Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Nakuambia mfumo wa uchumi wetu hatuufuati ndo maana izo pesa zinatoka wapi za kujenga .


Ivyo vyuo watu wanasoma bure au wanapewa huduma bure.
Unalalamika sana mkuu instead utafute suluhisho,mleta mada hayo yote ameshayazungumza pale juu sasa ni wewe kama kijana msomi wa kiislamu uichukue hii ili uipeleke msikiti unaoswalia iwe ni kila siku au ijumaa mpe imamu awasomee waumini ili nao waone kama itawafaa waifanyie kazi.

Watu watasomaje bure lectures,huduma za maji na umeme vitalipwaje,majengo yatafanyiwa ukarabati vipi?muhimu kwanza hivyo vitu viwepo vitajihudumia kwa ada za watahiniwa wakristo na wapagani wakiwepo tatizo lako wewe na dini yako ni umimi unataka tena hivyo vyuo wasisome wasiokuwa waislam kwamba watavitia unajisi hali ya kuwa watawaingizia hela.

Mna safari ndefu,ndefu mnoo ndugu zangu.
 
Jamaa kwa misikiti wana bidii kiukweli. Kitaani kwetu misikiti ipo minne. Ya maskini waafrika upo wanapaita Kibrateni, waarabu nao wanao wa kwao mzuri kuliko Kibrateni. Afu kuna wa wapemba wanavaa suruali "njiwa" nao wameujenga siku sio nyingi. Walinunua nyumba mbili kibabe wakazivunja kujenga msikiti.
Pembeni ya msikiti kulikuwa bar wakanunua nyumba kibabe wakavunja wakajenga madrasa humo watoto wanajifungia na wengine hatujuagi wanapotoka waanaishi hapo hapo na Mwalimu wao. Kuna fimbo balaa hapo madrasa, watoto wanakula bakora hataree.
Wajenge ila waache ubaguzi kwenye misikiti. Maskini waafrika wanasali Kibra, Matajiri wanasali "Msikiti wa waarabu" wale wenye imani kali wana msikiti wao.

Hii dini imekuja kuharibu dunia,china wamewashitukia wamewapiga ban.
 
nyiyi wakirito mmeleta maendeleo gani? kupitia makanisa yenu? mbona wakirisito wengi wako vijijini wanajikuna vimbi iawatoka kwa uhafu,maedeleo yenu ni wizi tu na ufisadi serikalini kwa taharifa yako hapa nilipo nisehemu wanako ishi wakirisito asilimia 98 nyasa kawa danganye washenzi wenzenu huko
Maskini wee,....hata ku-type tu tena kwa kutumia maandishi ambayo tayari yashawekwa huwezi sasa sijui utakuwa na elimu gani,kama siyo la tatu B sijui!

Ila nilichogundua wewe mada imekuingia kisawasawa bahati mbaya kuielewa ndo hutaki.
 
Nakuambia mfumo wa uchumi wetu hatuufuati ndo maana izo pesa zinatoka wapi za kujenga .


Ivyo vyuo watu wanasoma bure au wanapewa huduma bure.
Kujenga hospitali kunahitaji mfumo wa uchumi?

Hamuwezi kuchangishana hela kila muumini mkajenga hospitali?

Kama hizi ndio akili za waislam, basi Hii dini ina Wajinga wengi sana.
 
wakirisito hosipitali yao inayo wasaidia wakina mama ni hipi na chuo?ujui kuwa hizo shule viuo na hasiptali serikali inawapa ruzuku(kodi yako) tatizo waisilamu walio wengi jf hawa jitambui uzi huu kauanzisha mkirisito hili watutukane heti nao wanachangia hovio
Wewe JF's member unayejiita 25000q nakushauri kwanza kama kata uliyopo kuna uwezekano wa kupata darasa la watu wazima rudi kajipige msasa ujue angalao kuandika vizuri ndo urudi hapa.

Hisia zangu zinaniambia kama wewe siyo wa Ikwiriri basi utakuwa wa Nanjilinji.
 
wewe usikodoe macho wewe kama wewe umeleta maedeleo gani kijijini kwenu hata kwa wazazi wako ndugu zako kazi kusifia mali za watu
Wewe ni mjinga eh! Sasa kwa taarifa yako wazazi wangu hawahitaji msaada wowote wa kutoka kwangu wapo vizuri kabla hata mimi sijazaliwa..kwahiyo hapa tunaongelea mali za watu binafsi!? We mpuuzi nini...ndio shida ya kutokunywa chai hii
 
uzuli wake nini? kusifia mali za kanisa ambazo hazina tija hata kwa wakiristo,na kuwa wabeza waisilamu kuwa awana maendeleo mada hii uzuli wake ni upi haswa ulio uona wewe?
Tukisema tuwekeze kwenye sekta nyingine za maendeleo tuachane na misikiti mingi katika eneo moja tunamaanisha hivi..Imagine mtu hajui hata kuandika hajui wapi kwa kuweka r na wapi kwa kuweka L halafu anakaza fuvu kwelikweli

Huyu jamaa anawakilisha wapumbavu wengi wanaohitaji ukombozi wa kifikra
 
Lengo la uislam ninkuabudu tu hizo biashara wafanye wengine Kama wamejenga na hawatuzuii kupata huduma tatizo liko wapi dunian tupo kwa ajili ya ibada na muda ni mfupi Sana hivyo Sion haja ya kukompilicate kiivo
 
Maendeleo ni muhimu katika jamii za Kiislamu.
Uislamu na maendeleo ndiko kutakidhi mahitaji ya kimsingi ya watu.

