Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, Mwl. Nyerere hakuwa mwanademokrasia!


Kwahiyo TL yeye ndio yuko perfect?
 
Hata mwigulu nchemba naye ni mnafika, ... Duh! Sorry! Kumbe hapa tunamjadili Mwl Nyerere!
 

Sasa mfumo wa ujamaa na demokrasia wapi na wapi.Sawa na maji na mafuta havichangamani.Mwalimu hakuwa mwanademokrasia ni baada ya kung'atuka.Hata speech zake nyingi zilikuwa zikiyaponda aliyoyafanya.Mwalimu aliweza dhibiti mabaya yake yasiweze julikana alifaulu sababu za kutokuwepo kwa technologia ya mawasiliana tofauti sasa wameshindwa kudhibiti teknologia ya mawasiliano sababu hawaimiliki.
 
Mimi nilijua umeandika huo upande wa pili wa mwl Nyerere
 
Katiba aliyoiasisi ndio imeleta udikteta japo alionya bila kufuta vipengele vya kidikteta.Hii katiba ni ya kijamaa ilikopiwa toka kwa dikteta Mao wa China aliyekuwa Swaiba wa Mwalimu.Ujamaa na udikteta ni sawa na sukari na chai ujamaa na umasikini ni sawa na sukari na chai.Lengo la ujamaa ni kutawala watu na sio kuongoza watu.Ujamaa unapingana na demokrasia,Ujamaa katu hauruhusu mawazo huru (challenge) bali fikra za mwenyekiti
 
Ukiulizwa tetea kuwa Nyerere alikuwa Mwana Demokrasia jibu lake ndio hilo kuwa tuangalie nyumba yake Butiama?
Ishu ya nyumba ni itikadi za kijamaa si demokrasia, ujamaa upingana na maendeleo.
Maana ya democracia ni
-Haki za binadamu
-Uhuru wa watu
-Ushirikishwaji wa watu kwenye maendeleo yao
-Uchumi huru watu wawe huru kumiliki Mali
-Utawala wa sheria
-Ushiriki huru wa vyama vya siasa ( kazi ya vyama upinzani ni kusukuma maendeleo kwa kuleta changamoto na mawazo mapya ili serikali isilale)
-Nk.
 
Alishaona upepo wa mabadiliko na mbinyo wa jumuia za kimataifa baada ya kuanguka na kushindwa kwa mfumo wa kijamaa duniani,hivo hakuwa na chaguo.
 
Nyerere alikuwa cold blood dikteta ayeweza itumia vizuri akili yake kwa hapa Mungu alimjalia kipaji hiki cha kutoumiza watu,alitumia akili zaidi tofauti na pure dictator mfano kina Mao,Hitler,Mobutu,Kamuzu Banda,Saddam, nk hawa walitumia zaidi nguvu kuliko akili.Mwalimu alifuta vyama vingi na kuzuia shughuli za kisiasa nchini,watu wenye mawazo tofauti walifungwa waliwekwa kizuizini mfano Kina Kambona,James Mapalala,Tuntemenke Sanga,Bibi titi,Abdul jumbe,Kassanga Tumbo,Maalimu Sefu list ni kubwa,haya ya misukosuko ya kina Mbowe na chadema ni copy na paste yalikuwepo.
 
Mimi nilisoma bure mpaka college na vichere juu. Kazi ulikuwa unapewa barua siku unamaliza chuo. Vyakula tulikuwa tunakula vya 3 star.

Je ilikuwa lazima tulazimishwe kuwa na kadi za Tanu baadaye CCM kwenda elimu ya juu? Kuna wengine hata hamu ya siasa haipo ila tulilazimishwa kuhudhulia mikutano ya wakubwa wakija bila kwenda adhabu. 75 tulipigishwa kura kwa nguvu ila hapo ndo kasheshe ukienda kwenye kumbukumbu ndo mwaka alipata kura chache kuliko miaka ya nyuma.

