Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, Mwl. Nyerere hakuwa mwanademokrasia!

Walioandaa kinachoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ haikuwa ni kongamano bali ni mkusanyiko wa wapiga propaganda zenye unafiki.
Hili lilikuwa kongamano lao, kwa nini uwapangie cha kufanya.
Nenda na wewe kaandae la kwako uwaalike unaotaka waje kuwasilisha mada. Shida ipo wapi?
 
Nyerere alikuwa dikteka kwa sababu moja tu. Kura za maoni wengi walichagua kuendelea na mfumo wa chama kimoja...demokrasia inatuambia alipaswa kufuata maoni ya wengi, hata kama hawako sahihi.
 
Nyerere alikuwa dikteka kwa sababu moja tu. Kura za maoni wengi walichagua kuendelea na mfumo wa chama kimoja...demokrasia inatuambia alipaswa kufuata maoni ya wengi, hata kama hawako sahihi.
Unaelewa maana ya neno Demokrasia???
 
Na ni hawa hawa, "vijana waliotumwa kijiji cha pili wakahemee, kuepusha njaa iliyokikumba kijiji chao kisiangamie;" badala yake wakawa ndio maadui wakubwa wa kijiji chao na kuharibu kila mradi waliopewa kuuendesha!

Leo hii wanakuja hapa na kujibaraguza kwa kushindwa kwa kutekelezwa kwa ufanisi mipango mingi ya maendeleo iliyowekwa, na kutoa shutuma kwa mtu mmoja kana kwamba ni yeye pekee aliyetakiwa kutekeleza kila sera iliyotungwa.

Na wakati huo huo, mtu huyo anayejidhani anazo za kumtosha anashindwa kujiuliza inakuwaje mtu huyo huyo aliyeondoka miaka 29 iliyopita bado anakumbukwa na kuthaminiwa na watu aliowaongoza kwa miaka yote ile.

Hataki kujiuliza na kulijibu hilo.
 
Kiongozi yupi ni mwana demokrasia? Tupe mfano.
Halafu lengo lako ni lipi? Au umeamua tu kumjadili J.K.Nyerere (RIP)
 
By then, Foreign Policy ya TZ ilikuwa ni kutofungamana na bloc yoyote (East au West).

Huo ni unafiki mwingine

Unapokea mafungu ya urusi kupiganisha vita Africa

Unasimama kidete kutetea Wajamaa kupata kiti Chan kudumu UN then unataka kuaminisha watu Wewe ni ‘Non aligned Movement’
 
Ukiulizwa tetea kuwa Nyerere alikuwa Mwana Demokrasia jibu lake ndio hilo kuwa tuangalie nyumba yake Butiama?
Mkuu;
Nimesoma maoni yako nikacheka sana!

Kuna baadhi ya watu mnajua kujibu hoja!

Akirudi tena naomba unitag!
 
Mkuu;
Nimesoma maoni yako nikacheka sana!

Kuna baadhi ya watu mnajua kujibu hoja!

Akirudi tena naomba unitag!
Nikuulize tena???
Hivi unaweza kuwa Mwanademokkrasia wakati umejilimbikizia ukwasi wa Utajiri +Majumba ya Kifahari????
Wakati Wananchi wako ni Mafukara wa Kutupwa???
Ndo maana nikakuuliza
Unaelewaje maana ya Neno Demokrasia????
 


Uko sahihi.
Na pia, mijadala ya kumhusu huyu Mzee, inaharibiwa na watu wanaomtazama kidini. Kuna watu kadhaa wameanzisha threads hapa kwa vile tu wanamhusisha na upendeleo/uonevu na dini fulani. As a result, most of them present seemingly objective views which are in reality subjective.
 

..wanatumia kichaka cha "kutukanwa" kufanya mambo mabaya kwa waTz wenzao ikiwemo KUDHALILISHA, na KUTESA
 
Nyerere ndiye architect wa kuharibu chaguzi za Zanzibar

Hata hivyo tunamsamehe kwa sababu ndiye muasisi wa Taifa hili jambo hilo ni kubwa mno kuliko makosa aliyotenda akiwa madarakani
hebu elezea hapo kwenye uasisi wa taifa hili,huwa sielewi,maana mipaka ya nchi hii walichora wazungu
 
Kuna haja kubwa ya kutangaza mabaya ya mwalimu kuliko hata mazuri yake. Leo CCM wanaogopa kujitangaza kuwa siyo chama cha ujamaa kwasababu ni kama kumpinga mwalimu japo wakina Serukamba et al hawaamini tena ujamaa. Hilo linatuathiri wote, tuna taasisi za kijamaa kwenye ulimwengu wa kibepari. Hatuwezi songa mpaka tutakapoacha kuongozwa na mzimu wa Mwalimu.
 

..pamoja na mtizamo hasi ulionao dhidi ya TL ktk hoja hii mawazo yenu yanafanana.😁
 
Nyerere alishasema tunachukua mabaya yake na kuacha mazuri yake. Alishatuambia tunalikatiba libaya cha ajabu akatuachia likatiba hilo hilo na uchama dola wa CCM ambao sasa unatupa shida. Kuhusu demokrasia sijui nitamuweka wapi lakini watanzania walimuita "Mzee haambiliki" na waliompinga tunajua yaliyowakuta. Sasa kwenye midahalo wasemaji wanachaguana wao kwa wao ndiyo maana upande wa pili huwezi kuusikia. Tofauti kuu ya Nyerere ambayo hufanya watu wafunge macho ni hakuwa mbinafsi wa maendeleo ya familia wala nchi style ya project Bagamoyo na Project Chato acha familia za viongozi wetu etc.
 
Huo ni unafiki mwingine

Unapokea mafungu ya urusi kupiganisha vita Africa

Unasimama kidete kutetea Wajamaa kupata kiti Chan kudumu UN then unataka kuaminisha watu Wewe ni ‘Non aligned Movement’
Ita unafiki, wenye uelewa tunaita 'bloc politics'...
Ita kupokea mafungu kupiganisha vita, wenye uelewa tunaita TZ's Foreign Policy.. liberation of fellow african countries
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…