Wajinga hawajuagi kuongoza nchi, zaidi ya kuendekeza anasa tu na kujinufaisha wao na syndicates zao huku majority ya watanzania wakiteseka wenye hali ya chini, sababu nchi inakuwaga ni ya wachache sana wenye nguvu ndio wanaifaidi maana huwa wanafanya chochote wanachojiskia yaani bila hofu ya kuchukuliwa hatua.
Nakumbuka Kitana alikuwa anadhulumu sana watu kwenye shughuli za uvuvi huko ziwa Victoria, wavuvi wengi sana wadogo wadogo wameumia kwa kunyang'anywa mitumbwi yao na kitana kisa tu walikuwa wanavua karibu na kisiwa chake...
Alipoingia chuma madarakani alipigwa biti moja tu ule uonevu wote ukaisha na kila mtu akawa anavua kwa uhuru bila hofu yoyote hata kwenye maeneo ambayo kitana alikuwa amaye monopoly kuwa anavua peke yake yake tu.
Sasa hivi unaambiwa ule uonevu umerudi kwa kasi, na hakuna tena mvuvi mdogo anayesogelea kwenye himaya yake, yaani jamaa amerudi tena kuogopwa kama awali...
Na hakuna hata anayejali sio waziri wala raisi kwamba kuna wavuvi wadogo wadogo wanaonewa huko visiwani.