Tusipobadili mfumo wa Elimu, kila mwaka tutajenga madarasa hadi viwanja viishe!

Tusipobadili mfumo wa Elimu, kila mwaka tutajenga madarasa hadi viwanja viishe!

Kila mwaka idadi ya wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza na kidato cha kwanza inaongezeka, na itaendelea hivyo kwa miaka mingi ijayo.

Kuongeza madarasa na kununua madawati mapya kila mwaka siyo suluhisho la kudumu.

Niwaombe Waziri wa elimu Prof Ndalichako na yule wa Tamisemi Dr Jaffo mkae pamoja kuangalia nini kifanyike ikiwemo kupitia upya mfumo mzima wa elimu.

Elimu......Elimu......Elimu.

Maendeleo hayana vyama!
Sasa mbonqa huna lolote lw maana uliloshauri? Unasema tu waangali3 mfumo, je kweny3 huo mfumo wewe umeona dosari gani hasa mahsusi? J3 ujenzi wa madarasa na madawati wewe hujaona kuwa kama sehemu ya suluhisho la hizo changamoto?
 
" siyo suluhisho la kudumu"
 
H
Wabongo wanafyatuana Sana.
Ndo maana kila mwaka watoto wanaongezeka.
Hilo nalo ni neno.Nchi tulikuwa milioni tisa miaka ya sitini sasa tuko zaidi ya mara 6 (600% plus)
Wakati wa Raisi Nyerere alijua kwenda na wakati kuanzisha UMATI(Uzazi wa Mpango) akisaidiwa na taasisi za Umoja wa Mataifa.
Nimemsikia Raisi Magufuli akihimiza kufyatua watoto kwa kwenda mbele,lakini ameishia kusema wingi ni mtaji bila kuonyesha huo mtaji wa uzazi bila mipaka.
Je Nyerere na Magufuli nani sahihi kwenye sera za uzazi?
Kwa mwendo huu usishange hao hao wakaja na sera ya mtoto mmoja.
 
Tukianzia kwako mkuu, wewe unadhan nini hasa kifanyike

Wewe ni sehemu ya tatizo la nchi hii. Sio kila mtu atakuwa polisi, hakimu na bwana jela. Sio kila anayetambua tatizo basi huyo huyo aje na suluhisho!! Kwani Mungu aliposema “Usiue” alikuwambia pia usiue kwa risasi, panga, jiwe, sumu nk?? Go beyond kutaka anayesema tatizo aseme pia na suluhisho, je wewe nafasi yako ni nini??

Turudi kwenye mada. Elimu isiyo na msingi sio kwa ajili ya kila mtu!! Elimu ya juu sio kwa ajili ya kila mtu. Moja ya njia za kupunguza kuwa na wahitimu wa elimu ya juu isiyowasaidia katika kupata ajira au hata kujiajiri - ni kuthamanisha elimu ya msingi. Ili anayemaliza darasa la saba awe na uwezo wa kuamua anataka au anaweza nini maishani mwake. Kupata mwanafunzi aliyepata chini ya nusu ya alama za jumla na kusema aende sekondari ni kupeleka tatizo ngazi ya juu bila kumsaidia.

Elimu ya msingi iwe ni elimu ya maarifa na stadi za maisha! Sio nadharia!!
 
Na hapo serikali inatulazimisha tuseme harafu baadaye hakuna madarasa.
Achana na hayo mbaya zaidi wanasema kujiajiri na wanao sema hivyo wameajiriwa.
Addition points
Kila mwaka idadi ya wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza na kidato cha kwanza inaongezeka, na itaendelea hivyo kwa miaka mingi ijayo.

Kuongeza madarasa na kununua madawati mapya kila mwaka siyo suluhisho la kudumu.

Niwaombe Waziri wa elimu Prof Ndalichako na yule wa Tamisemi Dr Jaffo mkae pamoja kuangalia nini kifanyike ikiwemo kupitia upya mfumo mzima wa elimu.

