Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Tupunguze kujenga Misikiti, hakuna Uislamu kama hakuna maendeleo ya waumini

Dah pole Sana 😂🤣🤣 Leo umekula za uso , najua apo ulipo unaweweseka

Ila waislamu mjenge hospital, shule na vyuo

Jifunzeni pia kutoa sadaka nene
Umekaa wiki unafanya kazi inafika ijumaa unaenda kutoa jero
Shule,vyuo na hospital zinazojengwa na serikali ni kwa ajili ya nani!!
 
Umeishia darasa la ngapi??
Rudi Kwanza darasani muda bado upo wa kuendelea kujifunza kuandika na kusoma
tatizo sio kurudi darasani kinacho takiwa ujumbe ukufikie wacha tabia za kike nenda kawambie wahusika hapa hawapo
 
Maendeleo ni muhimu katika jamii za Kiislamu.
Uislamu na maendeleo ndiko kutakidhi mahitaji ya kimsingi ya watu.

Kiwango cha maendeleo duni katika maeneo ya Wailslamu hapa nchini kinaonyeshwa kwa kutumia mifano iliyo hai. Maeneo mengi ya Waislamu kuna tatizo kubwa la kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu. Hili linawafanya wasio waislamu kuulaumu Uislamu kuwa ni miongoni mwa sababu za kukosekana kwa maendeleo katika maeneo husika.

Inajadiliwa, sio kwamba uislamu hauna mbinu wala elimu za kiuchumi laa, ispokuwa waislamu wenyewe wameacha kufuata misingi iliyoasisiwa na Mtume wetu Muhammada (s.a.w). Kwamba uislamu daima umekuza shughuli za kiuchumi, na biashara na kipindi cha nyuma uislamu ulikuwa unachukuliwa kuwa njia bora ya kupata riziki ya mtu. Zaidi ya hayo, dhana ya maendeleo katika Uislamu ni mchakato muhimu, ambao unaboresha ustawi wa binadamu katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na akhera. Vielelezo vya MAKKA na MADINA vinawasilishwa kama mojawapo ya njia za maendeleo katika Uislamu wetu.

Waislamu kutoka mtaa mmoja wanakutana mara 5 kwa siku (sala tano), waislamu wa kitongoji kimoja wanakutana mara 1 kwa wiki (Sala ya Ijumaa), waislamu wa mkoa mmoja wanakutana mara mbili kwa mwaka (Sala za Eid), waislamu kote duniani tena walio matajiri wanakutana mara moja kwa mwaka (Hija).

Mlolongo huo alituachia Mwenyezi Mungu s.w kupitia Mtume wetu Muhammada (s.a.w), Lakini kukutana kwetu huko hakutakua na manufaa yoyote ikiwa bado kutakuwa na ukosefu wa maendeleo kwa watu wetu.

Lengo la watu kukutana sio kuswali na kuondoka tu, watu wanatakiwa kujadili, kufahamiana, na kupanga mikakati ya kusonga mbele zaidi kielimu, kiuchumi, kiafya na kimaendeleo kwa ujumla. Nasio kuishia kuswali na kuondoka hata bila kupeana mikono.

Wenzetu wamechukua mfumo huo wa kukutana, leo utaona kuna jumuiya nyingi za Kikristo zinakutana kila wiki asubuhi mapema, leo utaona kuna umoja wa kimataifa (mataifa yote yanakutana) asili yake hii ni Uislamu. Lengo la kukutana misikitini ni kufanya vikao vya kheri kwa umoja wenu msonge mbele kimaendeleo.

Ifake wakati sasa misikiti iyanze kuhudumia watu na kuwafanyia watu mambo yaliyo mema, nasio watu siku zote kuihudumia misikiti. Moyo wa mtu umeumbwa kukipenda na kukithamini kile kitu kinachomjali, na moyo umeumbwa kukichukia na kukidharau kile kitu kisichomjali.

