Tuseme ukweli, kuna mahali viongozi wa vyama vya upinzani "wanalegeza kamba"

Tuseme ukweli, kuna mahali viongozi wa vyama vya upinzani "wanalegeza kamba"

Wewe unamapendekezo gani?
1.....

2......

3......

Wanapita hapa wanasoma watakusikia.
Kiongozi bora na imara lazima awe na mikakati madhubuti iliyopangwa kumvusha yeye na watu wake! Mapendekezo unayotaka hapa ni nyongeza tu na si lazima ayafanyie kazi

Sina hakika kama taasisi imara kama vyama vya upinzani bado vinataka kupata mikakati madhubuti kwa njia hii kama unayataka mdau afanye
 
Kiongozi bora na imara lazima awe na mikakati madhubuti iliyopangwa kumvusha yeye na watu wake! Mapendekezo unayotaka hapa ni nyongeza tu na si lazima ayafanyie kazi

Sina hakika kama taasisi imara kama vyama vya upinzani bado vinataka kupata mikakati madhubuti kwa njia hii kama unayataka mdau afanye

Wewe unataka nini kitendeke? Mathalani

Hili swali limetokakana na wewe binafsi kutokubaliana na changamoto nilizokuorodheshea.

Yumkini unamapendekezo bora kukabiri changamoto zilizopo

1. Kupotezwa

2. Kuuwawa

3. Kupigwa risasi

4. Kubambikiwa kesi

5. Marufuku siasa majukwaani/mikusanyiko

6. Bungeni unatimuliwa uki- present strategic plans

7. Ukipelekwa mahakamani unahukumiwa bila kuzingatia matakwa ya sheria

Nknk

Katika mazingira haya wewe unasuluhisho lolote bora iili litumike.
 
Kwa akili yako unadhani nguvu ya umma ni machafuko tu. Kunaweza kusiwe na machafuko na watu wakaisusia serikali, ikiwemo kutokutoa ushirikiano kwa viongozi walioko madarakani, wakiitisha mikutano hamtokei, kukiwa na jambo la kijamii kama kifo au sherehe hamuendi. Hiyo ni nguvu ya umma tosha bila vurugu.
Mkuu unachokisema kina ukweli lakini hakuna mdanganyika mwenye UTHUBUTU wa kufanya hivyo, viongozi wanatujua vizuri sana sisi wananchi kuliko sisi(wananchi)tunavyowajua wao, ndiyo maana kiongozi anaweza kuipeleka nchi atakavyo na sio wananchi kumpeleka kiongozi watakavyo.
sioni wa kuitoa CCM hapo ilipo labda iki kizazi kiishe kije kizazi kingine, ambacho kina UTHUBUTU.
 
adolay,

Hakuna mtu atakayekataa kukubaliana na changamoto hizo ulizoorodhesha. Hizo zipo wazi hata mtoto mdogo anazijua.

Kusema nije na suruhisho uko sawa kabisa lakini tufanye hiyo iwe topic ya siku nyingine.

Swala langu kuu kwenye mada hii ni kwa viongozi wa siasa za upinzani.

Wao kama viongozi wenye kundi kubwa wanamikakati gani madhubuti ya kushughulika na hizo changamoto ulizoorodhesha?

Inatosha tu kususia chaguzi?

Baada ya kususia wana uhakika kwamba hizo changamoto ulizotaja zitakuwa zimeisha?

Ndiomaana nikasema kiongozi lazima aje na suruhisho madhubuti la kukomesha kitu kinachoonekana kuwa kikwazo kwa taasisi au watu anaowaoongoza.

Hapa kwetu vikwazo viko wazi, vinasemwa hadharani, vinaonyeshwa hadharani, na vinatendeka mchana kweupe!

Wamejipangaje kumaliza vikwazo hivyo? Hii ndo hoja yangu ya msingi wala sio Mimi kuja na nini kifanyike maana naamini uimara wa Taasisi hujengwa na mfumo imara wenye mikakati madhubuti.

Ili kuyafikia mafanikio ni lazima kuwa na ramani (road map) inayokuelekeza unayafikiaje hayo mafanikio.
 
Upinzani please.

Msikubali uchaguzi uendelee.

Wekeni masharti ya kubatilisha machafu yote mliyotendewa.

Mfano katiba mpya, siasa huru kwa watu wote, uhuru wa vyombo vya habari, tume huru, kufutwa kwa sheria za kifashisti nk.
Muda ndio huu ccm washaanza kupoteana kwa wazee kuwalaumu vijana washamba kwa kuipelekesha ccm kishambashamba,wapinzani watumie mwanya huu kuwapa masharti haya ccm Kama hawataki basi washikilie palepale kwa kutoshiriki.
Nalog off
 
Tunapoelekea wanasiasa wa upinzani watakosa imani kwa wananchi
 
Back
Top Bottom