisha watu wakawa wananufaika ukiweza taja vijiji waakoishi wakirito tu
NI jukumu lako wewe sio mimi
 
Maendeleo ni muhimu katika jamii za Kiislamu.
Uislamu na mendeleo ndiko kutakidhi mahitaji ya kimsingi ya watu.

Kiwango cha maendeleo duni katika maeneo ya Wailslamu hapa nchini kinaonyeshwa kwa kutumia mifano iliyo hai. Maeneo mengi ya Waislamu kuna tatizo kubwa la kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu. Hili linawafanya wasio waislamu kuulaumu Uislamu kuwa ni miongoni mwa sababu za kukosekana kwa maendeleo katika maeneo husika.

Inajadiliwa, sio kwamba uislamu hauna mbinu wala elimu za kiuchumi laa, ispokuwa waislamu wenyewe wameacha kufuata misingi iliyoasisiwa na Mtume wetu Muhammada (s.a.w). Kwamba uislamu daima umekuza shughuli za kiuchumi, na biashara na kipindi cha nyuma uislamu ulikuwa unachukuliwa kuwa njia bora ya kupata riziki ya mtu. Zaidi ya hayo, dhana ya maendeleo katika Uislamu ni mchakato muhimu, ambao unaboresha ustawi wa binadamu katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na akhera. Vielelezo vya MAKKA na MADINA vinawasilishwa kama mojawapo ya njia za maendeleo katika Uislamu wetu.

Waislamu kutoka mtaa mmoja wanakutana mara 5 kwa siku (sala tano), waislamu wa kitongoji kimoja wanakutana mara 1 kwa wiki (Sala ya Ijumaa), waislamu wa mkoa mmoja wanakutana mara mbili kwa mwaka (Sala za Eid), waislamu kote duniani tena walio matajiri wanakutana mara moja kwa mwaka (Hija).

Mlolongo huo alituachia Mwenyezi Mungu s.w kupitia Mtume wetu Muhammada (s.a.w), Lakini kukutana kwetu huko hakutakua na manufaa yoyote ikiwa bado kutakuwa na ukosefu wa maendeleo kwa watu wetu.

Lengo la watu kukutana sio kuswali na kuondoka tu, watu wanatakiwa kujadili, kufahamiana, na kupanga mikakati ya kusonga mbele zaidi kielimu, kiuchumi, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla. Nasio kuishia kuswali na kuondoka hata bila kupeana mikono.

Wenzetu wamechukua mfumo huo wa kukutana, leo utaona kuna jumuiya nyingi za Kikristo zinakutana kila wiki asubuhi mapema, leo utaona kuna umoja wa kimataifa (mataifa yote yanakutana) asili yake hii ni Uislamu. Lengo la kukutana misikitini ni kufanya vikao vya kheri kwa umoja wenu msonge mbele kimaendeleo.

Ifake wakati sasa misikiti iyanze kuhudumia watu na kuwafanyia watu mambo yaliyo mema, nasio watu siku zote kuihudumia misikiti. Moyo wa mtu umeumbwa kukipenda na kukithamini kile kitu kinachomjali, na moyo umeumbwa kukichukia na kukidharau kile kitu kisichomjali.

Misikiti mingi haina hata orodha (Record Keeping Books) ya kuwatambua waumini wake, idadi yao na shughuli zao. Misikiti mingi haina vipaombele katika swala la maendeleo, misikiti mingi haina orodha ya wajane, haina orodha ya mayatima, haina orodha ya wanafunzi walio kwama Masomo kwa ukata wa pesa, haina orodha ya wagonjwa, imekuwa ni sehemu ya kuswalia tu na kuondoka.
Msikiti ni kituo cha Kiislamu kinachotakiwa kuzalisha usasa wa kijamii na kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Dini ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu unaofuata sheria za MUNGU. Panapokuwa na dhiki inaashiria kwamba malengo ya Uislamu hayawezi kutimizwa, kwasababu watu hawajiwezi kwa kutofautiana kijamii na kiuchumi, rushwa na ukosefu wa haki. Haina faida kujenga msikiti ilihali wake za Masheikh wanazalishwa na Madaktari wa kiume, haina faida ya kujenga msikiti ilihali kuna kundi kubwa la vijana wa kiislamu wanakwama masomo kwa ukata wa pesa, haina faida ya kujenga msikiti ilihali wanawake wa kiislamu wanadhalilishwa kwenye mikopo ya Riba. Na mambo mengine ya kuudhi yanayoofanyika dhidi ya watu wetu.

Tusisahau kwamba ni kanuni na maadili ya Kiislamu ambayo yalisaidia jamii za Kiislamu kujenga ustaarabu wenye mafanikio makubwa na mafanikio yaliyoonyeshwa katika kukusanya rasilimali na kuunda fursa, na ambayo ilizisaidia jamii kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi hadi karne ya kumi na tisa.

