Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, Mwl. Nyerere hakuwa mwanademokrasia!

Ukiwa shabiki wa chama chochote cha siasa (wewe mmoja wapo) tayari unakuwa mnafiki. Hii nchi inahitaji wagombea binafsi labda itasaidia kufungua watu macho na kuishi kwenye ukweli.
 
Nyerere alikuwa Dikteta Mnafiki
Upande mmoja alikuwa kibaraka wa Urusi na China upande wa pili alikuwa Kibaraka wa Mabepari kuzuia Znz isiangukie kwenye Ukomunist
Znz imeungana na bara Kabla ya azimio la Arusha
 
Ukiwa shabiki wa chama chochote cha siasa (wewe mmoja wapo) tayari unakuwa mnafiki. Hii nchi inahitaji wagombea binafsi labda itasaidia kufungua watu macho na kuishi kwenye ukweli.

Unadhani mimi kuwa shabiki wa chama basi naunga mkono kila jambo la chama? Pigania basi huyo mgombea binafsi, au unadhani wenye vyama watukupa mgombea binafsi?
 
Unadhani mimi kuwa shabiki wa chama basi naunga mkono kila jambo la chama? Pigania basi huyo mgombea binafsi, au unadhani wenye vyama watukupa mgombea binafsi?
Huwezi kuwa shabiki wa chama kama huungi mkono sera zake -nzuri na mbovu. Wagombea binafsi watakuja tu.
 
Huwezi kuwa shabiki wa chama kama huungi mkono sera zake -nzuri na mbovu. Wagombea binafsi watakuja tu.

Huenda hujui tofauti ya shabiki na mwanachama. Tafuta Kamusi ya kiswahili uongalie tofauti ya shabiki na mwanachama, kisha uje tuendelee na mjadala.
 
Huenda hujui tofauti ya shabiki na mwanachama. Tafuta Kamusi ya kiswahili uongalie tofauti ya shabiki na mwanachama, kisha uje tuendelee na mjadala.
Sihitaji kamusi, ujumbe umeshakufikia.
 
Ndio!
 
Mwalimu alikuwa na upungufu wake na mara kadhaa alikiri kufanya makasa kama binadamu. Alipata kuwashangaa kwa kung'ang'ania mambo ya ovyo aliyofanya na kutupa mazuri.
 
Mkuu;
Sijaelewa hoja yako! Nielimishe zaidi!
 
"MsemajiUkweli, post: 33260843, member: 91662"]Wangeweza hata kumuarika
Kumuarika= Kumualika Kinachokukera ni kusikia mazuri ya Mwalimu yakielezwa hivyo huenda yakafunika mengine au kutuonyesha matundu mengine.

Tayari kuna pande mbili!
Upande wa kwanza ni ule unamtuhumu Mwalimu kwa kutojenga ''Vituo vya afya 300 hata kama hatukuhitaji''.

Ni ule usiosema changamoto na mafanikio ya Mwalimu
Upande huu hudhani Tanzania ya 1961 ni sawa na ya 2019 ambako wasomi hawana kazi
Hawaelewi Tz ya Mwalimu kumpata mkuu wa Wilaya ilikuwa taabu sana

Upande huu wa kwanza unamhukumu Mwalimu kwa kujenga taasisi na miundo mbinu kwa kumsumanga tu. Hauelezi Mwl alifanya nini kiuchumi, kijamii na kisiasa!

Kwa ufupi Mwalimu akiwa amepumzika kaburini anatukanwa na kusumangwa na upande huu wa kwanza ili kumshushia heshima na hadhi yake. Kufanya hivyo kutarahisha kazi nyingine...

Upande wa Pili ni huu wa Kongamano la Mwalimu.
Upande huu umeishi na kuona ya Mwl, wanachokifanya ni kusahihisha upotoshaji unaoenezwa kuhusu Mwl na upande wa kwanza

Hivyo Kongamano linajibu kadhia, indhara na matusi dhidi ya Mwalimu
Ni kongamano linalomsemea Mwalimu kutoka kabarini

Hadi hapo matusi, indhara, kadhia na kashfa dhidi ya Mwl zitakapoachwa, tutaona Mwl asiyeweza kujitetea kwa kuwa ni marehemu akitetewa na waliomfahamu

Utetezi wa Mwl anayehukumiwa hauhitaji pande mbili, huu ni uetetezi unamweleza Mwalim
 
..ilibakia kidogo waTz tuanze kula NYASI.

