Kwanza tume huru sio jambo la kuikalili tu,hiyo tume huru haigozwi na Malaika wa mbinguni wala Ummoja wa nchi za Ulaya au Marekani. Tume huru ni kundi la watu tena Watanzania wanaongoza taasisi ya serikali.Hakuna jambo jipya mpaka hapo.
Je nani atapima weledi wa tume hiyo kama si mahakama zetu?
Huko Kenya walijitambulisha kama wametunga katiba mpya na kuunda tume huru.
On paper tuliwaona wapo juu licha kucopy na kupaste katiba ya Marekani.
Lakini ebu twende reality check ni ngumi,mapambano ni maadamano ya kumwaga damu kwa maefu kila uchaguzi mkuu.
Ni vurungu kwa jina la tume huru,ni kusweka ndani na kuzota jela,ni kesi zisizoisha mahakama kuu kila uchaguzi na latest ni vurugu za Gen Z zilizopoteza maefu ya maisha na kupotea au kuangamiza mali za wananchi.
Hakuna tofauti ya mlalamika na mlalamikiwa,wote wakipata nafasi ni chumia tumboni,bora mimi akina pangu pakavu.Mwisho wamehamia makanisani kutumia nyumba za Mungu kuhubiri ukabila,umimi na uzandiki,ndio Kenya ya leo ambayo anadaiwa hadi kiama.
Ni siasa za kilaghai kwa jina la demokrasia.
Kwa kumalizia kutaja tu tume huru bila componets zake kuzipima kuona mapungufu yake,ndio mambo ya kila mara kuunda tume akina Warioba ambazo by the end of day hazifanyi kazi ni wastage of public monies.
Wake up.