tindo,
Humtendei haki kusema mleta mada hakutoa mapendekezo wafanye nini, hata kama hukuona mifano iliyo dhahiri kama uliyotoa wewe. Viongozi wenye sifa alizozitaja katika andiko lake hawahitaji kulishwa, tayari wao wanajua kula bila ya msaada uliowazi kama unavyopendekeza wewe.
Hata hivyo, mapendekezo uliyotoa wewe ni kama umeshuka leo kutoka sayari mpya.
Mbowe nusura ale shaba pale Kinondoni, na polisi wanachekesha watu mahakamani wakisimlia jinsi Mheshimiwa alivyotimua mbio aliposikia milio ya bunduki.
Leo hii unapendekeza aitishe maandamano, ataandamana na nani? Tena maandamano ya kila wiki? Ndio maana nasema ni kama hujawahi kuishi hapa kwa kutoa pendekezo la namna hiyo.
Mbowe amekwishatambua, mapendekezo kama hayo akiyafuata imekula kwake! Si Tundu Lissu yule pale, hata kuvaa tu fulana za kumuombea apone watu hawawezi, sembuse kuandamana kila wiki? Hawa watu unaowazungumzia wametoka wapi ghafla mara moja hivi!
Ninakubaliana nawe, pasiwe na uchaguzi bila kuwepo "Tume Huru"; bila hivyo hakuna uchaguzi, au CCM wajichague wenyewe. Katiba mpya haiwezekani kabla ya uchaguzi huo, labda ikubaliwe kusogezwa mbele.