Elimu......Elimu......Elimu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Iko hivi kwa tathmini yangu,tatizo linaanzia kwa maafisa elimu kata.
Wao inapofika January wanatakiwa wafanye yafuatayo
1.afisa elimu kata aangalie Ana shule ngapi za msingi zenye darasa la Saba wangapi,kwa mfano Ana shule 7 za msingi Kila shule Ina wanafunzi wa darasa la Saba 60 ,maana yake 60*7 sawa na wanafunzi 420 wa standard seven, Hawa unaweka asilimia tisini watafaulu,maana yake 400 wataenda sekondari.
Unaangalia shule zako za sekondari hapo katani ni ngapi kwa mfano ziko 3,sawa,Kila shule Ina uwezo wa kuchukua form one wangapi? Mfano uwezo ni 300 wanafunzi,kwa hiyo 100 hawatakua na nafasi wakifaulu,unalipeleka, kwenye kikao Cha maendeleo ya kata na kwa afisa elimu na mkurugenzi umemaliza.
Wazo zuri lakini linahiaji maboresho. Akiangalia darasa la saba tu atakuwa amechelewa. Muda wa kujenga madara ya nyongeza hautatosha, Nashauri tathmini ifanyike kuanzia darasa la tano ili madarasa yajengwe kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa na si kwa njia ya zima moto.
 
Ongezeko la watu sio la kuangalia india, china nk ni la kuangalia sisi JE tunaweza kulibeba hili ongezeko.....
Uchumi wa mtu moja moja ukoje??
Je serikali inauwezo wa kulibeba hili tuchukue mfano mdogo ktk elimu??

China ongezeko la watu linaenda sambamba na ukuajinwa uchumi na teknolojia.. Tanzania je??
Ukuaji Wa uchumi China umekuja ivi karibuni wakishakuwa wengi mbona.
 
Mwisho kama elimu ya uzazi hatitolewa kwa baadhi ya maeneo TANZANIA tumekwisha.
[/

Hapo ndo napingana nawewe! Nchi haiwezi kuendelea bila watu! Wenye uwezo wa kuzaa wazaliane tu hili linchi ni likubwa mno na liko tupu
 
Kila mwaka idadi ya wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza na kidato cha kwanza inaongezeka, na itaendelea hivyo kwa miaka mingi ijayo.

Kuongeza madarasa na kununua madawati mapya kila mwaka siyo suluhisho la kudumu.

Niwaombe Waziri wa elimu Prof Ndalichako na yule wa Tamisemi Dr Jaffo mkae pamoja kuangalia nini kifanyike ikiwemo kupitia upya mfumo mzima wa elimu.

Elimu......Elimu......Elimu.

Maendeleo hayana vyama!
Leo umetisha mzee
 
Wape ushauri nn cha kufanya
 
Na mimi nilitaka kumkusha hicho hicho. Unajua viongozi wasio na maono ni maangamizi kwa Taifa. Tanzania sasa hivi moja ya sababu zinazofanya nchi ielemewe na mambo mengi ni hili suala la kuzaa hovyo. Ukiaenda uswazi huko majira ya jioni mitaani kuna vitoto kama sisimizi. Nchi kama watu wake wanazaa hovyo hovyo ni ngumu mno kupanga maendeleo. Halafu unakuta mtu anathubutu kuwahimiza watu ''wafyatue'' watoto eti ndiyo uchumi utakuwa!
Tatizo la shida Kama hizi linatokana na Sera mbovu za kidemografia ( demographic policies), tuanze kwa kuamua kudhibiti uzalianaji holela ili kuwe na takwimu halisi za vizazi na vifo.
Serikali ibadilike na kuamua kutoa agizo maalumu la wastani wa watoto katika kila kaya.

Tusiendelee kudanganywa na wanasiasa eti tufyatue tu, tutajenga madarasa kila mwaka mpaka tutachoka huku utegemezi na umasikini vikiongezeka.

Acheni ubinafsi na uoga kuhusu changamoto ya population hatuwezi kuitatua kwa kuacha kuzaa,tujifunze kutoka Nigeria, China na India kwani wao wanawezaje?!!!!!!
 
Kila mwaka idadi ya wanafunzi wanaoingia darasa la kwanza na kidato cha kwanza inaongezeka, na itaendelea hivyo kwa miaka mingi ijayo.

Kuongeza madarasa na kununua madawati mapya kila mwaka siyo suluhisho la kudumu.

Niwaombe Waziri wa elimu Prof Ndalichako na yule wa Tamisemi Dr Jaffo mkae pamoja kuangalia nini kifanyike ikiwemo kupitia upya mfumo mzima wa elimu.

Elimu......Elimu......Elimu.

Maendeleo hayana vyama!
Kuna haja ya kupitia upya sera ya elimu.
1. Elimu ya msingi iwe form four.
2. Elimu ya sekondari iwe form six na kwamba isiwe kumbakumba. Yaani ziwepo shule chache za sekondari na idadi ya wanafunzi iwe fixed. Wazazi watakao taka watoto wao ambao hawajafaulu kwenda sekondari wawe na uhuru kuwaleka private.
3. Vyuo vikuu navyo vidhibitiwe idadi ya wadahiliwa.
 
Back
Top Bottom