Tuseme ukweli, uchaguzi wa CCM uliofanyika una viashiria vya udini

Status
Not open for further replies.
Pamoja na uchaguzi lakini uwakilishi ni muhimu pia uzimgatiwe na hapo ndio busara inatakiwa.
 
We nae tumekuchoka kila kitu udini udini chuki zako dhidi ya uislam hazitokufikisha popote wewe mtu wa Mara.......
 
Kwenye siasa hakuna msafi ila wapo wenye huruma tu
 

Mkuu hebu tuwekee safu/list ya viongozi wa CHADEMA ili tuone na kwenyewe kukoje
 
Ngoja nikuongezee, Mwenyekiti wa CCM Dar ni Abbas Mtemvu Mwislamu pia.

Ni hivi Wakristo tuna roho mbaya sana, natamani waislamu waongezeke kwenye uongozi kwa sababu ushahidi uko wazi waislamu hawapendi dhiki na dhulma.

Utawala wa Wakristo ni chuki tupu, roho mbaya na kuuwa watu, waislamu wameprove utu kwenye utawala wao ukianzia Mwinyi, Kikwete na Samia.

Mkapa na Magufuli ni mfano wa shetani.
 
Huo ndio ukweli na inaonekana agenda kuu ya mama ni kupromote dini yake na Uzanzibari.
 
Haya mawazo hayatakiwi kuwepo kwa wa Tanzania. Pia, walio na madaraka hawaruhusiwi kufanya mambo yanayoweza kuleta mawazo ya udini katika vichwa vya wa Tanzania.

Ningewashauri kabla ya kuanza kazi wachaguliwa ndani ya CCM, chama kiwapeleke Hijja ndogo Macca inatwa sina hakika ummrah.

Na Wakristo ambao ni Wanachama wa CCM wajitafakari na waishinde dhambi ya unafiki.
 
CCM siyo jumuia, kigango, Parokia wala Jamaati. wanachama wa CCM wamechagua viongozi wanaowataka.

By the way wakati Magufuli anajaza Wakiristo serikalini mbona hizi kelele hatukuzisikia?
Zilikuweko lakini haukutaka kuzisikia. Magufuli alilaumiwa kwa vyote, udini na ukabila. Kama vile ambavyo Chadema inalaumiwa. Ukweli ni kuwa wako watanzania wengi ambao dini na kabila ni vitu muhimu kwao. Kwenye hili la sasa ni vigumu kuona namna gani huo upendeleo ulifanyika. Wanachotakiwa kufanya viongozi wetu ni kuonyesha kwa vitendo kuwa hizi shutuma ni za kipuuzi kwa kuongoza bila kuangalia dini au kabila la anaowaongoza. Wachina wanasema " haijalishi rangi ya paka, kilicho muhimu ni kuwa anakamata panya".

Amandla...
 
Acha uongo Mwenyekiti Baraza la wazee ni Muislam

Mwenyekiti BAWACHA ni Sharifa Suleiman Muislam

BAVICHA uchaguzi uliopita
Makam mwenyekiti Moza Ally Muislam
Katibu mkuu Nusrat Hanje Muislam
Hapo sijataja naibu mwenyekiti na naibu Katibu kwa upande wa Zanzibar ambao nao wote ni waislam.

So Mkristo alikua Kaunya na Pambalu peke Yao kwenye nafasi almost 8 za Bavicha kitaifa!!!
 
Waislamu walipokuwa wanalalamika kuhusu udini wa Magufuli mlikuwa mkimtetea kuwa hatuteui masheikh wala mapadri

Sasa kwenye chaguzi hizi za ndani ya CCM utalaumu udini kivivipi wakati watu wamechaguliwa kwa kura?

Na waliogombea walikuwemo watu wa dini zote!

Nadhani wana CCM wameamua kuchagua watu wanaowataka. Hayo ya kuangalia dini ya mtu hayamo katika miongozo , katiba na kanuni za CCM.

Kama mnataka habari za kubalance dini za watu katika teuzi, ajira, na fursa mbalimbali serikalini basi tuliweke katika katiba mpya au sheria zijazo. Lakini kwa sasa liko kama lilivyo
 
Hizi kelele za udini huwa zinapigwa sana pindi mtawala anapokuwa muislamu, lakini Mtawala anapokuwa Mkiristo na akateua wakiristo wenzie zaidi ya 80% huwa anapata utetezi kutoka kwa hawahawa wanaolalamikia udini leo

Hizi mada za kupiga mbinja kelele za udini pindi mtawala anapokuwa muislamu hazijaanza leo humu JF

Cheki hii mada ya 2007 hapa chini👇

 
Kwa hiyo kwako wewe kelele mpaka zipigwe na wakristu ndio unazisikia? Magufuli alipingwa na alikosolewa na wakristu wenzake wengi tu wakishirikiana na waislamu. Sasa hivi wengi wa waislamu waliokuwa critical wakati ule ama wamenyamaza, wamepunguza sauti au wanakataza asikosolewe kabisa.

Mimi sio msemaji wa wakristu lakini sikubaliani na wazo la kubalance dini katika jambo lolote. Ndio maana waislamu kuwa wengi katika uongozi hakunisumbui kama vile ambavyo sikusumbuliwa wamisheni walipojaa katika nafasi za uongozi.

Kipimo kwangu mimi ni namna gani viongozi hawa watawatumikia watanzania wote bila kubagua au kupendelea kwa misingi ya dini, kabila, eneo alilotoka na jinsia. Ninachotaka wakamate panya wanaonisumbua. Rangi na dini yao sio muhimu.

Amandla....
 
Naona unachanganya kachumbari na kande kidogo

Mwenyekiti wa BAWACHA aliyepita ni Halima Mdee Mkiristo

Mwenyekiti wa BAVICHA ni Pambalu Mkiristo, yupo mpaka Sasa
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…