Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,683
- 2,158
Kazi kubwa ya kiongozi yeyeto yule ni kuhakikisha taasisi au watu anaowaongoza wanafikia malengo waliyojiwekea kwa asilimia zote. Kiaongozi asiye na uwezo wa kuweka malengo mahususi (specific objectives) na njia za kuyafikia (strategic plan) hana sifa za kuwa kiongozi bora.
Kiongozi bora pia ni lazima awe na uwezo wa kuona mbele zaidi ya wenzake (ability to foresee/ability to anticipate) na ajue vikwazo vinavyoweza kumkwamisha asifikie malengo ya taasisi yake au watu anawaoongoza. Hapa hatakiwi kuishia ku "anticipate" tu au ku predict vikwazo vinavyoweza kumkwamisha, la hasha! Anatakiwa ajue pia atatumia mbinu gani kuepuka vikwazo hivyo au kukabiliana navyo ili hatimaye ayafikie malengo yake.
Hapa Tanzania, kuna mambo makubwa na magumu yanaendelea tangu uchaguzi wa 2015 umalizike. Ukihesabu miaka, ni miaka ya mtoto aliyezaliwa wakati huo sasa hivi yuko darasa la "vidudu" na ana mdogo wake ambaye naye sasa hivi anajifunza kuongea.
Tangu 2015, dalili zilionyesha wazi wazi kwamba vyama vya upinzani havitakiwi tena kujitanua hapa nchini. Bahati nzuri ni kwamba haya yalisemwa hadharani na baadaye yakajidhihirisha kwa vitendo pale kwa kila kilichofanywa na wapinzani kilionekana ni usaliti na uhaini uliotakiwa kufunguliwa mashitaka mahakamani.
Sote ni mashahidi, kuanzia kiongozi wa chama hadi mwanachama wa kawaida alifunguliwa mashitaka kwa comment za facebook, whatsap au kutoa maoni yake. Tulishuhudia vyombo vya habari vilivyoanza taratibu kususa kufanya mahojiano na wanasiasa wa vyama pinzani na hadi sasa imeshazoeleka.
Kama haitoshi, hata mahakamani kuna watu wanahisi baadhi ya kesi ziliendeshwa kwa kuangalia nani mdai ni wa mlengo gani na mdaiwa anamlengo gani. Kina Lema walikaa mahabusu kwa makosa ambayo yalidhaminika, kina Sugu walihukumiwa hukumu zilizokuja kufutwa baadaye, kina Mbowe walikaa gerezani kwa makosa ya kukiuka dhamana kana kwamba wangetoroka nchini, kina Lisu wanakesi hadi leo hatujui idadi yake. Na mengine mengi sana.
Kama hiyo haitoshi viongozi wa bunge nao walikumbatiana hadharani na muhimili wa serikali kufanya yale waliyoyaweza ilimradi tu wabunge wa upinzani wasikae kwa amani mjengoni. Kama haitoshi kuna wakati ni kama walifanya mazungumzo ya njama! kwamba wewe watoe huko mimi ni dili nao huku!
Hivi kweli kwa hayo yote na mengine mengi ambayo wewe msomaji unayafahamu, Mbowe na watu wake walitegemea kutakuwa na fairness kwenye uchaguzi wowote ule watakaoshirikiana na CCM!?
Kweli kabisa tuseme yaliyotokea kwenye chaguzi za marudio ya wabunge na madiwani hasa waliounga juhudi hayakutosha kutoa somo na kugonga kengere ya hatari!?
Kwa hayo yote, mnataka tuamini kabisa strategic plan waliyojiwekea kina Mbowe na kina Zitto ni kususia uchaguzi tu!?
Mimi sitaki kuamini kwamba ubize wa kuhudhuria mahakamani uliwafanya washindwe kukaa chini na kujiwekea mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanajiimarisha.
Sitaki kuamini kwamba katika ulimwengu huu wa kutumia akili zaidi wamekubali kukaa na kutulia kusubiri CCM na serikali yake waamue kwa niaba yao halafu wao wafuate tu halafu wategemee ushindi
Kiongozi bora haishiwi mikakati ya kufikia mafanikio. Kiongozi bora hakubali taasisi yake ishindwe kufikia malengo. Kiongozi bora hasubiri mambo yaharibike ndo abuni mbinu mbadala. Kiongozi bora hawaachi watu wake wakiwa hawajui wafanyeje. Kiongozi bora huongoza watu wake kufikia malengo. Kiongozi bora ni yule ambaye anajua njia yenye miiba atavukaje yeye na watu wake. Kiongozi bora haishii kusema hili sifanyi tu, akishasema hivyo lazima aseme anafanya lipi
Hii ni changamoto kwa vyama vyote vya upinzani. Wana malengo madhubuti? (Specific objectives?). Wana mikakati madhubuti ya kufikia hayo malengo!? Je, malengo yao yanapimika? (measurable), yanaonekana? (obsevable?), yana muda mahususi ya kuyafikia? (Time bound?)
Mmeona jinsi CCM na baadhi ya viongozi wa serikali walivyo na mbinu nyingi! Halali na haramu! Je, wanasiasa wa upinzani mlijiandaa kukabiliana na mbinu zote hizo za halali na haramu?
Kama kweli wataishia kususia uchaguzi huu harafu wasije na suruhisho madhubuti litakaloungwa mkono na kila mpenda amani, ni dhahiri kuna mahali katika mfumo wa siasa za upinzani patakuwa pamelegea na patahitajika kurekebishwa ili mshindani wao naye asiwe anajiamulia atakavyo. Kwenye ushindani lazima uwe na uwezo wa "kumtisha" mshindani wako ili akuheshimu asifanye atakavyo! Angalieni majigambo ya wale mabondia kabla ya kuanza pambano! Hivi unadhani zile mbwembwe hazina maana kweli!?
Ngoja nifuate korosho kwa Mangi niendelee kusindikiza wekeend labda kutatokea "kituko" kingine cha uchaguzi baada ya hiki cha kulazimisha waliojiondoa wote kurudi na kushiriki kwa lazima!