Saa nyingine huwa nahisi hawa watu wa chini ya mwalimu walikuwa na nidhamu ya woga kama hawa wa sasa ambao kila kitu lazima waanze na "Hii serikali ya JPM haina msalie" kila siku misifa bila kuangalia impact yake.

Je wale waliosombwa kupelekwa kwenye mapori eti vijiji vya ujamaa na wengine barabarani, wanasemaje?
 
Makongamano lazima yawepo, yule ni ndie Tanganyika na Tanzania kiujumla..

Ni kama Leo hii uwambie wachina wasimkumbuke Mao, wala wasiazimishe kifo chake na kuyaishi alioyaona yafaa licha ya mambo mengi alioyafanya...

Yani wewe u mpuuzi fulani ambae hujui wataka nini na huna point.. Kisa makongamano ndo uchukie?

Hebu jiulize, kama Mwinyi na Mkapa wangeendeleza ya Mwalimu, leo hii usingejaji uzuri wake.

Afrika nzima inamheshimu, tafadhali, acha apumzike huko aliko
 
Nyerere aliweza toa hizo huduma bure sababu alikuwa bado ana hazina ya kutosha ya pesa na mifumo ya uzalishaji iliyoachwa na wakoloni. Lkn si kwamba aliweza chochea uzalishaji vingi vilikufa walipoondoka wakoloni, hata ukitazama exchange rate ya shilling na dola haijawahi kupanda baada ya Uhuru imekuwa ikishuka baada ya wakoloni kuondoka na uzalishaji wa kukuza pato la taifa ulizidipungua na haujawahi ongezeka kuendana na idadi ya watu na kupelekea umasikini kuongezeka.Hata Mugabe mwanzoni alimudu kuendesha nchi sababu ya ziada ya hazina ya Ian Smith hakuwa chochea ukuaji wowote wa uchumi baada ya Uhuru waliweza tumia walivyokuta sio walivyowezalisha.Kwa Africa ni Ghadafi tu kidogo na nchi hizi za waarabu waishio Africa kama Egypt, Tunisia, Morroco, ndio kwao Uhuru una maana kwao wameweza piga hatua za kimaendeleo baada ya Uhuru.
 
Nakuunga mkono ingawa nadhani Nyerere alikuwa na discipline kwenye matumizi ingawa waliochini yake walikuwa wanamdanganya saana.

Viwanda vyote alivyofungua na kuendeleza vililiwa baada ya yeye kuondoka madarakani. Alitunyamazisha saan nakubali ila aliweza kuona mbali na kupeleka vijana kusoma nje esp. Western countries kama US, Canada, UK ingawa alipeleka wengi USSR. Mimi simtetei kwa udictator wake baada ya kusoma story ya Mw. Ludovic Mwijage alivyoteswa. Kuna Dr. mmoja alikuwa Dr. wake naye wa Bukoba mpaka mazishi yake hakuna aliyejali. Yule mzee ali fall kwenye ile hearsay ya watu waliomzunguka Mwalimu. Wote wameshakutana huko sijui nani anajitetea kwa nani? For centuries history has been repeating itself. Hawa watu hawakosi kila muongo.
 
Kilichomsaidia Mwalimu asiwe pure dictator anayeuwa watu kama blood dikteta wengine, ni malezi bora aliyopata utotoni na kusoma shule za dini zikamshape akawa na utu na hofu ya Mungu.
 
