Tuseme ukweli tu, Hayati Magufuli aliivuruga sekta ya ujenzi akiwa Rais

Tuseme ukweli tu, Hayati Magufuli aliivuruga sekta ya ujenzi akiwa Rais

Ungetutajia miradi 3 ambayo mlipewa mkaikamilisha...lazima wakandarasi wajiunge pamoja na kutengeneza makampuni yenye uwezo wa kupokea kazi...lazima tukubali kuwa wakandarasi mnahitaji kubadili mindset zenu kwanza ..ili kushinda tenda...mbona Estim wanapqta kazi na kupiku makampuni ya nje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkibishana miradi ya ujenzi muwage na akili basi.
Estim anapiga rangi nyumba za Halmashauri?
Estim anarepair mabomba ya majengo ya serikali?
Kazi kama hizo ndogo ndogo ndizo zinawaajiri makandarasi wazalendo.
Sasa ninyi mnaotoa mawazo kwa nini msiwe kama Kibajaji au Makamba kwa weledi?
 
Hapana alivuruga kila kitu. Acheni kuleta vi uchambuzi vidogo vidogo kupoteza muda. Hana jema na alivuruga nchi yote!
 
Poleni mnaona mabaya tu mazuri yake hamyaoni barabara nyingi mnapita ila ni usimamizi wake thabiti ndo mnaziona mnajifanya hamuoni hata huko vijijini wazee wetu wanawasha umeme kwa bei chee vitu bei ilipungua ila sasa viko juu bado mnamsema yule mzee kwa mapungufu yake madogo wakati tz hata wakenya walianza kuogopa tutawapita ila sasa wanatucheka sana kwamba hatuna kiongozi mwenye vision.
Kwa East Africa Tanzania tunaweza kuwa tunaongoza kwa kuwa na barabara nyingi substandard.
 
Kumnang'a ×
Kumnanga ✓

Punguza panic sukuma gang, au ni kweli kwamba ulikuja Tanzania kutoka nchi iliyopakana na Kigoma baada ya mjomba yako kupata Urais?
Kumbe nawe ni mpuuzi!
 
Hii akili yangu ndogo ni kubwa kuliko yako.
Na ubinafsi na roho mbaya kinara ni jamaa yako.
Na baada ya hapo jibu hoja siyo kubwabwaja tu.
Acha ubinafsi ndiyo maana unahangaika na micro issues badala ya macro issues.
 
Tulio sekta ya ujenzi bado hatujatengemaa kutokana na vurugu tulizopitia miaka hii mitano.

Kabla ya kupata urais Magufuli na sekta ya ujenzi tulikuwa chanda na pete.

Mikutano yote ya wajenzi alihudhuria tena kwa kujipigia chapuo kuwa kwa Rais iwe Mkapa au Kikwete.

Sasa alipopata Urais tukifikiri sasa tutakula bata!

WACHA!

Kwanza kazi zote za serikali akaamuru wapewe TBA, JKT-SUMA Magereza.

Consultancy zote zikaamriwa zifanyike Chuo cha ARDHI.

Hapo makampuni mengi tu yakafa, iwe ya ujenzi au ya consultancy.

Hatujakaa sawa Mwamba akaamuru kazi zote zifanywe kwa mtindo wa Force Account.

Kuna watendaji serikalini wakaenda mbali na kuwapiga marufuku makandarasi katika kazi zozote za Halmashauri au serikali!
Makampuni mengi yakafa mkupuo wa pili.
Sekta aikadhurika sana.

Sekta hii duniani kote ndio ina sambaza fedha kwa uchumi na umma, iwe vibarua, mama ntilie, mabenki na hata ulipaji wa kodi.

Mpaka sasa sekta haijatengemaa vizuri hata baada ya kuona madudu ya TBA, SUMA-JKT, MAGEREZA na vyombo vingine vya serikali ambavyo kuna sehemu vimefanya kazi chini kabisa ya viwango na havisambazi fedha kwenye uchumi.

Tukubali tu Magufuli aliivuruga sekta ya ujenzi akiwa Rais.
Alivuruga uchumi jumla wala sio sekta ya ujenzi pekee.
 
Miradi mikubwa walipewa/wanapewa makampuni ya kigeni hasa China.
Makampuni hayo yalileta/yanaleta subcontractors kutoka kwao.Asili mia kubwa ya fedha za miradi mikubwa ya ujenzi inarudi kwao.
Laiti kama masharti ya mikataba ya ujenzi kwa miradi mikubwa yangewahusisha makampuni ya kizalendo yenye vigezo,fedha angalau asilimia 60 zingebaki nchini na mzunguko wa fedha ungeimarika.
Wachina sio muarobaini wa kujenga Tanzania bali ni kirusi kibaya kuliko saratani.
 
pamoja na yote hayo…Hayati John Magufuli ndio Mtanzania aliehusika moja kwa moja na masuala ya ujenzi wa miundombinu kuliko Raia yeyote yule

kwa Hayati Benjamin Mkapa alihudumu Kama Naibu wa ujenzi maika 5 na kama waziri kamil kwa miaka mitano…

kwa Jakaya kahudumu kama Waziri wa Ujenzi 5 years

kama Rais kahudumu kama Rais was Ujenzi 6 years

kwa ujumla kahudumu kwa miaka 21 na kafanya kazi kubwa Sana
Bado haikuwa tiketi inayomruhusu kufanya ufisadi. Ni kwamba jamaa alikuwa mbinafsi, katili na anataka apate peke yake. Rot in Hell Magufuli
 
Back
Top Bottom