Misikiti mingi haina hata orodha (Record Keeping Books) ya kuwatambua waumini wake, idadi yao na shughuli zao. Misikiti mingi haina vipaombele katika swala la maendeleo, misikiti mingi haina orodha ya wajane, haina orodha ya mayatima, haina orodha ya wanafunzi walio kwama Masomo kwa ukata wa pesa, haina orodha ya wagonjwa, imekuwa ni sehemu ya kuswalia tu na kuondoka.
Msikiti ni kituo cha Kiislamu kinachotakiwa kuzalisha usasa wa kijamii na kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Dini ni mfumo wa maisha ya mwanaadamu unaofuata sheria za MUNGU. Panapokuwa na dhiki inaashiria kwamba malengo ya Uislamu hayawezi kutimizwa, kwasababu watu hawajiwezi kwa kutofautiana kijamii na kiuchumi, rushwa na ukosefu wa haki. Haina faida kujenga msikiti ilihali wake za Masheikh wanazalishwa na Madaktari wa kiume, haina faida ya kujenga msikiti ilihali kuna kundi kubwa la vijana wa kiislamu wanakwama masomo kwa ukata wa pesa, haina faida ya kujenga msikiti ilihali wanawake wa kiislamu wanadhalilishwa kwenye mikopo ya Riba. Na mambo mengine ya kuudhi yanayoofanyika dhidi ya watu wetu.

Tusisahau kwamba ni kanuni na maadili ya Kiislamu ambayo yalisaidia jamii za Kiislamu kujenga ustaarabu wenye mafanikio makubwa na mafanikio yaliyoonyeshwa katika kukusanya rasilimali na kuunda fursa, na ambayo ilizisaidia jamii kufikia maendeleo makubwa ya kiuchumi hadi karne ya kumi na tisa.

Turudi katika misingi na kanuni zetu. Muislamu kupewa msaada na Kanisa inatia aibu ilihali misikiti ipo.

frauenindermoschee.jpg



BAKIIF ISLAMIC
Kimara, Dar es salaam
Mtuwache tupumue, ondoeni majeshi yenu ya Uvamizi huku Zanzibar kwanza.
 
Kagame hajafuta makanisa,kaweka utaratibu kila mchungaji akasome elimu ya dini theology.

na makanisa sio utapeli,we wenyewe elimu upepewa na shule za kanisa,ebu kaa utulie.
kawadanganye mbulula wenzio mbona utapeli wao uko wazi tu kwa mwenye macho labda ww kipofu
 
Unalalamika sana mkuu instead utafute suluhisho,mleta mada hayo yote ameshayazungumza pale juu sasa ni wewe kama kijana msomi wa kiislamu uichukue hii ili uipeleke msikiti unaoswalia iwe ni kila siku au ijumaa mpe imamu awasomee waumini ili nao waone kama itawafaa waifanyie kazi.

Watu watasomaje bure lectures,huduma za maji na umeme vitalipwaje,majengo yatafanyiwa ukarabati vipi?muhimu kwanza hivyo vitu viwepo vitajihudumia kwa ada za watahiniwa wakristo na wapagani wakiwepo tatizo lako wewe na dini yako ni umimi unataka tena hivyo vyuo wasisome wasiokuwa waislam kwamba watavitia unajisi hali ya kuwa watawaingizia hela.

Mna safari ndefu,ndefu mnoo ndugu zangu.
wewe hivio vio vina msaada gani sasa kama luzuku inatoka serikalini kazi wizi tu
 
😂😂 Wee unatoka wakati wanao wanasoma shule za kata sio st.francis ..Imekusaidia nn?
Pole sana leo huta lala ni kuweweseka tu , umewekwa mtu kati
ila inakuwaje unapinga maendeleo? mimi watoto wangu wanasoma shule za kanisa tena bora kabisa

NImewapa ushauri pia toeni sadaka nene , wewe ungekuwa kipindi cha Muhammad ungempelekea Jero?
Koran 58:12. Enyi mlio amini! Mnapo sema siri na Muhammad, basi tangulizeni sadaka kabla ya kusemezana kwenu.....
 