Kiwango cha maendeleo duni katika maeneo ya Wailslamu hapa nchini kinaonyeshwa kwa kutumia mifano iliyo hai. Maeneo mengi ya Waislamu kuna tatizo kubwa la kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu. Hili linawafanya wasio waislamu kuulaumu Uislamu kuwa ni miongoni mwa sababu za kukosekana kwa maendeleo katika maeneo husika.

Inajadiliwa, sio kwamba uislamu hauna mbinu wala elimu za kiuchumi laa, ispokuwa waislamu wenyewe wameacha kufuata misingi iliyoasisiwa na Mtume wetu Muhammada (s.a.w). Kwamba uislamu daima umekuza shughuli za kiuchumi, na biashara na kipindi cha nyuma uislamu ulikuwa unachukuliwa kuwa njia bora ya kupata riziki ya mtu. Zaidi ya hayo, dhana ya maendeleo katika Uislamu ni mchakato muhimu, ambao unaboresha ustawi wa binadamu katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na akhera. Vielelezo vya MAKKA na MADINA vinawasilishwa kama mojawapo ya njia za maendeleo katika Uislamu wetu.

Waislamu kutoka mtaa mmoja wanakutana mara 5 kwa siku (sala tano), waislamu wa kitongoji kimoja wanakutana mara 1 kwa wiki (Sala ya Ijumaa), waislamu wa mkoa mmoja wanakutana mara mbili kwa mwaka (Sala za Eid), waislamu kote duniani tena walio matajiri wanakutana mara moja kwa mwaka (Hija).

Mlolongo huo alituachia Mwenyezi Mungu s.w kupitia Mtume wetu Muhammada (s.a.w), Lakini kukutana kwetu huko hakutakua na manufaa yoyote ikiwa bado kutakuwa na ukosefu wa maendeleo kwa watu wetu.

Lengo la watu kukutana sio kuswali na kuondoka tu, watu wanatakiwa kujadili, kufahamiana, na kupanga mikakati ya kusonga mbele zaidi kielimu, kiuchumi, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla. Nasio kuishia kuswali na kuondoka hata bila kupeana mikono.

Wenzetu wamechukua mfumo huo wa kukutana, leo utaona kuna jumuiya nyingi za Kikristo zinakutana kila wiki asubuhi mapema, leo utaona kuna umoja wa kimataifa (mataifa yote yanakutana) asili yake hii ni Uislamu. Lengo la kukutana misikitini ni kufanya vikao vya kheri kwa umoja wenu msonge mbele kimaendeleo.

Ifake wakati sasa misikiti iyanze kuhudumia watu na kuwafanyia watu mambo yaliyo mema, nasio watu siku zote kuihudumia misikiti. Moyo wa mtu umeumbwa kukipenda na kukithamini kile kitu kinachomjali, na moyo umeumbwa kukichukia na kukidharau kile kitu kisichomjali.

Misikiti mingi haina hata orodha (Record Keeping Books) ya kuwatambua waumini wake, idadi yao na shughuli zao. Misikiti mingi haina vipaombele katika swala la maendeleo, misikiti mingi haina orodha ya wajane, haina orodha ya mayatima, haina orodha ya wanafunzi walio kwama Masomo kwa ukata wa pesa, haina orodha ya wagonjwa, imekuwa ni sehemu ya kuswalia tu na kuondoka.
Msikiti ni kituo cha Kiislamu kinachotakiwa kuzalisha usasa wa kijamii na kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Dini ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu unaofuata sheria za MUNGU. Panapokuwa na dhiki inaashiria kwamba malengo ya Uislamu hayawezi kutimizwa, kwasababu watu hawajiwezi kwa kutofautiana kijamii na kiuchumi, rushwa na ukosefu wa haki. Haina faida kujenga msikiti ilihali wake za Masheikh wanazalishwa na Madaktari wa kiume, haina faida ya kujenga msikiti ilihali kuna kundi kubwa la vijana wa kiislamu wanakwama masomo kwa ukata wa pesa, haina faida ya kujenga msikiti ilihali wanawake wa kiislamu wanadhalilishwa kwenye mikopo ya Riba. Na mambo mengine ya kuudhi yanayoofanyika dhidi ya watu wetu.

Tusisahau kwamba ni kanuni na maadili ya Kiislamu ambayo yalisaidia jamii za Kiislamu kujenga ustaarabu wenye mafanikio makubwa na mafanikio yaliyoonyeshwa katika kukusanya rasilimali na kuunda fursa, na ambayo ilizisaidia jamii kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi hadi karne ya kumi na tisa.