Turudi katika misingi na kanuni zetu. Muislamu kupewa msaada na Kanisa inatia aibu ilihali misikiti ipo.

frauenindermoschee.jpg



BAKIIF ISLAMIC
Kimara, Dar es salaam
Usije kwa kujifanya uko upande fulani then kumbe tunakuja fikra hata avatar yako iko against.

Tambua hakuna chuo cha dini sio UDSM, SUA, UDOM ,ARDHI ivyo vya st. Sijui ni takataka wala sio vya maana
Mkuu una matatizo siyo Bure. CUHAS, SAUT, st JOHN, KCMC etc
 
Mada nzuri sana,mikoa au maeneo yenye waislam wengi kuna hali duni za maisha hali iyo maranyingi huwa inazaa vibaka,singeli,vigodoro na wazazi kupuuzia malezi na elimu kwa watoto wao.
Ukweli mtupu,shida iko kwa viongozi waliopshika mpini elimu ziro na kijana anapoenda kusoma akarejea kujaribu kuleta mageuzi hapo ataonekana adui,
Unaweza kuingia msikiti wenye miaka Mia hata hao waumini wanaofanya ibada humo zaidi ya miaka 20 hawajui kitu,
 
Msikiti ndio kituo Cha uislam,ndio msingi wa kuhuisha uislam
Tatizo ni kuwa uislam halisi umeachwa, pasipo kusimamisha utawala wa kiislam hayo uongeayo ni ndoto
Simamisha uislam msikiti isimame
Illogical!!!

Umeambiwa pamoja na dini kuwepo mzingatie pia masuala ya msingi ya jamii zenu (wewe ukiwepo) ila nashangaa unakata kata viuno hapa eti simamisha utawala wa kiislamu kwamba muingie vitani nchi isilimishwe ili wote tuendelee kuwa wajinga siyo?
 
Misikiti inatakiwa kuimarishwa na hii ndio amri ya allah, ufafanuzi wa kuimarisha upo na je makusudio ya maendeleo ya waumini unakusudia maendeleo gani? na maendeleo yao yanahusiana nini na kujenga misikiti?.

BAKIIF Islamic
 
Kuna dhambi gani Kwa mtoto wako kwenda kusoma kwenye shule bora?

Sidhani kama unajuwa hata huo uislamu na Quran, Mwislamu unatakiwa na Quran uitafute elimu hata China siyo shule za masister tu.

Halafu sidhani kama unafahamu kwenye Quran Maria/Mariam ana sura nzima inaitwa Surat Mariam, je unalifahamu hilo?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mambo yanayowangusha waislam kwenye maendeleo ya kaya zao ni:
1 polygamy: ni ngumu kiendelea kama huna mahusiano stable ya familia hii onazaa la watoto ambao hawana misingi imara ya kifamilia kwa hiyo kukosa uelekeo sahihii.pia resources nyingi hutumika kwenye recurrent expenditure za kuwa na kuhudumja wake

2. Msisistizo mdogo kwenye secular education.
3.kuamini sana kwenye ushirikiana
Uislam haumini kwenye shirk,dhambi ya kwanza kubwaa ni shirk ,shirk inamtoa straight Muslim kwenye dini,hakuna jinni mzuri Wala Nini majini wote wabaya,muislam anaeamini shirk huyo ni kafiri,ramli haramu,uchawi haramu kuabdu majini haramu
,"Sikuwaumba majini na watu isipokua mniabudu Mimi"
 
Nchi nzima haina maendeleo
Tuko nyuma na katika nchi masikini tuko mwisho mwisho kabisa

Wanaopokea misaada wanakula peke yao wakati ni misaada ya wote

Wanaokusanya sadaka wanajineemesha peke yao na wakitoa huduma ni mwendo wa kulipisha masikini maana hata maji mnauziwa masikini

Umasikini umetamalaki kwa sababu serikali ni masikini na viongozi hawana mbinu zozote bali ni wizi na kejeli kutwa

Misikiti inasaidia kwa watu kuswali ila pia watu wajitambue kwani Kazi ni IBADA pia
 
Uliyoyazungumza yana mashiko ila mtu mwenye mtazamo hasi hataichukulia hii katika uchanya wake, mtoa mada kazungumzia mengi ikiwemo suala la jumuiya na kukutana ili kuweza kusaidiana masuala mbalimbali, hiki ni kitu chema cha kuiga kwa hao ambao wamefanikiwa.

Suala la kiuchumi haliepukiki, ni muhimu kuwekeza ili muwe na miradi ya maendeleo itakayowanufaisha mfano ni Bakwata Bukoba wanajenga jengo la bilioni 5.2 ambalo litawezesha kuingiza mapato ambayo yatawasaidia katika shughuli zake. Sasa na hii ikienda katika maeneo mengine kama shule,zahanati, na huduma jamii mutaweza kuwagusa waumini wenu na pia kuisaidia jamii kwa ujumla
 
Back
Top Bottom