Kujenga hospitali kunahitaji mfumo wa uchumi?

Hamuwezi kuchangishana hela kila muumini mkajenga hospitali?

Kama hizi ndio akili za waislam, basi Hii dini ina Wajinga wengi sana.
kwani nchi hii hosipitali hakuna? makanisa ndio yamejenga hositali nitajie faida unayo ipata wewe kama wewe waisilam wanayo ikosa wakiugua hawatibiwi? mtaacha lini kusifia mali za watu zisizo wanafaishi nyiyi wala ndugu zenu? huo nao ni upunguani
 
Ili uweze kumtawala binadamu mfundishe na umpe elimu itakayomjaza hofu (dini) angalia walokole na baadhi ya jamaa zetu wasabato yaani utafutaji kwao unajengwa na hofu ya dini na ndiyo maana hata Zanzibar misikiti inajegwa kwa wingi sana, so watu wanakuwa na muda mwingi kwenda kufanya ibada kuliko jambo lingine.

Na laiti Zanzibar kungekuwa na muingiliano mkubwa wa jamii nyengine basi mabadiriko yangepenya kwa ukubwa, maana mtu wa kuja haji kupoteza muda anakwenda na muda kuisaka shekeli.
 
Serekali ikijenga inaweka masharti ya serekali , kila kukicha waislamu wanalalama dini yao hairuhusu wanawake wahudumiwe na wanaume , unaonaje mngejenga muwe na masharti yenu
Serekali ndiyo nini!!?..shule,vyuo na hospitali za serikali waislam hawaruhusiwi!?
 
Wewe ni mjinga eh! Sasa kwa taarifa yako wazazi wangu hawahitaji msaada wowote wa kutoka kwangu wapo vizuri kabla hata mimi sijazaliwa..kwahiyo hapa tunaongelea mali za watu binafsi!? We mpuuzi nini...ndio shida ya kutokunywa chai hii
huna lolote wewe mvimba macho tu haya hao wanao kuzunguka umewasaidiaje? uko vizuli wakuwa vizuli atakuwa wewe wenye nazo hawasemi wasio kunazo kazi kujikweza tu
 
Tukisema tuwekeze kwenye sekta nyingine za maendeleo tuachane na misikiti mingi katika eneo moja tunamaanisha hivi..Imagine mtu hajui hata kuandika hajui wapi kwa kuweka r na wapi kwa kuweka L halafu anakaza fuvu kwelikweli

Huyu jamaa anawakilisha wapumbavu wengi wanaohitaji ukombozi wa kifikra
hacha ujinga wewe na kujiona bora hao wamejenga misikiti wewe kajenge shule na viwanda kwanza uanze na ndugu zako kisha wengine umekaza kuponda wanao jenga misikiti unakili wewe ? ndilo tatizo la kukosoa kusoa kulalama hovio wenzako wameza hilo nawe fanya jengini limbukeni wewe
 
Lengo la uislam ninkuabudu tu hizo biashara wafanye wengine Kama wamejenga na hawatuzuii kupata huduma tatizo liko wapi dunian tupo kwa ajili ya ibada na muda ni mfupi Sana hivyo Sion haja ya kukompilicate kiivo
hakika
 
Serekali ndiyo nini!!?..shule,vyuo na hospitali za serikali waislam hawaruhusiwi!?
Serikali Ina masharti yanayo kiuka Imani Yako , nimekwambia kila kukicha waislamu wanalala wanawake kuhudumiwa na wanaume , Kuna hospital za dini kila asubuhi waislamu wanasali na wakristo ibada ya kikristo
Na mashule vivyo hivyo

Mkiwa na zenu mtaweka utaratibu wenu
Kumbuka pia uwa mnajitapa Sana kwamba Uislam ni mfumo mzima wa maisha ,
 
Back
Top Bottom