..na kungekuwa na uhuru wa kisiasa, au wenye mawazo mbadala wangepewa nafasi ya kuzungumza na wananchi, nadhani nchi ingechukua muelekeo tofauti.
Ninakubaliana na angalizo lako.
 
Tanzania ilikuwa ni nchi isiyofungamana na upande wowote katika siasa za kidunia na kwa misingi hii hakukukwepo na threat za mataifa makubwa!
 
Mkuu;
Hoja yangu sio kufanya ulinganisho na waliomtangilia au waliokuja baada yake bali ni kuchambua maisha ya Mwl. Nyerere kama kiongozi anayedaiwa ni mwanademokrasia.
Siku za nyuma tulikuwa na mijadala ya kuchambua mazuri na mabaya.
Nipo katika rekodi nikieleza mapungufu yake na kusema alikuwa mwanadamu kama wengine

Kinachotokea sasa hivi ni jitihada za makusudi kabisa za kumweka Mwl katika mizani na viongozi waliofuata ili kuona atakayevaa viatu vyake.
Haiwezekani kufanya hivyo kwa wingi wa mazuri yake ukilinganisha na mapungufu na kwamba mazingira ya wakati wake si ya leo.

Ukimsoma mleta mada vizuri utaona hilo na amekereka sana Kongamano kuongelea mazuri yake. Anachotaka ni kuongelea mabaya yake ili iwezekane kumweka katika mizani na waliofuata.

Kwa upande mwingine, Kongamano ambalo wazungumzaji ni wanafunzi wa Mwl wanaona kuna upotoshaji. Hivyo, katika kumuenzi Kongamano linamwelezea Mwalimu kama kuwajibu wanaomkejeli ambao kwa bahati nzuri ni CCM

Katika hali ya kawaida Kongamano lingekuwa na kazi ya kuchambua yote yanayomhusu Mwl.
Kwa mazingira yaliyopo kongamano linajaribu kumtetea Mwl kama reaction ya kejeli zinazoelekezwa kwake na CCM wa leo hii
 
Kama unataka Mwl. nyerere aachwe apumzike basi wambie wale wanaoandaa makongamano ili tumjadili waache kuandaa hayo makongamano.

Hoja yangu isingekuwepo kama kusingekuwepo na makongamano ya kumchambua mwl. Nyerere kama binadamu na kiongozi wa juu wa Tanganyika na Tanzania.

Please, don't shoot the messenger!
 
Mwalimu alipenda sana vitu vifuatavyo

1. Uafrika
2.Ukatoliki wake
3.Madaraka yaani power
4. Utu

Maamuzi yake mengi yalibase kwenye kimoja kimoja katika vitu hivyo au combination ya atleast vitu viwili katika listi ya vitu hivyo.

Sometimes ukatoliki wake ulimzidi nguvu kwa mfano Kutuingiza kwenye mgogoro dhidi ya Nigeria sababu ya yeye kuwaunga mkono waasi wa Kikatoliki wa Biafra ili wajitenge dhidi ya Shirikisho la Nigeria

Wakati Mwingine alisukumwa na utu na Uafrika kwa mfano kupigania ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika

Wakati mwingine alisukumwa na kupenda sana power ndiyo maana alijua katiba ya mwaka 1977 inaweza kutumika kidikteta effectively lakini hakufanya juhudi za maana kuleta iliyobora zaidi, aliishia kuweka viraka vya hapa na hapa baada ya kustuka kuwa atamwachia Mwinyi nchi ili kumbana asiwe na mamlaka kama yeye, kwa mfano kuweka ukomo wa madaraka mwaka 1984 na pia kuweka bills of human rights mwaka 1984
 
Hakuna binadamu aliyekamilika akiwemo mleta mada, lakini kwa Hawa Viongozi tulionao baada ya NYERERE ndio wangeanza wao, Tanzania ingekuwa na Rais mmoja hadi sasa au marais 20 kama Uganda

Pia Kwa makabila mengi tuliyonayo nchi ingekuwa imeshagawanyika kama sudan

Kuhusu Demokrasia, Naamin mleta mada ungepata référence za nchi nyingi afrika miaka hiyo

Halafu nyie, msituletee Demokrasia ya magharibi ambayo ni ya kinafiiki ndio itumike kama référence, Demokrasia ni pana na inatumka Katika Jamii ambayo wao wanaona inafaa

Mleta mada na genge lenu chuki zenu, hazitafanikiwa na kila Mwaka NYERERE ataenziwa na vizazi kama Baba wa Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…