Tuseme ukweli tu, Hayati Magufuli aliivuruga sekta ya ujenzi akiwa Rais

Ambapo yote hayo alikua anatimiza wajibu wake kwa sekta ambayo alikubali majukumu yote!!
 
Leo tumekusoma ndiyo maana una chuki zisizo na kichwa wala miguu kwa JPM
 
Siyo sekta ya ujenzi tu,aliivuruga nchi nzima. Alaaniwe hata huko jehanam aliko
Hili ndilo tatizo la watanganyika wengi,kila mtu anaitazama Serikali imwajili au imugawie kazi,akuna mtu mwenye ubunifu wa wasomi kujitajitafutia, mbona enzi za Mkapa na Kikwete hao wakandarasi walikuwa wanapata tenda mwisho wanazigawa kwa wageni wao wanapata 10/% uzuri wa Magufuri alikuwa anajua ukweli wote,hivo alivyoingia hakuangaika Sana hakaamua kazi kubwa awape tasisi za Serikali ili mtu akiboronga hatambana kwa sheria za utumishi,sio hao watu binafisi akibanwa anakimbilia mahakamani kupoteza mda, ndio maana Magufuri amefanya Mambo mengi kwa mda mfupi.
 
Ni sredi nyingi unaanzisha za kumnang’a JPM na nyingine zikizidi huwa tunakusitua. Kumbe matumbo yenu!
Sijaajiriwa na babaako.
Nimejiajiri ili tumbo lishibe.
Sasa ninyi mnaotegemea kodi ili mle tualikeni kula basi maana jomba lenu lenye roho mbaya limetueeka kijiweni.
 
Imugaiwie ×
Imgaiwie ✓

Kujitajifutia ×
Kujitafutia ✓

Punguza panic sukuma gang.
 
Uongo wa mchana.
Na inaelekea unababia tu vitu ambavyo huvijui katika sekta ya ujenzi.
Makampuni ya wapiga rangi nyumba za Halmashauri, nyumba za serikali na hata ukarabati wa mitambo midogo midogo, watu gani wa nje wamekuwa sublet.

Hilo ndo eneo ambalo wajenzi wote wameumizwa.

Taasisi za serikali TBA, SUMA-JKT, na wengine , hata Idara za serikali zenyewe zinasita kuwapa kazi baada ya kuboronga pakubwa.

You cant re invent the wheel in old age, matokeo yake ni chuki na taabu tu kwa wananchi.
 
Ndio maana wizi ukawa mkubwa sana, akawa anazitunza kwa bosi wa tanroad, alipodanja, bosi anaitwa kuulizwa, huu mpunga wote umeutolea wapi, serikali inautaifisha, aliposikia hivyo, presha ikapanda, akafa
 
Ndio maana wizi ukawa mkubwa sana, akawa anazitunza kwa bosi wa tanroad, alipodanja, bosi anaitwa kuulizwa, huu mpunga wote umeutolea wapi, serikali inautaifisha, aliposikia hivyo, presha ikapanda, akafa
Mkuu hao wapambe wa Magufuli hawajatueleza, alipata wapi fedha za kujenga Kebbys zHotel , jengo la ghorofa nafikiri nane au zaidi.
 
Endeleeni.

Mmeona huko hamueleweki Sasa mmehamia kwenye ujenzi.

Huku mtapigwa hadi mchakae.

Tuanchojua sisi Hayati alikuwa mtalaamu wa ujenzi nchi hii hatokaa akatokea.

Kwa hili hata mkijipa airtime zote.. hamtafanikiwa...hahaha.. kila Kona nchi hii kajenga Magufuli.
 
Umenena kwa uchungu sana mkuu.
 
Zamu yako kupalilia kaburi?
 
KILA KITU ALIHARIBU YULE MTU
 
Poleni mnaona mabaya tu mazuri yake hamyaoni barabara nyingi mnapita ila ni usimamizi wake thabiti ndo mnaziona mnajifanya hamuoni hata huko vijijini wazee wetu wanawasha umeme kwa bei chee vitu bei ilipungua ila sasa viko juu bado mnamsema yule mzee kwa mapungufu yake madogo wakati tz hata wakenya walianza kuogopa tutawapita ila sasa wanatucheka sana kwamba hatuna kiongozi mwenye vision.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…