Kuna siku nilikuwa napiga story na mzee mmoja wa Kinyamwezi mwenye umri wa miaka 85, aliniambia endapo kama Nyerere angetaka kuifanya familia yake iwe ni moja ya familia tajiri zaidi barani afrika kwa miaka mingi kama walivyofanya akina Eduardo Santos au Teodore Nguema, huo uwezo alikuwa nao.
Maana kama ni hongo alikutana nazo sana, waingereza walihaidi mpaka kumpa ulinzi kwa kipindi chake chote atakachotawala endapo kama angekubali kuwaachia rasilimali.
Imagine walikuwa wanamuita London asaini mikataba ya madini, ila yeye anawaambia subiri nikawaulize kwanza wanainchi wangu kama watakubali... kumbe ndio amewakataa hivyo, na kipindi hicho watanzania wengi bado ni mambumbu waliokuwa na elimu wachache sana... hivyo hata maamuzi mengi ya kiserikali aliyafanya mwenyewe, kwa hiyo hata angetaka kuuza migodi yote nchi hii na hela kuzifaidi yeye na familia yake kwa mwamvuli wa uwekezaji uwezo ulio alikuwa nao tena kirahisi sana.
Mimi huwa najiulizaga hivi Tanzania ingekuwa na kiongozi aina ya Samia au Kikwete au Mkapa kwa miake ile sijui ingekuwaje, sijui hata tungebakia na nini Leo..
Halafu eti unakutana na kitoto cha late 90s au 2000s kina tema shiiit na kumbeza Nyerere huku kikiwasifia hawa maraisi waliofuata ambao obviously ni madalali wa rasilimali kuwa eti ndio bora san.. huwa napatwa na hasira sana.