Huo uzuri wake uliousema na wenzio wanausifia ni kwasababu aliwadhibiti hao wanao wanaompinga. Huwezi kuwa mzuri kwa mtu uliyemdhibiti asijilimbikizie mali.
Kauli yako inaonesha kuwa hata mtoto aliyezaliwa na mama akiwa Shuleni awe tayari kulaumu mama yake kwa kufanya tendo hilo akiwa Shuleni na atasema hiyo ndio dosari ya mama yake.
Iwapo bandiko hili ni wivu wa kuona sifa za Nyere zimemzidi mbali sasa kiongozi mnayemnathibisha naye, nakupa pole. Tambua haya mazuri yanayofanywa sasa kuna makundi kadhaa yameathirika
Wanakongamano wapo sahihi sana Nyerere ni kiongozi wa karne
 
Kilichomsaidia Mwalimu asiwe pure dictator anayeuwa watu kama blood dikteta wengine, ni malezi bora aliyopata utotoni na kusoma shule za dini zikamshape akawa na utu na hofu ya Mungu.
Ndo maana wale wenye uelewa wa utakatifu wanamfananisha vile. Mimi ni mkatoliki 100 ila nina walakini na mwenye heri wetu. ingawa history and reality collide tuache yanayokuja. Ukiishi na watu wasioamini ukristo unakuwa na mentality tofauti na ukristo.
 
Kuna kongamano nchi hii utathubutu kuweka madhaifu ya Nyerere ueleweke? Kuweka mapungufu ya Nyerere hadharani ni kama tusi fulani hivi. Hata wanaoujua ukweli hawathubutu maana ni kama mungu fulani. Hiyo hunifanya nione Watanzania 90% ni wanafiki.
Nadhani kutowakaribisha wale wenye mtizamo mwingine tofauti kuhusu maisha ya Mwi. Nyerere hakuwezi kuondoa ukweli kuwa Mwl. Nyerere alikuwa na mapungufu kama binadamu.

Waandaaji wa kongamano wanafanya kosa kudhani kongamano ni sehemu ya propaganda wakati Mwl. Nyerere hatunaye!
 

Tatizo sio hao waandaaji wa kongamano maana tayari wao hayo wanayoongea ndio wanayoamini. Tatizo ni pale litakapoandaliwa kongamano na watu wakazungumza ukweli wote mpaka upande wa pili wa shilingi, wataibuka hawa wapiga propaganda kuwa Nyerere anatukanwa.
 
Nyerere alikuwa Dikteta Mnafiki
Upande mmoja alikuwa kibaraka wa Urusi na China upande wa pili alikuwa Kibaraka wa Mabepari kuzuia Znz isiangukie kwenye Ukomunist
Hili neno "mnafiki" linatumika isivyostahili.

Mtu mwenye unafiki kama wewe na kundi unaloliwakilisha ni upuuzi kumpachika sifa ya unafiki mtu aliyeona na kutambua unafiki wenu tokea mwanzo na akawakomesha.

Wakati huu hamuwezi kuhaada watu wasitambue unafiki mliokuwa nao enzi hizo.
 
Mimi nafikiri udumavu wa demokrasia nchini tusimulahumu Mwalimu Nyerere ambaye aliyekuwa anatawala kwa kwenda na wakati.Pamoja na kutumia mfumo wa ujamaa na kujitegemea yeye alitekeleza siasa hizo kwa dhati bila ya ubaguzi,wala unafiki.Kama watu nikusoma bule kuanzia primary mpaka University,matibabu bure nk.Kama nikutaifisha majumba,mashule,ya makabaila,mabwanyenye hakubaguwa kwa kusema huyu ni mwenzetu wa chama changu TANU,au ndugu yangu,kabila langu au dini yangu.Ali establish viwanda tangible,alinunua ndege za Air Tanzania bila ya kuruka ruka vyote hivyo vimetokomezwa na sisi wenyewe .Mwisho aliona dalili au zama zimebadilika yakuendelea na mfumo wa chama kimoja akangatuka akatushauri tuwe na mfumo wa vyama vingi pia tubadiri katiba ya mwaka 1977 maana katiba inampa madaraka makubwa kiongozi kuwa mfalme .Je tangu Mwalimu atutoke mbona tume ignore yale aliyotushauri?
 
Wanayao kwa tafsiri zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…