Turudi katika misingi na kanuni zetu. Muislamu kupewa msaada na Kanisa inatia aibu ilihali misikiti ipo.

frauenindermoschee.jpg



BAKIIF ISLAMIC
Kimara, Dar es salaam
[emoji120]
 
wisilamu afadhiri wake ni muisilam nenda wewe kajenge shule hositali kisha waisilam watibiwe bule kama unavio taka kazi kulaumu tu hata huko msikitini kwanza upajui
Yani bro unavyo-type kiboya boya unazidi kudhihirisha uwezo wako wa ku-reason hata mambo ya msingi.

Tusizungumzie waislam tu tuzungumze kwanini wagonjwa watibiwe bure?yeyote yule hata mimi Mkatoliki sitegemei kutibiwa bure au mwanangu kusoma bure kwenye hospital au shule iliyojengwa kwa mchango wangu(kwanza nitakuwa mwendawazimu nikiwaza hivyo),mule kuna wanaowezesha mimi nipate huduma bora hawa watakuwaje na moyo wa kufanya kazi yao ya kitabibu kama hawakulipwa vizuri?dawa zitanunuliwa vipi?bills mbalimbali zitalipwaje ikiwa mgonjwa hakuchangia matibabu yake?

Wakaibe ili hayo yote yafanyike?hiyo serikali yako inayokusanya kodi zooote na ina mpaka access ya kukopa ilipe baadae haijafanya hivyo leo likafanye Kanisa?em ongea kama mtu mzima bwana.
 
Utapeli eti akasome mbona yamefungwa wengi walikuwa vilaza ,wanatumia ujinga wa waumini kuwadanganya ila kichwani zero
Dah pole Sana 😂🤣🤣 Leo umekula za uso , najua apo ulipo unaweweseka

Ila waislamu mjenge hospital, shule na vyuo

Jifunzeni pia kutoa sadaka nene
Umekaa wiki unafanya kazi inafika ijumaa unaenda kutoa jero
 
Nafikiri history huijui ndio maana umekwenda ku generalised Waislam kwa ujumla na kulaumu sn lakini umeshindwa kutaambua JUMUIA yoyote ina simamiwa na TAASISI iliye kuwa IMARA sasa jiulize wewe kama wewe BAKWATA ni institution ya namna gani Ukipta jibu basi inatosha kuelewa mfumo uliopo.

Nenda vikindi na sehemu nyingi za DAR ES SALAAM kaone RC walivyo kuwa na maeneo makubwa hasa wamepewa au kununua kwa hela kidogo na wizira na wala sio kosa kwao kuwa na maeneo mengi sababu wanatumia opportunities wanayo pata kama taasisi sasa waulize BAKWATA wana nini ? Hawana maeneo yoyote mapya zaidi ya yale ya zamani na mengi wameuza.

Sent from my SM-S901B using JamiiForums mobile app
Tengua kauli hapo juu kwenye bold unaamsha taharuki bila sababu.

Hawakupendelewa na wizara sema wamewahi kukiwa bado gizani,Vikindu mpaka leo bado vipo viwanja vya 1.5mill 50×50 assume kama RC walinunua eneo sehemu pana viwanja vya bei hiyo leo early 2000 unadhani miaka ile heka ilikuwa bei gani?

Ni watu wamebarikiwa kutumia upeo wao vizuri japo najua wengi hawapendi kusoma nilichoandika hapa.
 
Hapa IKWIRIRI unamkuta Mzee ana SIGDA Ila anaomba-omba tu mtaan na KANZU+KOBAZi


Mwenyezi Mungu tunakuomba msaidie kila anayekuamini abarikiwe kwa pesa na Mali kama baba yetu Ibrahimu

Ukimjua Mungu na kuheshimu sheria zake halafu ukawa huna kiti unadharaulika sana haswa na wale wanaoabudu mashwetani
 
Dah pole Sana 😂🤣🤣 Leo umekula za uso , najua apo ulipo unaweweseka

Ila waislamu mjenge hospital, shule na vyuo

Jifunzeni pia kutoa sadaka nene
Umekaa wiki unafanya kazi inafika ijumaa unaenda kutoa jero
😂😂 Wee unatoka wakati wanao wanasoma shule za kata sio st.francis ..Imekusaidia nn?
 
hiyo michango hao watoaji inawdaidia nn?
Wewe uliye nje huwezi kuona lakini kama siyo hiyo michango aliyeandika hii mada hapa ange-compare uislam na serikali lakini kwa sababu ameona huko kuna tofauti na uislam ndiyo maana tupo hapa tunapeana elimu.

Well,japokuwa wewe elimu haikuingii.
 
Ndio mali ni za kanisa,na wala si zangu wala mchungaji.

Kama kuna mchungaji alikupanga ana hisa kwenye mradi wa kanisa,alikuwa anataka akupate tu kisha asepe.
mali ya haina msaada kwa wakiristo wala watu baki wapia dili tu hao
 
Back
Top Bottom